Kwa haya FIFA mmenidanganya

Danpol

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
5,727
Reaction score
8,918
Nilibahatika kumuona Thiery Henry niliwahi kujiita Ronaldinho namkumbuka Peter Schmeichel nimemshuhudia Xavi nilimpenda David Beckham, sikumfaidi Zizou vizuri, Nawakumbuka kina Shevshenko ,Kaka wote walikua wakali, nachojivunia ni kitu kimoja tu , Kuwashuhudia Liones Mess na Cristiano Ronaldo wakifanya vitu ambavyo kabla ya uwepo wao vilikua ni vitu vya kufikirika tu , hakuna alie amini kwamba vinaweza kutokea , nachosikitika ni kwamba wamebadili maana halisi ya mpira wa miguu , wameibadili tuzo ya mchezaji bora wa dunia[ Ballon D'Or] kua tuzo ya mfungaji bora wa Madrid na Barcelona mbaya zaidi vichwa vya Wendawazimu vimepewa jukumu la kumchagua wanaetaka atwae tuzo na sio banaestahili kutwaa tuzo, Leo hii anaetwaa tuzo ni aliefunga magoli mengi kuliko mwenzie na wala sio mchezaji bora, Nazikumbuka zama za kina Fabio Cannavaro Matthias Sammer, Michel Platini na wengine wengi najiuliza wangekuwepo uwanjani leo hii je wangepata hii tuzo? jibu ni hapana,

Ukiniuliza ni nini kilichomuweka David Luis kwenye kikosi bora cha dunia sina jibu na hata yeye hajui, Iniesta anafanya nini kwenye kikosi bora cha dunia ndio kabisa sielewi , Ukimuuliza Tony Kross ni nini kilichomuweka kwenye kikosi bora cha dunia hawezi kukujibu, Iniesta huyu sio wa kipindi kile , Davidi Luis & Kroos hawakua na namba za kudumu kwenye timu zao ( Chelsea & B Munich ) kabla ya kuhamia timu nyingine , Kombe la dunia Iniesta alirudi nyumban bado asubuh, David Luis licha ya kukosa namba Chelsea lakini pia aliliangusha taifa lake kombe la dunia , alikuwepo kwenye kikosi kilichofungwa 7, Je, waliyoyafanya ndani ya miezi hii minne ( august to December) n bora kuliko waliyofanya wenzao ndani ya mwaka mzima? Fifa inazidi wanazidi kunidanganya, Najiuliza tena , Kwanini Yaya Toure hayupo kwenye hiki kikosi? Nakuja kugundua bado ni kazi ya jopo la wendawazimu, Mchezaji bora wa bara la Africa , Club ya Manchester city na ligi ya Uingereza anakosa namba kikosi bora cha dunia?

Najiuliza , ni kigezo kipi kilichotumika kumpa tuzo ya goli bora James Rodriquez ? Kazi ya wendawazimu tena , waliamua kumpa tuzo walietaka ashinde dhidi ya aliestahili kushinda, Adidas na Nike wanaupeleka mpira wapi? Sioni sababu ya kuziita tuzo za mchezaji bora wakat wachezaji bora hawatunukwi , wanatunukwa wenye faida na Adidas au Nike , wanatunukwa wenye sura za Hollywood kwasababu za kibiashara ,

John Cruyff " Ballon D'Or? A bunch of journalists and people voting for their friends"

Mfumo ndio tatizo , ifike mahali mfumo ubadilike, mfumo uliopo wa kupiga kura unawakandamiza wanaostahili kupata tuzo, viwekwe vigezo na mashart atakae fit ndie mshindi, Ni kura hizi hizi zilitumika kumnyima tuzo Sneidjer 2010, kura hizi hizi zimemnyima Frank Ribery uchezaji bora wa dunia mwaka Jana , zimetumika kumnyima Manuel Neur haki yake mwaka huu , Kikosi bora cha dunia hakina mshambuliaji wa kati , kazi ya wendawazimu, Kikosi bora cha dunia kina washambuliaji wanne wa pembeni , wawil kulia wawili kushoto , tokea lini timu ikawa na four wingers? Nafasi ya Yaya Toure ndio iliibiwa hapa . Lakini utamlaumu nani? Kazi wamepewa wendawazimu

by Dan Pol
 
Natumaini umetumia Jicho la tatu kuyaona haya yanaoendelea.
Maswali yako mengi lakini ayana majibu kamili na hakuna wakutujibu.?
Kuna kipindi Mshidi wa sasa CR7 alitaka kususia kushiriki sherehe hizo.
Hili katika vitabu vyetu TAKATIFU tunaita ni FUMBO LA IMANI
 
Fifa sijui wanalipeleka wapi soka la dunia hii
 
hivo vitu vipo! ila vinafanyika kwa influence ya watu wenye masilahi ya binafsi kupitia Mpira.....Goli na James Rodriguez limenishangaza kuna goli Arjen Robben aliwafunga waspain....kuna Goli la van persie....bt Goli la Roben liko more interesting ! anafunga goli kwa kumkwepa kipa na mabeki 3 wanakaba Moira.....wamechange ladha ya soka
 
Goli bora lililkuwa la Robben au van persie....ni mtazamo tuu
 
Gafla fumbo LA imani likageuka na kuwasala ya salamu ronaldo nasasa akiamka anasali oo sala ya baloon d-or isitoke kin ywanimwake milele
 
Gafla fumbo LA imani likageuka na kuwasala ya salamu ronaldo nasasa akiamka anasali oo sala ya baloon d-or isitoke kin ywanimwake milele

hahahahaha
 

Bao zuri la mpira wa MIGUU
ni la JAMES RODRIGUES. Lile
la VAN PERSIE ni bao zuri la
SHAOLIN SOCCER. Ubora
umechangiwa pia na
mazingira ya kukabwa kwa
JAMES tofauti na ile free
header.
 
Bao zuri la mpira wa MIGUU
ni la JAMES RODRIGUES. Lile
la VAN PERSIE ni bao zuri la
SHAOLIN SOCCER. Ubora
umechangiwa pia na
mazingira ya kukabwa kwa
JAMES tofauti na ile free
header. Lile goli la yule dada
ni zuri pia kuliko la RVP

Ni saa sita usiku sasa
 
Unaanzaje kuComplain uwepo wa TONY KROOS kwenye hyo World XI??

and unasema KROOS hakuwa Starter pale Bayern last season????

Unamjua TONY KROOS uliyemuandika hapo???

Au ndo yale yale ya kuwafatilia wachezaji ambao hawachezi EPL kwenye UCL tu????

Complain kuhusu INIESTA na kina LUIZ lakin syo TONY KROOS asa kwa perfomance yake uwanjan last season na mafanikio alyoyapata!!!

mfatilie KROOS, umjue vizuri!
 
wewe mkuu unaonekana ni nguli wa madrid
 

Tony hakuna chaguo namba moja B Munich chin ya Pep Guardiola hasa mwaka Jana , Kawaja kua chaguo namba moja chin ya Carlo Real Madrid
 

Attachments

  • Ballorn D'or 2014.jpg
    187.1 KB · Views: 125
  • Ballorn D'or 2014.jpgg.jpg
    162.3 KB · Views: 114
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…