Kwa haya FIFA mmenidanganya

Kwa haya FIFA mmenidanganya

Tony hakuna chaguo namba moja B Munich chin ya Pep Guardiola hasa mwaka Jana , Kawaja kua chaguo namba moja chin ya Carlo Real Madrid

Tony Kroos alicheza game nyingi sana msimu uliopita na aliwasaidia sana Bayern na Germany kama unakumbuka game za champions league dhidi ya Arsenal,ManUnited na Real Madrid zote alicheza na World Cup alicheza karibia game zote.Tony anastahili kuwepo kwenye hicho kikosi
 
Mkuu unafatilia vema ....naona Canavalo , wambura, Norj, nae kafanya yake, natamani hadi kula za bunge la katiba zingekuwa wazi namna hii.
Inabidi ifike pahala tusiwe watu wa kulalamika tu coz watu walio wengi hawaangalii mtu amefanya nn hasa wanachoangalia ni kwamba wanampenda waliempigia kura
 
Tony hakuna chaguo namba moja B Munich chin ya Pep Guardiola hasa mwaka Jana , Kawaja kua chaguo namba moja chin ya Carlo Real Madrid

ImageUploadedByJamiiForums1421327133.440021.jpg
 
Hizi kelele za mfumo mbovu and blah blah mara zote mnazianzisha kwa mapenzi yenu binafsi na sasa ivi mmeanza tena sababu Messi kakosa naamini angechukua basi mashabiki wa CR7 wangekuja na analysis mbovu kama hii.
Mahaba yanajionyesha wazi wakati unajua mfumo mzima wa kumpata mchezaji bora wa Dunia tena uko wazi kabisa kwa mpenda soka hawezi kulalama eti CR7 kawa mchezaji bora mbele Neur lazima utakua na mahaba tu na chuki,kitu ambacho nafurahi hapa ni kelele za chura ambazo tembo hazimzuii kunywa maji,tulimnanga Blatter anambeba Messi ghafla tunalalamika mfumo sasa sijui mnataka tupige kura kama tunamchagua raisi.
Mkumbuke ni macaptain,makocha wa timu za taifa na waandishi nguli hawa wote ni wataalamu ndio wamefanya maamuzi haya kama Brazil wamempa timu Dunga na yeye kasema CR7 ame-deserve na sisi hatutaki inabidi washuke malaika kutuchagulia na tulivyo wabishi tutakataa mpaka aje Yesu.
1.Najua una-question kuhusu goli bora kisa MAHABA na kufuata mkumbo.
2.Lazima ukae kimya uwepo wa Di Maria kwenye World XI kisa MAHABA.
 
goli kama la rodriguez tutalishuhudia tena katika soka lakini goli la van persie thats a history written
 
Hizi kelele za mfumo mbovu and blah blah mara zote mnazianzisha kwa mapenzi yenu binafsi na sasa ivi mmeanza tena sababu Messi kakosa naamini angechukua basi mashabiki wa CR7 wangekuja na analysis mbovu kama hii.
Mahaba yanajionyesha wazi wakati unajua mfumo mzima wa kumpata mchezaji bora wa Dunia tena uko wazi kabisa kwa mpenda soka hawezi kulalama eti CR7 kawa mchezaji bora mbele Neur lazima utakua na mahaba tu na chuki,kitu ambacho nafurahi hapa ni kelele za chura ambazo tembo hazimzuii kunywa maji,tulimnanga Blatter anambeba Messi ghafla tunalalamika mfumo sasa sijui mnataka tupige kura kama tunamchagua raisi.
Mkumbuke ni macaptain,makocha wa timu za taifa na waandishi nguli hawa wote ni wataalamu ndio wamefanya maamuzi haya kama Brazil wamempa timu Dunga na yeye kasema CR7 ame-deserve na sisi hatutaki inabidi washuke malaika kutuchagulia na tulivyo wabishi tutakataa mpaka aje Yesu.
1.Najua una-question kuhusu goli bora kisa MAHABA na kufuata mkumbo.
2.Lazima ukae kimya uwepo wa Di Maria kwenye World XI kisa MAHABA.

Maana yako n ipi hasa , kati ya mm na ww mwenye mahaba n nani? au kwasababu Dunga kasema na mm nikubali? Iruhusu akili yako ifikirie usisubiri wakusaidie watu kufikiri , Unasema wao n wataalamu , n nan aliekuambia mie sio mtaalamu?

Uheshimiwe mtazamo wa mtu yyt yule .
 
Nilibahatika kumuona Thiery Henry niliwahi kujiita Ronaldinho namkumbuka Peter Schmeichel, nimemshuhudia Xavi nilimpenda David Beckham. Japo sikumfaidi Zizou vizuri, lskini Nawakumbuka kina Shevshenko, Kaka wote walikua wakali. Nachojivunia ni kitu kimoja tu, Kuwashuhudia Liones Mess na Cristiano Ronaldo wakifanya vitu ambavyo kabla ya uwepo wao vilikua ni vitu vya kufikirika tu. Hakuna aliyeamini kwamba vinaweza kutokea.

Nachosikitika ni kwamba FIFA wamebadili maana halisi ya mpira wa miguu, wameibadili tuzo ya mchezaji bora wa dunia [ Ballon D'Or] kua tuzo ya mfungaji bora wa Madrid na Barcelona. Mbaya zaidi vichwa vya Wendawazimu pale FIFA vimepewa jukumu la kumchagua wanaetaka atwae tuzo na sio anayestahili kutwaa tuzo. Leo hii anaetwaa tuzo ni aliyefunga magoli mengi kuliko mwenzie na wala sio mchezaji bora.

Nazikumbuka zama za kina Fabio Cannavaro Matthias Sammer, Michel Platini na wengine wengi najiuliza wangekuwepo uwanjani leo hii je wangepata hii tuzo? jibu ni hapana, Ukiniuliza ni nini kilichomuweka David Luis kwenye kikosi bora cha dunia sina jibu na hata yeye mwenyewe akiulizwa hajui. Iniesta anafanya nini kwenye kikosi bora cha dunia ndio kabisa sielewi. Ukimuuliza Tony Kross ni nini kilichomuweka kwenye kikosi bora cha dunia hawezi kukujibu.

Davidi Luis & Kroos hawakua na namba za kudumu kwenye timu zao ( Chelsea & B Munich ) kabla ya kuhamia timu nyingine. Kombe la dunia Iniesta alirudi nyumban bado asubuhi, David Luis licha ya kukosa namba Chelsea lakini pia aliliangusha taifa lake kombe la dunia , alikuwepo kwenye kikosi kilichofungwa 7, Je, waliyoyafanya ndani ya miezi hii minne baada ya World cup (august to December) ni bora kuliko waliyofanya wenzao ndani ya mwaka mzima?

Fifa inazidi wanazidi kunidanganya, Najiuliza tena, Kwanini Yaya Toure hayupo kwenye hiki kikosi? Nakuja kugundua bado ni kazi ya jopo la wendawazimu, Mchezaji bora wa bara la Africa, Club ya Manchester city na ligi ya Uingereza anakosa namba kikosi bora cha dunia? Najiuliza , ni kigezo kipi kilichotumika kumpa tuzo ya goli bora James Rodriquez ? nagundua ni Kazi ya wendawazimu tena. Waliamua kumpa tuzo waliyetaka ashinde badala ya kumpa aliyestahili kushinda.

Adidas na Nike wanaupeleka mpira wapi? Sioni sababu ya kuziita tuzo za mchezaji bora wakati wachezaji bora hawatunukwi. Wanatunukwa wenye faida na Adidas au Nike, wanatunukiwa wenye sura za Hollywood kwa sababu za kibiashara. John Cruyff anasema tuzo za mwanasoka bora wa dunia kupigiwa kura ni utaratibu wa kishenzi maana watu huwapigia marafiki zao. " Ballon D'Or? A bunch of journalists and people voting for their friends"

Mfumo ndio tatizo , ifike mahali mfumo ubadilike, mfumo uliopo wa kupiga kura unawakandamiza wanaostahili kupata tuzo, viwekwe vigezo na masharti atakayekidhi ndiye mshindi. Mtindo wa kura ni wa kipuuzi. We unadhani leo Toure akishindana na mchezaji wa ligi daraja la kwanza Uingereza kwa mtindo wa kura nani atashinda? Licha ya Toure kuwa bora lakini atashindwa kwa sababu hana watu wa kutosha kumpigia kura.

Hata waafrika tujikusanye wote wenye smart phones tupige kura, waingereza wakicomand system mara moja tu wanatuzidi kura mara milioni. So mtindo wa kupima ubora wa mtu kwa kura ni mtindo wa hovyo sana kuwahi kutokea. Ni kura hizi hizi zilitumika kumnyima tuzo Sneidjer 2010, kura hizi hizi zimemnyima Frank Ribery uchezaji bora wa dunia mwaka Jana , kura hizihizi zimetumika kumnyima Manuel Neur haki yake mwaka huu.

Cha kushangaza Kikosi bora cha dunia hakina mshambuliaji wa kati, kazi ya wendawazimu. Kikosi bora cha dunia kina washambuliaji wanne wa pembeni , wawil kulia wawili kushoto, tokea lini timu ikawa na four wingers? Nafasi ya Yaya Toure ndio iliibiwa hapa . Lakini utamlaumu nani? Kazi wamepewa wendawazimu!

Kilaza
 
Mpira wa miguu hauchezwi na mikono.
Neuer atatusamehe kwa hili
 
Umeongea ukweli mtupu…n wanafiki sana...na hawipendi ligi ya England
 
mbona umecopy na kupest mkuu ??

cc Dan Pol
 
Last edited by a moderator:
Hawa wanafanana na wale wa huu ukanda wetu wa nchi za A.mashariki na kati (cecafa),
 
mbona umecopy na kupest mkuu ??

cc Dan Pol

Fafanua Mkuu, kaiba kauli ya mtu mwingine? Kama ni kweli na kwa kuwa haku-acknowledge source bila shaka atakuwa amevunja kanuni za JF. Mods - kazi ni kwenu.
 
Last edited by a moderator:
Maana yako n ipi hasa , kati ya mm na ww mwenye mahaba n nani? au kwasababu Dunga kasema na mm nikubali? Iruhusu akili yako ifikirie usisubiri wakusaidie watu kufikiri , Unasema wao n wataalamu , n nan aliekuambia mie sio mtaalamu?

Uheshimiwe mtazamo wa mtu yyt yule .

Haaaaahaaa na wewe mtaalamu..??
Aya tuambie huo utaalam wako duh wa-Bongo tuna mbwembwe au ni mwandishi wa spoti starehe tehe tehe tehe piga kelele ila CR7 kafunga mjadala hautaki andamana,uandishi wako tu unaonyesha uwezo wako wa kufikiri pamoja na umri wako alafu unajiita mtaalamu AIBU kubwa kwa wataalam.
 
Najivunia kua mm ndugu , Bado mdogo nimesha zaid ya article 300 . aliekuambia umri wa mtu unapima uwezo wa mtu n nani? Am proud of who I am ,

na nachojivunia zaid n kwamba nafanya kitu ambacho sikuwahi kukisomea . Sikuhitaji kumezeshwa maneno ya watu au taaluma ya watu ili niandike yote niliyokwisha yaandika .

Kwann nisivunia na kujiuta mtaalamu? Au mpaka mzungu akisema ama kuandika ndio unakubali? Hata hvyo sishangai n Tanzania yetu ilivyo .

* Hutaki andamana* ndio kauli uliyoitoa , Ukajiona mkuuubwa , unajua sana . hongera
 
mbona umecopy na kupest mkuu ??

cc Dan Pol

Fafanua Mkuu, kaiba kauli ya mtu mwingine? Kama ni kweli na kwa kuwa haku-acknowledge source bila shaka atakuwa amevunja kanuni za JF. Mods - kazi ni kwenu.

Article nimeandika mwenyewe , kama umeiona popote naomba taarifa huyo mtu kaiba

Tafuten jina langu fb Dan Pol mtakuta nimepost pale , angalia mda na tarehe niliyoipost na mda na tarehe ya huko mliko ikuta , pia naomba nipajue huko mliko ikuta
 
Last edited by a moderator:
Kuna baadhi ya mamabo umezungumza sawa ila tatazo nliloliona hoja yako inakosa uhalali wa kisoka kwa sababu tu unazungumza kishabiki na kinazi zaidi,nina hakika wewe ni mshabiki wa timu mojawapo ya uingereza...sasa kwa yaya yeye uwezo wake unaishia EPL..
 
Najivunia kua mm ndugu , Bado mdogo nimesha zaid ya article 300 . aliekuambia umri wa mtu unapima uwezo wa mtu n nani? Am proud of who I am ,

na nachojivunia zaid n kwamba nafanya kitu ambacho sikuwahi kukisomea . Sikuhitaji kumezeshwa maneno ya watu au taaluma ya watu ili niandike yote niliyokwisha yaandika .

Kwann nisivunia na kujiuta mtaalamu? Au mpaka mzungu akisema ama kuandika ndio unakubali? Hata hvyo sishangai n Tanzania yetu ilivyo .

* Hutaki andamana* ndio kauli uliyoitoa , Ukajiona mkuuubwa , unajua sana . hongera

Haaaaahaaa kiddo hapa sio FB kwamba unaleta article za kinazi ukadhani watu watakenua meno kwanza uandishi wako mbovu alafu unaleta utoto wa kua umeandika articles 300 ukidhani ita-justify utaalam wako.
Hapa nna ku-quote kwa mara ya mwisho maana ni kupoteza muda.
 
Back
Top Bottom