Kwa haya mambo 2 natangaza rasmi kuunga mkono January Makamba kukamata kijiti kuongoza Tanzania kuanzia 2030

Kwa haya mambo 2 natangaza rasmi kuunga mkono January Makamba kukamata kijiti kuongoza Tanzania kuanzia 2030

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Dunia inakabiliwa na changamoto kuu mbili sasa;

1. Uharibifu wa Mazingira
2. Kujenga uchumi imara katika mazingira magumu

Kwa kuangalia kuanzia mwaka 2030 sioni mwanasiasa mwenye upeo wa kuiongoza Tanzania kupita kwenye changamoto hizi na kushinda zaidi ya January Makamba.

Kwanini January Makamba
1. Akiwa Waziri wa Mazingira alifanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kusimamia sera ya kuondosha mifuko ya plastiki ambayo ilikuwa kikwazo kikubwa katika usafi wa Mazingira hapa Tanzania. Akiwa chini ya Rais wa sasa ambaye alikuwa Makamu wa Rais na Msimamizi wa Masuala ya Mazingira January Makamba alifanikiwa kwa asilimia zaidi ya 90 kufanikisha hili. Tanzania ilikuwa safi na ilifanikiwa kuondokana na mifuko ya plastiki chini yake

2. Sasa akiwa Waziri wa Nishati ameanzisha movement ya kuhamasisha nishati mbadala ya Gesi ili kuliokoa Taifa hili ambalo sasa linatishwa kiuchumi kutokana na ukataji mkubwa na uharibifu mkubwa wa misitu unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa katika kupikia.

Kwa mambo haya napenda kusema mimi Lord Denning namuunga mkono January Makamba for presidency coming 2030.

Lord Denning
Mwanza
 
Umesahau jambo moja kubwa kuliko alilofanikiwa ndani ya muda mfupi zaidi: kukatika katika kwa umeme nchi nzima, bei ya nishati kutokushikika.

Lingine ni kale ka uchawi kao mvua kugoma nchi nzima tangu achukue wizara. Mwaka huu ndio itakuwa balaa nasikia alikuwa kwenye msitu mnene akifanya yake.
 
ALICHOFANIKIWA NI KUMTOA MSHAMBA MJINI TU!!! BASI![emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji125]
Hapana! Kwa changamoto za kidunia sasa tunahitaji watu wenye upeo wake kuongoza kuanzia 2030
 
Unataka tutumie nishati mbadala wakati bei ya umeme na gas ni km anasa .....wapunguze bei ya umeme na gas waone km watu watahangaika na mikaaa ....lakini bila kufanya hivo wanapiga kelele tu[emoji41]
Kwa hii movement nahisi bei ya gesi itashuka sana hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom