Kwa haya yaliyotokea Florentino Perez ndiyo mwisho wake?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Jamaa aliejulikana kama "The greatest seducer of Men". Rais wa Real Madrid sasa naona ana bonge la kashfa. Audio leaks za mazungumzo yake na mtu aliemrekodi zinaachiwa.

Hadi sasa kawatukana wachezaji walioiletea timu yake sifa zote. Raul na Cassilas kawaita 'fraud'.
Cristiano Ronaldo .. idiot
Morinho .. abnormal..

Na bado audio inaendelea.

Achilia ugomvi wake na Uefa kuhusu . Super ligue na ugomvi wake na Zidane hadi Zidane akatimua.

Bado shida ya hela walizo nazo Hadi wanashindwa kusajili.

Inawezekana huu ndo mwisho wa Florentino Perez?
 
Jamaa mpaka anakufa huyo hawezi wasahau waingereza kamwe na waziri wao mkuu walichomfanya kwenye ile super league 😀😀😀😀.

Pale ndio niligundua rasmi epl ina nguvu mno kwenye soka la ulaya hata uefa wenyewe wanasanda jamaa wakiamua jambo lao

Walianzisha goal line technology uefa wakiongezea na VAR.
 
Kila kitu kina mwanzo na mwisho wake, Amefanya mambo mengi Makubwa katika soka la dunia hii hata yeye anafikiri tayari amefikia mwisho na Moja kati ya project yake ya mwisho kubwa ni kuufanya uwanja Wa nyumbani Wa Santiago Bernabeu kuwa moja ya viwanja Vikubwa zaidi duniani na hilo linakamillika Muda si mrefu.

Florentine Perez kipindi hiki Amekuwa akifanya vituko mbalimbali na kujiuliza kwann Alikuwa hafanyi kipindi cha nyumba ikiwemo ya Kuanzisha European super league lengo Lilikuwa ni kutaka battle la UEFA, na hata hizi video zinazoleak kipindi hiki nadhani yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya legacy yake katika world football, The greatest seducer in world football
 
Jamaa mpaka anakufa huyo hawezi wasahau waingereza kamwe na waziri wao mkuu walichomfanya kwenye ile super league 😀😀😀😀...
Jamaa hakuwa na sure target ya hiyo league, alikuwa anajua eefect zake baada ya kuandaa mpango huo, kwamba timu zitatangaza kujiunga na hiyo superleague na Perez atatoa nyaraka za kusaini katika umoja huo wa European superleague ili baadae timu Zikianza kujitoa, tayar yeye ana nyaraka za kisheria ili awapige faini zile timu zote zinazojitoa

Bahati mbaya kwake timu mbalimbali kubwa zilimuunga mkono ila ilibaki process ya mwisho ya kusaini nyaraka za superleague hili ndo lilishindikana baada ya effect zake kuanza kutokea mapema sana bila mategemeo ya Perez

Na lengo la yeye kufanya vile ilikuwa ni mpango wa Kuongeza mapato kwenye klabu yake ambayo Kwasasa pesa mingi imeingia kwenye Kurekebisha uwanja wa Santiago bernabeu hivyo kupelekea timu hiyo kuyumba kidogo na Kushindwa Kuonesha zake katika usajili wa wachezaji kama ilivyo kawaida yake ya kuvunja record yaan The Galacticos
 
Aliijali madrid tu
 
Hamna marefu yasiyo na ncha
 

The Onda Cero Transistor reveals that Abellán had a meeting in 2011 with the vice president of the RM, Eduardo Fernández de Blas, at the Combarro restaurant, in which he blackmailed him by asking for 10 million euros to make illegal and manipulated recorded audios disappear.

=========
Let's see if I find out, the Vice-president of the @realmadrid He accuses me of extortion in 2011 ... 10 years ago ... and nobody reported me then? and the president, meanwhile, uses the club's website and the members for his personal benefit .. You are almost like the Calderón Board ... or worse ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…