Kwa haya yaliyotokea Florentino Perez ndiyo mwisho wake?

Abellan alichokuwa anataka ni fedha, inasemekana alijaribu kuuza hizo recording mara nyingi bila mafanikio kwa muda kidogo mpaka hapa juzi El Confidential walivyo kubali kuchapisha hayo maongezi, so si ajabu angepata alichokuwa anataka tusingesikia hizi taarifa.,
Na kilichofanya Perez kukataa kumpatia fedha ni kwa kuwa aliwahi kuchapisha hizo taarifa ila hazikuwa na mapokeo mazuri, halafu jambo jingine ni kuwa Perez kipindi kile ndio alikuwa amejiuzulu kama Rais wa Club ya Real madrid so alikuwa na hasira na hao waliomkwamisha ndio maana ni kama alikuja kumtoa Casillas kupitia mlango wa nyuma.
Bado sioni mwisho wa Perez kwasababu sioni akijiuzulu hiyo nafasi kwa kuwa club na board member wanamuunga mkono., kama akijiuzulu ndio itakuwa mwisho wa enzi yake kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…