Kwa Hayati Magufuli hela anazotumia Tundu Lissu kuzurura zingetumika kujenga zahanati nchi nzima

Ilishindikana au ilikuwa ipo kwenye process. Walianza na bunge, ikaja ofisi ya Waziri Mkuu etc, muwe wakweli.
Na ukweli wa chadema kushindwa kujenga ofisi ya chama kwa miaka 30 ni ipi?
 
Hii ya kuhamishia wanyama Burigi, Chato?
Hii ya kujenga majengo makubwa Chato?
Hii ya kujenga airport Chato bila bunge kupitisha?
Hata barabara za juu ulikuwa unaziona ulaya sasa hivi unajifanya hujui bingwa wa miundombinu alifanya makubwa ndani ya muda mfupi hadi watangulizi wake wakaona aibu.
 
Kwani Chato sio Tanzania ni Burundi?
Unajua maana ya STRATEGIC MRADI..!! Usije ukadhani unajenga tu popote ilimradi ni Tanzania..!!! Unadhani kwanini Kiwanda cha Cement kijengwe karibu na raw materials zinakopatikana, eg Dangote, Wazo hill..??? Kwanini Mwendokasi haikujengwa huko Kilando Sumbawanga? Kwanini Kiwanda cha sukari hakikujengwa Mbambay huko Ruvuma?
Huweki kitu kisa tu ni Tanzania..!! Basi meli za uvuvi zingekuwa zinapaki Dodoma..!!
 
Hata barabara za juu ulikuwa unaziona ulaya sasa hivi unajifanya hujui bingwa wa miundombinu alifanya makubwa ndani ya muda mfupi hadi watangulizi wake wakaona aibu.
Kujenga flyover ndio mambo makubwa?. Watu wamejenga uwanja wa Taifa na hawaringi. Watu wamejenga bunge letu na hawaringi. Watu wamejenga UDOM, UDSM na wapo kimya. Ila nyie kujenga daraja moja tu kelele nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…