eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Napenda nichukue fursa hii kuwapa pongezi na kuwashukuru kwa jinsi tulivyokuwa pamoja kwa kipindi chote cha mwaka 2017. mwaka ulikuwa mzuri licha ya changamoto kadhaa. wana JF hususan jukwaa la Afrika Mashariki mumekuwa mstari wa mbele kuleta na kuchambua mada motomoto, huku mkionesha weledi kwenye kutumia takwimu toka kwenye vyanzo rasmi. najisikia furaha na fahari kuwa katika jukwaa hili dogo la Afrika Mashariki. limesheheni vipawa na vipaji ambavyo kila unapoingia kwenye mijadala lazima utoke na ujuzi wa ziada.
nawatakia kila la kheri kwa mwaka mpya (2018) ujao kwa wajumbe wote wa jukwaa hili la Afrika Mashariki.
ndimi mwanajukwaa mwenzenu.
eliakeem.
aksante.
nawatakia kila la kheri kwa mwaka mpya (2018) ujao kwa wajumbe wote wa jukwaa hili la Afrika Mashariki.
ndimi mwanajukwaa mwenzenu.
eliakeem.
aksante.