Serikali iliwapa Wananchi wa vijiji sita vinavyozunguka shamba la Mifugo la Utegi baada ya Serikali kuwaeleza kuwa hawatalipwa chochote badala yake watapewa shamba kufidia malipo ambayo wangelipwa baada ya kuhamishwa na Serikali. Hata hivyo Serikali iliwaomba walipe kiasi kidogo (token figure) ya Tshs.90,000,000(millioni tisini) ili waiiliki shamba hilo kwa asilimia mia.
Kuna kijana wetu alijitolea kuwalipia wananchi ili baadaye waje wamrudishie fedha zake lakini kumbe ilikuwa janja yake ya kumiliki moja kwa moja shamba hilo. Baada ya kilio cha wananchi cha muda mrefu Serikali iliingilia mgogoro huo na kumnyang'anya Ndugu aliyewalipia wananchi fedha zake. Baada ya Serikali kumaliza mgogoro huo badala ya kuwarudishia wananchi shamba lao sasa tukaona Maaskari wakiletwa pale pia na ng'ombe walionunulia wakiletwa pale bila hata kuwaelezea wananchi kinachoendelea.
Kabla hapo wananchi walikuwa wakipata fursa ya kuchunga mifugo yao kwenye shamba hilo, kukata majani kwa matumizi mbalimbali na akina Mama kujipatia kuni kwa ajili ya kupikia. Tangu Maaskari hao wafike hapo wamepiga marufuku wananchi kukanyaga, kutembelea, kuchunga katika shamba lao wanalolimiliki kisheria na kupata vitisho vya kila aina.
Tunajiuliza Je, Maaskari hao wako hapo kwa shughuli gani, Je shamba hilo ameuziwa nani? Je, umiliki wa wananchi ambao ni wa kisheria umefutwa?. Sisi wananchi bado tunatambua shamba ni letu na tunaiomba Serikali iturudishie shamba letu kwa maendeleo ya Vijiji sita vinavyozunguka Shamba la Mifugo la Utegi vinginevyo itabidi twende Mahakamani kudai haki yetu.