Kwa hii aibu niliyopata, naenda kujifunza Kiingereza

Dr Msweden

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2020
Posts
2,629
Reaction score
9,530
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no,mmmh sir,yes boss, yaah yaah,ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
 
Kwani kingereza ndo nn yan watu kibao wanaishi Europe na hawajui hata hicho kingereza sembuse sisi wa Tz? Mtu yuko Amsterdam Yan akitaka kuingia London ni ferry tu hapo masaa kadhaa kaingia Uk ila hajui kingereza wala siyo udhaifu mbona ye mzungu hajiskii udhaifu kutokujua kiswahili
 
Wala sio aibu na usijione wewe ndio mwenye jukumu la kujua kiingereza, hata huyo mzungu naye inabidi ajifunze kiswahili mbona wenzake nyomi huku street wanaongea hadi kinyakyusa??
Umemaliza
 

Kwahiyo mzungu alipata huduma au alikosa[emoji28]
 
Kwahiyo hata cha kuombea maji hujui???

Okay, ngoja nikupe njia rahisi ya kujifunza kingereza, tafuta story book zile za chekechea na pembeni uwe na dictionary jitahidi kusoma vingi uwezavyo alafu jitahidi uwe unaongea na anayejua Kama yupo karibu (sio mpaka uende darasani)
 
Mkuu wewe siyo kiazi tu bali kiazi mbatata (kidding).

By the way pole sana kadhia hiyo.
 
Umeshakosa point tatu muhimu kwa mama mkwe.....[emoji3][emoji3]
 
Sasa mama mkwe anakucheka wakati haelewi kitu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Umenikumbusha ile misamiati ya kingereza Cha hayati πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…