Kwa hii aibu niliyopata, naenda kujifunza Kiingereza

Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
Wewe na mama mkwe wako mtauzaje famasi bila vyeti hamukumaliza form four na kusoma chuo cha afya.....mgejua angalau kiingereza cha kuanzia.
 
Wala sio aibu na usijione wewe ndio mwenye jukumu la kujua kiingereza, hata huyo mzungu naye inabidi ajifunze kiswahili mbona wenzake nyomi huku street wanaongea hadi kinyakyusa??
Usipotoshe mwezio, bila kujua kiingereza katika hi nchi masikini kama Tz, utakua unajinyima fursa zingine, wazungu hawaitaji kiswahili kwa vyovyote lbda kwa utalii tu.
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
basi wewe ni kilaza mkuu, unashindwaje kuzungumza kiingereza na huku unasema unakijua balaa
 
Nimefurahi ulivyoongea ukweli, yes, no, yah boos..haha
 
Mi nazani ni suala tu la umasikini wetu ndo linasababisha tuangaike kujua lugha nying ila mbona wezetu Wachina Wahindi wamexico na wa hispania wengi hawajui kiingereza ila biashara wanafanya na maisha yanaenda.

Mzungu kaja Tz ajifunze kiswahili au atafte mkaliman sio ww Mtz ujifunze kingereza kuongea na mzungu
Ni maoni yangu tu
 
Mwalimu wa kiingereza kwa madaraja yote yaani

1. Beginner’s Level
2. Intermediate Level
3. Advanced Level

Wasiliana 0743123946 WhatsApp
0684436954 Call/SMS
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
Nyie kimombo hakipandi kwa kimbelembele chenu mnaweka duka la madawa kwenye njia wanazopita wadhungu! Ondoeni huko uswazi kwenu zipo flemu nyingi tu za kupanga.
 
Ndiyo shida ya kujimwambafy, hadi mama mkwe akadhani unajua ung'eng'e kumbe wapi. Ukabaki yes yes mzungu kala mafenesi.Mkuu acha hizo!
 
Muonekano wangu umekaa kishua mtu akiniona tu anajua nina hela halafu naongea Kiingereza balaa.

Jana kuna mzungu kaja pharmacy ya mama mkwe kununua dawa sasa mama mkwe Kingereza akipandi akamtuma mtoto aje kuniita, nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha.

Kilichofata najua Mimi na Mungu wangu yes no, yes boss, yaah yaah ndio zilitamalaki hadi mama mkwe akaanza kucheka.

Hii aibu nzito sana. Kweli Mimi ni kiazi
Ze,ze waters zilikuwa nyingiii,jifunze mkuu,hiyo lugha ya malkia muhimu kujiua...
 
"nimefika dukani ile kumuona mzungu tu kimoyo moyo nikajisemea nimekwisha. "

hii inferiority ni mbaya sana
yani unaona aibu kutokujua lugha ambayo sio asili yako

sidhani kama mzungu huko ulaya angeshtuka kukuona tu pharmacy, kwamba angeshindwa kukuongelesha kiswahili
Hapa bila shaka alimuogopa Mama mkwe zaidi kuliko huyo mzungu,angekua mzungu peke yake isingekua shida.
 
Pole sana msweden Ila wewe siyo kiazi aicee basi tu hizi lugha zilizokuja na majahazi mda mwingine inabid uwe unajitahidi kujua hata cha kunywea maji ili kukwepa hizi aibu ndogo ndogo.
 
Back
Top Bottom