matokeo ya ELimu Mbali Mbali toka Pakistani! mtu pekee mwenye maono wanataka kumnyonga hadi kufa! atuache na hawa mbu mbu mbu.Wakuu habari zenu!
Nadhani hakuna mtu ambaye hajapita Morogoro road hasa eneo la Kimara mwisho! Kinachoendelea hapa ni masikitiko, maana hili ndilo lango la jiji, ila foleni ya eneo hili inatia kinyaa!
Ukitoka mjini si ajabu kumaliza saa zima au nusu saa kutoka kimara korogwe mpaka kuvuka pale Kimara mwisho! Pale kuna upanuzi unafanyika ila la maana hakuna! Maana kama unatoka mjini kulikuwa na service road ya kuchepukia Bunyokwa ila nayo wameiua wameweka vitu vya ajabu ajabu pale!
Licha ya ujenzi usioisha ila barabara ya kutokea mjini ni kama imeisha na hakuna solution yeyote, hata ule upande wa pili wa kwenda mjini , hata pakiisha hakuna unafuu wowote utapatikana!
Hapa ndipo huwa nakaa nawaza, hivi watanzania hatuna akili kabisa!? Barabara kuu ya Kuingia DSM tumeshindwa kujenga hata express way? Mbona Nairobi wameweza? Je wakenya wana akili nyingi kutuzidi? Yaani ukiangalia ile Express way yao toka Jomo Kenyata Airport mpaka James Gichuru Road mpaka unapata hasira, na cha zaidi wale jamaa ile express way bado inaendeleq!
Sisi Watanzania kwani tuna shida gani? Kuna hasara gani tukijenga hiyo miradi ya maana husasani barabara?
NB: Nyie watu ambao huea mnavompare DSM na Nairobi muache mara moja, maana Dsm ni uchafu tu! Lile jengo la mawasiliano tower na TPA mnayoyapiga picha kila uchao, kule Nairobi yapo kwa mamia!
Wanachojua kila siku ni Kubishana na Viongozi wa DINI!