Kwa hii idadi ya noti za tsh 10,000 ziazotoka kila dakika kwenye ATM kuna ulinganifu kweli na noti nyingine mtaani?

Kwa hii idadi ya noti za tsh 10,000 ziazotoka kila dakika kwenye ATM kuna ulinganifu kweli na noti nyingine mtaani?

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Salam humu.

Hizi noti zinasumbua Sana mtaani kwenye mzunguko wa pesa hasa kwenye biashara.Nahisi zimekuwa nyingi idadi tofauti na noti nyingine.

Sasa hivi ukienda kwenye ATM hawatoi kabisa noti za elfu tano.Yaani wanakwambia kabisa tunatoa mafungu ya kumi kumi tu.Na hata ukienda ndani ya benki idadi kubwa inayopatinaka no misimbazi tu.

Hebu wataalam wa fedha jaribuni kuangalia hii hali ikoje.Haya manoti inawezekana yako mengi mtaani kuliko noti zingine na yanaeumbua.

Benki nazo zijaribu kuangalia hii hali inaendaje hivi hakuna utaalamu wa kuchagua kwenye ATM kutoa noti nyingine..yaani magwiji wanafeli wapi kwenye hizi atm tunapata noti ya aina moja tu.Wazungu utaalam wao umeishia kutoa hela tu wanafeli wapi.!!??
 
Hv pale kwenye ATM inawezekana kutoa 5000, mfano naweza kutoa labla 85000.?
 
Salam humu.

Hizi noti zinasumbua Sana mtaani kwenye mzunguko wa pesa hasa kwenye biashara.Nahisi zimekuwa nyingi idadi tofauti na noti nyingine...
Mkuu umefikira mbali sana, umewaza kitu ambacho hata sikukifikiria kabisa. Nakubaliana na wewe kwamba inakuwaje ATM zisiwekwe noti za dinominasheni mbali mbali ili mtoaji achague kiasi kulingana na dinominasheni anayotaka kulingana na matumizi yake.

Hizi kumi kumi zitakuwa nyingi mtaani zinaweza leta mtafaruku kwenye kununua bidhaa ( attract higher prices).
 
Upo sahihi Mkuu niliwahi kujiuliza hili swala kipindi fulani kila ATM utakayokwenda inatoka elfu kumi tuu..
 
10,000 yenyewe ukishaichenchi shughuli imeshaisha[emoji23]
Ni huzuni na masikitiko
 
Mnatakaje sasa Watanzania

Hivi na haya matumizi ya Mobile Banking, bado mnasumbuka kwenda ATM...? Embu acheni utoto
 
00 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 15 shilingi laki na 50

nina 5000 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 2 shilingi 10000

nina 2000 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 1 shilingi 2000

nina 1000 hizi kubwa kabla ya hizi mpya 1 shilingi 1000
jumla =======163000
nipeni utaratibu ni bahasha yangu ya 2007 nimezikuta nipokilimanjaro now
 
Back
Top Bottom