Kwa hii katiba ya mwaka 1977 nashangaa watu mnaomsifu Nyerere nakumuita shujaa

Kwa hii katiba ya mwaka 1977 nashangaa watu mnaomsifu Nyerere nakumuita shujaa

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
32,386
Reaction score
83,431
Kama kweli hii katiba ya mwaka 1977 imebarikiwa wakati wa utawala wa Mwl: Nyerere ni wazi Hapa mzee wetu alikusudia kuangalia self interest. Rais kujigawia madaraka makubwa then mnabaki kumuita shujaa.

Nawasilisha hii katiba ya Mwl Nyerere hiko vibaya sana. Inapaswa kufumuliwa mara moja.
 
Nyerere ameshafariki badala ya kupoteza muda kutoa lawama ni bora ungeanza jitihada za kupigania vifungu vibovu viondoke katiba yake ilikuwa sahihi.kwa wakati ule ndio maana tulipoingia vyama vingi kulikuwa na tume ya Nyalali ambayo mbali ya kukusanya maoni ilipendekeza sheria 40 ziondolewe kitu ambacho hakikufanyika ni Nyerere huyohuyo unayemsema.aliunga mkono vyama vingi na kuishauri serikali iunge mkono mgombea binafsi
 
Umeandika ukifikiri kila mtu anayo hiyo katiba mezani kwake na anajua hicho kifungu unachoongelea.
Nonsense!
 
Kipindi hicho Nyerere alikuwa ndo kwanza anaijenga nchi na ukiangalia kwa jinsi alivyokuwa mzalendo naona ni sawa kuwa na katiba ya aina hii kipindi kile lakini kwasasa haitufai inatakiwa katiba mpya inayoendana na wakati huu.
 
Kama kweli hii katiba ya mwaka 1977 imebarikiwa wakati wa utawala wa Mwl: Nyerere ni wazi Hapa mzee wetu alikusudia kuangalia self interest. Rais kujigawia madaraka makubwa then mnabaki kumuita shujaa.

Nawasilisha hii katiba ya Mwl Nyerere hiko vibaya sana. Inapaswa kufumuliwa mara moja.
Angalau Nyerere alikuwa na busara na hekima sababu ya malezi bora thus akawa cold blood dikteta, tofauti na ma pure dikteta Kama kina moi,mobutu, bokasa, mugabe,nk.Nyerere alikuwa na utu ndani yangu sababu ya malezi bora thus alisita kuwatendea ukatili wengine.
Lakini alituachia katiba mbovu kabisa alipoicopy toka nchi za kikomunisti na kuileta itumike pasipowashirikisha wananchi kwenye utungaji.Leo ni wahanga wa katiba mbovu
 
Katiba yetu 100% inabase kwenye udikteta labda tu mtawala awe civilized na matured asiitumie vibaya kuumizia watu
 
Nyerere alikuwa dictator. Ukiangalia wale waliotofautiana nae jinsi alivyowafanyia acha tu.Aliruhusu vyama vingi baada ya kuona hawezi kupambana na nature,yaani alikuwa ameshakuwa mgonjwa hivyo akaona na hizi fuku fuku za mageuzi angekufa kabla ya siku zake.
 
Kipindi hicho Nyerere alikuwa ndo kwanza anaijenga nchi na ukiangalia kwa jinsi alivyokuwa mzalendo naona ni sawa kuwa na katiba ya aina hii kipindi kile lakini kwasasa haitufai inatakiwa katiba mpya inayoendana na wakati huu.
Katiba mfu katiba chakavu sii sahihi kwa kizazi cha sasa
 
Nyerere alikuwa dictator. Ukiangalia wale waliotofautiana nae jinsi alivyowafanyia acha tu.Aliruhusu vyama vingi baada ya kuona hawezi kupambana na nature,yaani alikuwa ameshakuwa mgonjwa hivyo akaona na hizi fuku fuku za mageuzi angekufa kabla ya siku zake.
Copy na paste,alivifuta vyama vingi baada ya Uhuru kuogopa challenge,waliomchallange aliwatia jela na kizuizini, wengine aliwateua ubalozi nje ili wasimsumbue,alimiliki akili na mawazo ya watu kwa kumiliki printing room na kuzuia uwepo wa tv na radio binafsi ili watz wasijue kuhusu external world.
 
Kuna ulazima wa kuendelea kupaza sauti zetu ikiwemo humu mitandaoni kuidai Katiba Mpya. Hii ya mwaka 1977 ni ya Ccm na siyo ya Watanzania tulio wengi.
 
Nyie mnao mkosoa Nyerere sasa hivi, wakati alipofanya hayo makosa mababu zenu walikuwa wapi?
 
Hata kama kuna mambo kakosea, mimi nakaa kimya tu maana nchi hii kiukweli sijaifanyia makubwa yoyote kwanza muda ninaoutumia kubet au kwenda uwanjani taifa kumuangalia yipe na molinga, nyerere angeutumia kuwaza mambo ya msingi kuhusu maendeleo ya Tanzania.. siwezi kumsema nyerere kwanza kwa lipi hasa nililoifanyia nchi hii?
 
Back
Top Bottom