Kwa hii Shida ya Mitandao ya simu iliyotokea leo, turuhusu Starlink iingie Tanzania

Mpaka leo sielewi kwanini statlink waliwekewa figisu, inastaajabisha sana nchi hii, kuna wataalamu kibao wa mambo haya ila wamekaa kimya bila kulisemea hili, mpaka unajiuliza tupo kwenye ulimwengu upi na karne ipi.

Vijana wengi wanazalishwa kutoka vyuoni, fursa ya cheap Internet ingewezesha vijana kujiajiri sana, inaumiza sana nchi haina huruma kwa vijana, ajira matatizo, hata hili la fursa kwa vijana kujiajiri bado serikali inaweka uzio. So pain.

Nchi imefuga watu wachache na wengi wakiumia, imefikia hatua mbunge anahoji bumu kwa wanafunzi akiwatuhumu kwa ulevi na uhuni, je pale bungeni hakuna walezi na wahuni na wanapokea posho kibao? Yani mbunge anawaza minority anasahau majority? Kweli huyu ana sifa za kuwasemea wananchi? Hebu angalia nchi zenye cheap Internet na utaona kila siku wanaibuka watu na mawazo mapya ya kuboresha maisha yao na ulimwengu kwa ujumla. So shame kwa viongozi wa namna hii.
 
Nchi ni siku ya tatu leo watu wapo na mkwamo wa internet waziri yupo tu karelax

Anafanya nini ofisini?Kwani asijiuzulu haraka huyu mtu?

Nape anafaa kuwajibishwa!! Kwanza yeye kwa maksudi ndo aliwapiga vita StarLink kwasababu tu na yeye ni mnufaika wa makampuni ya simu

Huyu jamaa amekua anapokea mishahara mitano hadi sasa

Mshahara wa kwanza ni kutokana na cheo chake serikali

Pia amekua akilipwa na Tigo kila mwezi

Analipwa na Vodacom kila mwezi

Analipwa na Halotel kila mwezi

Analipwa na Airtel kila mwezi

Analipwa ma Tigo kila mwezi

Kwa maksudi na turufu yake aliondoa watu watatu pale tcra kwa kukataa kufata matakwa yake na kuhakikisha wanaingia watu wa team yake ili ulaji wake uendelee kuwepo

Huyu waziri hatufai!! Nape ajiuzulu
Wacha kukurupuka wewe, Internet siyo huduma ya kisisasa, au kama umeme wa Tanesco, wala sio huduma ya Taifa fulani. Internet ni huduma ya kidunia, inayotolewa na ma ISP wakubwa duniani kuiunganisha dunia yote kuwa moja kimawasiliano ya kimtandao kupitia miundomibinu yao inayounganisha mabara yote, bara moja na lingine kupitia baharini hivyo kunapotokea na hitlafu yoyote katika miundominu hiyo basi watumiaji hawawezi pata huduma za kimtandao duniani(Internet). Wewe unataka huyo Nape afanye nini, Unafikiri SEACOM na EASSY ni watanzania?
 
Mnalilia starlink lakini hamjui Ina gharama kuliko hawa watoa huduma wa hapa;

1. Ni ghali. Kule Kenya kununua vifaa ni Ksh 88k~Tsh 1.76m, na unalipia Ksh 6.5k~Tsh 130k kwa mwezi.
Japo kina muda walipunguza bei kwa 55% ila bado ghali, ndo maana mpaka sasa inatumika na wakenya karibia 3000 tu

2. Inasumbua kwenye mvua kama visimbuzi

3. Kuna muda kunakuwa na watumiaji wengi kwa wakati mmoja, ile high traffic inafanya mtandao kupungua kasi

4. Inabidi dish liwekwe sehemu ya wazi (sio karibu sana na miti au milima) lasivyo inasumbua
 
Nape anatakiwa aingize ushindani kwenye soko la Internet ,pamoja na kutumia njia ya bahari,sasa ni muda wa kuleta pia njia ya angaa!!
 
Habari ipo duniani underwater sea cable 2 zimekatika 28 km ufukwe wa S.A, alternative ni ku swap kuna cable za ulaya ndio makampuni yanaamia huko shughuli pevu ni kuamisha data zao which is a lot.

Kuna podcast kwenye article inaelezea how the global underwater internet works na changamoto za kutengeneza ikikatika.

Sasa hapo Nape au makampuni ya simu yafanye nini zaidi ya kusubiri.

View: https://m.youtube.com/watch?v=d0gs497KApU&pp=ygUddW5kZXJ3YXRlciBjYWJsZSBpbnN0YWxsYXRpb24%3D

99% ya internet duniani zinasabazwa na submarine cable it’s cheaper technology na kazi yenyewe sio rahisi, meli zinazofanya hiyo kazi azizidi kumi na zinakuwa booked months in advance na shughuli yenyewe sio ya kitoto (uwezi kuipangia bahari lini itulie, ikija rough sea shughuli inasimama).

View: https://m.youtube.com/watch?v=l1knCR6xAzo&t=12s

Halikadhalika nyaya zikikatika shughuli ya repair underwater divers wa kufanya repair work duniani wanahesabika, high depth ni ROV ndio inaweza fanya hiyo shughuli ndio maana makampuni yana amishia shughuli zao kwenye cable za Europę kuliko kusubiri S.A watengeneze.

Hapo kumlaumu mtu ni kumuonea, ni swala la ‘ajali kazini’ hakuna wanachoweza fanya Tanzania ni vitu vilivyo juu ya uwezo wao.
 
Wacha kukurupuka wewe, Internet siyo huduma ya kisisasa, au kama umeme wa Tanesco, wala sio huduma ya Taifa fulani. Internet ni huduma ya kidunia, inayotolewa na ma ISP wakubwa duniani kuiunganisha dunia yote kuwa moja kimawasiliano ya kimtandao kupitia miundomibinu yao inayounganisha mabara yote, bara moja na lingine kupitia baharini hivyo kunapotokea na hitlafu yoyote katika miundominu hiyo basi watumiaji hawawezi pata huduma za kimtandao duniani(Internet). Wewe unataka huyo Nape afanye nini, Unafikiri SEACOM na EASSY ni watanzania?
Mkuu acha uongo na rudi darasani ujifunze tena haya mambo.
 
Mnalilia starlink lakini hamjui Ina gharama kuliko hawa watoa huduma wa hapa;

1. Ni ghali. Kule Kenya kununua vifaa ni Ksh 88k~Tsh 1.76m, na unalipia Ksh 6.5k~Tsh 130k kwa mwezi.
Japo kina muda walipunguza bei kwa 55% ila bado ghali, ndo maana mpaka sasa inatumika na wakenya karibia 3000 tu

2. Inasumbua kwenye mvua kama visimbuzi

3. Kuna muda kunakuwa na watumiaji wengi kwa wakati mmoja, ile high traffic inafanya mtandao kupungua kasi

4. Inabidi dish liwekwe sehemu ya wazi (sio karibu sana na miti au milima) lasivyo inasumbua
Ila wabongo kwa ujuaji na uongo, tunatisha sana. Dah mkuu nmecheka sana hizi facts zako na umezipa na namba kabisa dah 😂 kweli mshamba hachekwi
 
Mpaka leo sielewi kwanini statlink waliwekewa figisu, inastaajabisha sana nchi hii, kuna wataalamu kibao wa mambo haya ila wamekaa kimya bila kulisemea hili, mpaka unajiuliza tupo kwenye ulimwengu upi na karne ipi.

Vijana wengi wanazalishwa kutoka vyuoni, fursa ya cheap Internet ingewezesha vijana kujiajiri sana, inaumiza sana nchi haina huruma kwa vijana, ajira matatizo, hata hili la fursa kwa vijana kujiajiri bado serikali inaweka uzio. So pain.

Nchi imefuga watu wachache na wengi wakiumia, imefikia hatua mbunge anahoji bumu kwa wanafunzi akiwatuhumu kwa ulevi na uhuni, je pale bungeni hakuna walezi na wahuni na wanapokea posho kibao? Yani mbunge anawaza minority anasahau majority? Kweli huyu ana sifa za kuwasemea wananchi? Hebu angalia nchi zenye cheap Internet na utaona kila siku wanaibuka watu na mawazo mapya ya kuboresha maisha yao na ulimwengu kwa ujumla. So shame kwa viongozi wa namna hii.
Akina nape na akili za kiccm watakuambia internet ikiwa cheap vijana watatumia kuangalia porn hivyo basi ibakie ghali

Hawakosi sababu Hawa wabnafsi
 
Nape anatakiwa aingize ushindani kwenye soko la Internet ,pamoja na kutumia njia ya bahari,sasa ni muda wa kuleta pia njia ya angaa!!
Kwa kipindi hiki teknolojia ya Faiba hutumika kwaajili ya mawasiliano masafa marefu, ndio teknolojia iliyo bora zaidi. Faiba haiwezi pitishwa angani bara hadi bara, hupitishwa baharini.
 
Tatizo la huduma ya mtandao internet lililotokea juzi lilikuwa na njia mbadala kama Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ingefikiria njia mbadala yani Backup ya Satelite badala ya kutegemea mkongo chini ya Bahari.

Kuwepo na backup ya Satelite link
 
Back
Top Bottom