Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema watumishi wa umma wasipoweza kuondoa viongozi dhalimu bora wafe tu.
Nakubaliana na Mwalimu Nyerere ila najiuliza kama watumishi wa umma ni waoga na wameshindwa kuondoa viongozi dhalimu na kumwachia Rais kazi hiyo peke yake! Kweli tupo tayari kuwanenea kifo?
Tukumbuke watumishi wa umma ni wadogo zetu, wakubwa zetu, wazazi wetu na ndugu zetu. Tunakubali wameongeza unafiki na wanastahili kufa ila kama Taifa tupo tayari kuhimili majonzi yatakayotokea?
Wakifa sisi ambao siyo watumishi wa umma tutaweza kuwaondoa viongozi dhalimu? Kama tunaamini tunaweza kwanini tusianze sasa ambapo ndugu zetu watumishi wa umma wapo hai ili wajifunze?