Kwa hiki wanachokifanya DP WORLD bandarini, maadui zetu wakubwa ni viongozi wetu walioruhusu upuuzi kudumu muda mrefu

Kwa hiki wanachokifanya DP WORLD bandarini, maadui zetu wakubwa ni viongozi wetu walioruhusu upuuzi kudumu muda mrefu

Nilishangaa sana kuona watanzania wanaagiza mizigo kupitia bandari ya Mombasa.Kiufupi Huo uwekezaji wa dp world ni wa kinyonyaji.
Miaka yote kabla ya dp world kuna wabongo wanaagiza mizigo through bandari ya mombasa
 
So ilitengenezwa scenario ya kuonekana hatuwezi kujiendesha ili bandari iuźwe. Maana kama shida inajulikana kwanini tusinge deal nayo wenyewe?

Na je unafikiri sasa hivi hakuna upigaji? Unafikiri waliosaini huo mkataba hawajapiga na hawaendelei kupokea fungu?

Hii nchi ni ngumu sana asee unahitaji kuwa na upeo sana kuelewa kinachoendelea

ephen_

Kwni hayo mamtatizo Pale Bandarini yameanza leo na Jana?
 
Miaka yote kabla ya dp world kuna wabongo wanaagiza mizigo through bandari ya mombasa
Hii inaashiria kuwa bandari yetu siyo rafiki Kwa wafanyabiashara.Yaani anakodi lukuki
 
Kama nimeelewa haya maelezo unamaanisha endapo kungekuwa na viongozi wafuatiliaji, wawajibikaji, wanaopenda maendeleo na kujua wanachokifanya kulikuwa hakuna haja ya kuwaleta hawa DP WORLD kwasababu "ni kama" kila kitu kilikuwepo kilichofanyika ni kuwakabidhi tu wafanye kazi

Kama hivyo ndivyo, mimi nakubaliana na wewe kwasababu ni kweli tuko hapa si kwakukosa rasilimali vitu bali kwa kukosa rasilimali watu inayowajibika

Juzi nimemsikia Tibaijuka anasema alikataa kusaini ujenzi wa karakana ya mwendokasi iliyojengwa pale jangwani lakini hatimaye ilijengwa. Sasa jiulize mamilioni mangapi yameteketea pale?

Kuna upuuzi mwingi ukiufuatilia utaona jinsi tulivyo na viongozi ambao hawako serious. Kila sehemu wao wanaingiza siasa siasa, kujuana, kutegeana na kutengenezeana ajali tu

Ni dhahiri kabisa DP WORLD watapandisha mapato ya TPA, lakini haitaondoa ukweli kwamba watatucheka kwa kujipatia utajiri kwa bei rahisi maana watakachovuna ni kikubwa kuliko kitakachobaki
Uko sahihi. Yaani kwa huu uzembe na ufisadi fisadi wanapiga hela sana na umma kupitia serikali tunapata kiachi kidogo sana na hali halisi inayowezekana. Kwa kuwapa DPW fisadi bila shaka wamehongwa dola nyingi sana na pengine kwa kificho wako ubia na DPW. Mapato ya serikali yataongezeka ila kwa kiasi chini kabisa ya lengo kama tungekua na uadilifu wa watendaji. Isitoshe kama ulivyosema tunaonekana wajinga tu na njama za wajanja kuhujumu nchi yetu zinapata nguvu.
 
Wananzengo, mu Hali gani?

Kwa masikitiko makubwa Leo nawatangaza hadharani maadui wakubwa wa taifa letu.

Laiti tungekuwa na uongozi imara tungekuwa mbali sana kwenye mafanikio ya kiuchumi.

DP WORLD wamepewa bandari bure, wamepewa na vitendea kazi bure. Leo wameongeza Terminal Trucks kumi na trailers 27. Wameleta Rubbered Tyred Gantre (RTG) nane. Na sasa hamna meli inakaa mwezi mzima dock ikisubiri foleni. Container ships zinaingia moja kwa moja kupakua mzigo.

Pia soma: DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Walichofanya DP WORLD ni kujaza vipuri kwenye warehouse, TPA wao hawakuweka kipuri hata kimoja warehouse, hadi magurudumu yakiisha kwenye Rich Stacker, wanatafuta Rich Stacker mbovu wanaivua gurudumu.

Viongozi wetu walikuwa wanayaona haya lakini wakishirikiana na CCM wakawa wanachukulia poa sana.

Mapapapa fisadi wa CCM wakanunua Quay Crane mbili kwa mabilioni ya pesa, kwa miaka nenda rudi hizo QC hazikufanya kazi, wamekuja DP WORLD wamenunua jenereta mbili, QC zinafanya kazi sasa, wamepata bure.

Folk lifts zinakuwa grounded kwa kukosa matairi; ni aibu gani hii?
Kwani ilikuwa lazima kutoa bandari kwa mkataba wa milele ili kutatua matatizo yaliyokuwapo?

This is a logical fallacy, non sequitur.
 
Imeisha hiyo!
 
Attachments

  • 20240622_095239.jpg
    20240622_095239.jpg
    54.5 KB · Views: 5
Kusema kweli ni aibu sana sana kwa Nchi kushindwa kuendesha berths 10!
Wamekuja wageni (DP) kwa vifaa almost vilevile walivyokuwa navyo TPA tayari kazi zinakwenda barabara!
Shame!
 
Tumepaa kiuchumi..??

Au tupo pale pale?

Je presence yao inajustify umiliki wao wa bandari zetu?
 
Ni mjinga tu anayeweza kuamini kuwa watu wa nje ndio watakaoutuletea maendeleo tukiwa tumekaa na kupiga strahere tu.
 
Bwana Maulid wa Kitenge angefaa kujibu swali vyema kabisa.

By the way ulimuona siku ya Yanga day na "mishangingi" yake miwili akiwatambishia?
 
Wananzengo, mu Hali gani?

Kwa masikitiko makubwa Leo nawatangaza hadharani maadui wakubwa wa taifa letu.

Laiti tungekuwa na uongozi imara tungekuwa mbali sana kwenye mafanikio ya kiuchumi.

DP WORLD wamepewa bandari bure, wamepewa na vitendea kazi bure. Leo wameongeza Terminal Trucks kumi na trailers 27. Wameleta Rubbered Tyred Gantre (RTG) nane. Na sasa hamna meli inakaa mwezi mzima dock ikisubiri foleni. Container ships zinaingia moja kwa moja kupakua mzigo.

Pia soma: DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Walichofanya DP WORLD ni kujaza vipuri kwenye warehouse, TPA wao hawakuweka kipuri hata kimoja warehouse, hadi magurudumu yakiisha kwenye Rich Stacker, wanatafuta Rich Stacker mbovu wanaivua gurudumu.

Viongozi wetu walikuwa wanayaona haya lakini wakishirikiana na CCM wakawa wanachukulia poa sana.

Mapapapa fisadi wa CCM wakanunua Quay Crane mbili kwa mabilioni ya pesa, kwa miaka nenda rudi hizo QC hazikufanya kazi, wamekuja DP WORLD wamenunua jenereta mbili, QC zinafanya kazi sasa, wamepata bure.

Folk lifts zinakuwa grounded kwa kukosa matairi; ni aibu gani hii?
Sasa cha ajabu sana katika hayo uliyo eleza ni kipi hasa?

Ukisema uozo wa CCM na serikali yake, hapo nitakubaliana nawe moja kwa moja. Lakini umeishia kupapasa papasa tu juu juu kana kwamba unasubiri pesa ya Abdul ikufikie kwanza.
 
Ndoto za Bandari achana nazo! Fikiria mengine,Bandari ilishaenda!
Pale kila mfanyakazi alishapigiwa hesabu za mkono wa kwa heri na nauli ya kusafirisha mizigo mpaka kwao.
Asiyetaka kazi anachukua chake anaondoka zake.
 
Unafikiri pale bandari kuna cha maana , urasimu pale wa kuchelewa ilikuwa ni awatu wenyewe ...Wale wafanyakzi ambao sasa wapo Dp world ndio hao hao wanapiga kazi maana huku wanaweza kutimuliwa.

Hakuna cha maana zaidi ya kubweteka kwa watanzania , kufanya kazi kwa mazoea ...Lazima wamuogope Muarabu wafanye kazi .

Kama tungekuwa na utaratibu wa kuwa na DG kutoka nje labda wachina , wazungu , wahindi , basi wabongo wangefanya kazi kwa shuruti tungefika mbali sana .​
Pendekezo lako hili ningeanzia pale juu kabisa kwa 'Chura Kiziw', awepo mChina hapo kuhakikisha huyo 'Chura Kiziwi' na wenzake wote wanafanya kazi za waTanzania kikamilifu.
 
Sasa cha ajabu sana katika hayo uliyo eleza ni kipi hasa?

Ukisema uozo wa CCM na serikali yake, hapo nitakubaliana nawe moja kwa moja. Lakini umeishia kupapasa papasa tu juu juu kana kwamba unasubiri pesa ya Abdul ikufikie kwanza.
CCM Chanzo Cha Matatizo
 
Back
Top Bottom