Kwa hili alilolifanya Diamond, litamgharimu sana katika safari yake ya kimuziki

pirabiriani

Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
79
Reaction score
16
Diamond platnumz kaonesha wazi msimamo wake katika mgonbea anayemtaka yeye. Sipingani na maamuzi yake, ila naona kama alikurupuka kufanya maamuzi hayo. Diamond angetambua kuwa washabiki wake wengi wanaompa support hawapo katika mrengo anaoushabikia yeye.

Nimepitia baadhi ya comments za followers wake na kugundua kuwa 90% wamekuwa disappointed sana na alichokionesha.

Halafu ukiangalia ni kama wametumwa hivi baada ya ile hafla yao na mheshimiwa. Maana baada ya pale wasanii kibao wamekurupuka kuonesha support kwa Magufuli.

Kinachoendelea saiv ni kwamba washabiki wameanzisha kampeni ya kutomsapport tena Diamond kwa kuacha kumpigia kura katika tunzo anazoshindania.

Namuonea huruma sana
..
 
hadi hapo alipofika natumai anaujua vizuri mziki wa bongo, akifanya tofauti hiyo itakuwa juu yake
 
Kijana anajua kutumia fursa ipasavyo,cio mpuuzi yule awe mrahisi kihivyo kujirisk ktk kazi yake kwa ajili ya wanasiasa.cku zote anasema,anafanya kazi yenye maslahi kwake.

Bila Shaka kuna maslahi aliyopata ktk hilo.
 
Hawa wasanii njaa sana hawajielewi kbs watu wanadhurumiwa kazi zao na serikali leo hii wamepewa pesa wanawasapoti wanasiasa hawa vipi hawa
 
Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Inawezekana ina maslahi kwake, lakin ni maslah ya muda mfupi na yanaweza kumuathiri baadae kimuziki..
 
Wots your point???... ina maana Diamond ashabikie chama cha siasa kisa , mashabiki wake wanakipenda, kama hiyo nd pointi basi lazima ufahamu mpaka wa ushabiki wako na mapenzi kwa mtu.... Freedom of expression kwani nyie mashabiki nani amewachagulia...hao wanaoanzisha hizo kampeni sio mashabiki wa Diamond, hakuna shabiki wa Diamond anayeweza kufanya upumbavu kama huo
 
Ni kosa kubwa sana kumfananisha Diamond na marlaw, Diamond hajaanza kuipigia ccm kampeni leo wala jana, mbona alivyoenda kumpigia lowassa kampeni arusha hamkusema!!!! kuna baadhi ya watu wana uwezo mdogo sana wa kufikiri, ukiwa shabiki wa Diamond hakukupi mamlaka ya kumchagulia mtu wa kumpigia kampeni, lazima ufahamu mipaka yako unless otherwise uwe na mtori kwenye ubongo
 
ni mwananchi kama sie na ana maisha nje ya Muziki

Sioni tatizo kwa yeye kuandika hivyo ni uamuzi wake na nimependa alivyoandika kakaribisha mtu anayepingana nae aseme ni kwanini, ni kama ka dibeiti fulani kaweka.

Kuhusu muziki wake embu wekeni hayo pembeni na maisha yake na yeye aishi kama mtanzania . akiishi maisha feki ndio mtafurahia, anaishi yeye

msisahu kumpigia kura katika makategory na tuzo kibao tujivunie na nchi yetu


.
 

My point is, asingeonesha wazi maana itamletea effect kwenye kazi zake za kimuziki.
Just imagine saiv mashabiki washaanza kampeni ya kutompigia kura kwenye tunzo anazoshiriki. Na nimepitia comments za mashabiki, 90% hawakufurahishwa na kitendo hicho. Unategemea nn? Wakati kura za washabiki ndo zinampa ushindi katika tunzo?
 
Tatizo linakuja pale unapotaka fikra zako ziwe kwa watu WOTE, mtu alitoa mtazamo wake wake tofauti unaanza kusema itamgarimu kwani lowasa ndo alileta mafanikio ya diamond mpaka hapo alipo?

Sijasema Ampende Lowasa. Nimesema kuweka wazi upande aliopo kutamgharimu katika safari yake ya kimuziki.
 

Daaah!...mbaya sana hiyo japo mie sio #Teamondi lakini impact yake ataja iyona,nianze kwa kusema sio vibaya kwa yeye kuwa na political party lakini kulikua hamna haja ya kuexpose uchama wake maana yeye kazi yake sio SIASA ni MUZIKI na ndio uliofanya hadi akafika pale alipo leo na sio siasa na ndio madhumuni ya yeye kuwa na accounts kwenye social media ili apate support za mashabiki wake...SASA AKUMBUKE HAO MASHABIKI WANA ITIKADI TOFAUTI ZA VYAMA YANI WAPO WA CHADEMA,CCM,CUF,NCCR...n.k PIA WAPO WASIO NA VYAMA AMBAO WOTE KWA PAMOJA WAMEKUTANISHWA NA MUZIKI WAKE AMBAO NDO DHUMUNI NA NDIO KAZI YAKE HIVYO KITENDO CHA YEYE KUFANYA VILE AMEENDA KINYUME KIITIKADI NA FANS WAKE AMBAO SI MAFISIEMU KAMA YEYE AMBAO KIMSINGI HAWATAMSUPPORT KATIKA MUZIKI WAKE AMBAO NDO LENGO KUU KWA MASHABIKI KWAKE,SISITI KUSEMA WASANII WANATUMIKA TENA VIBAYA SANA...NA TUNAYAONA HAYA BAADA YA HAFLA YA MLIMANI CITY YA "KIKWETE NA WASANII" MAANA KAMA KWELI YEYE ANAMKUBALI MAGUFULI KUWA NI JEMBE KAMA ALIVYOSEMA ALITAKIWA KUPOST VILE KABLA YA HAFLA YA M.CITY ANGEELEWEKA KUWA ANA MKUBALI JAMAA LAKINI SIO BAADA YA ILE HAFLA NDO ANAPOST...KITU AMBACHO KINAONEKANA WAZI NI ANATUMIKA TENA KWA MASLAH YAKE BINAFSI NA SIO TAIFA KWA UJUMLA...NASEMA HIVII "HII ITAMGHARIMU SANAAA KIMUZIKI",NA NIWE MUWAZI MIMI KAMA FAN WA ALIKIBA...IKITOKEA KAPOST ISHU LIKELY NA HIYO NAACHA MARA MOJA KUSUPPORT MUZIKI WAKE...#NOCOMMENT !
 
Nirudie kwa kusema tuu "hili ni tatizo kweli"...ila huwezi kuligundua kama mtu una akili ndogo na fupiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…