Kwa hili alilolifanya Diamond, litamgharimu sana katika safari yake ya kimuziki

Kwa hili alilolifanya Diamond, litamgharimu sana katika safari yake ya kimuziki

ni mwananchi kama sie na ana maisha nje ya Muziki

Sioni tatizo kwa yeye kuandika hivyo ni uamuzi wake na nimependa alivyoandika kakaribisha mtu anayepingana nae aseme ni kwanini, ni kama ka dibeiti fulani kaweka.

Kuhusu muziki wake embu wekeni hayo pembeni na maisha yake na yeye aishi kama mtanzania . akiishi maisha feki ndio mtafurahia, anaishi yeye

msisahu kumpigia kura katika makategory na tuzo kibao tujivunie na nchi yetu

.

Sitoacha kumpigia kura diamond wangu na sitoacha kumpa sapoti yeyote ile anayostahili kutoka kwangu kama shabiki wa damu.Natambua ni haki yake ya msingi kufanya hivyo na siwezi kumpangia cha kufanya.

Mashabiki wa diamond tupo na tutaendelea kuwepo
 
Hiii moja ya post ya kufukiruka sasa unataka afate unachota ww...
Muache nae anautashi wake

Mkuu TATIZO SIO YEYE KUWA CCM...HAPANA MAANA ANA UTASHI WAKE PIA KAMA ULIVYOSEMA ILA HAKUTAKIWA KUEXPOSE HADHARANI HISIA ZAKE ZA UCHAMA ANGETULIA ASUBIRI OCTOBER-25TH akampe kura yake magufuli na sio kuwahadaa wengine kwa kuwashawishi kufuata lake yeye akijua wazi ana mashabiki wengi wanaomkubali nyuma yake na pia nchi ikichukuliwa na UKAWA anajiweka katika mazingira gani???
 
tatizo linakuja pale unapotaka fikra zako ziwe kwa watu wote, mtu alitoa mtazamo wake wake tofauti unaanza kusema itamgarimu kwani lowasa ndo alileta mafanikio ya diamond mpaka hapo alipo?

gamba at work!!!
 
Mkuu TATIZO SIO YEYE KUWA CCM...HAPANA MAANA ANA UTASHI WAKE PIA KAMA ULIVYOSEMA ILA HAKUTAKIWA KUEXPOSE HADHARANI HISIA ZAKE ZA UCHAMA ANGETULIA ASUBIRI OCTOBER-25TH akampe kura yake magufuli na sio kuwahadaa wengine kwa kuwashawishi kufuata lake yeye akijua wazi ana mashabiki wengi wanaomkubali nyuma yake na pia nchi ikichukuliwa na UKAWA anajiweka katika mazingira gani???

Nakusoma sana kiongozi sema kwa kuwa yy ni maarufu tu...lkn kila mtu anahisia zake wapo wengi tu ambao wamejipambanua wazwaz kuonesha misimamo yao..
For real democracy yuko sahh kabisa.
Na uwepo wake ccm au uungaji mkono wake hautulazmish cc kufata huki lkn kma tuna ona heri bas tuungane nae ..
Shabiki yeyote atakaye mkimbia kwa sababu hyo atakuwa mpumbavu...
 
Matokeo ya hafla hayo...

Ni kweli tunayaona mkuu kwa wasanii waliyoudhuria ile hafla pale M.city...uku wakikubali kuambiwa na JK kuwa "NITAJARIBU KUWEKA SAWA SWALA LA HATIMILIKI KATIKA KIPINDI HIKI KILICHOBAKI KATI YA SASA NA OCTOBER...NA IKITOKEA SIJAKAMILISHA RAISI AJAYE AKIWA MAGUFULI ATA MALIZIA"...SASA SWALI ZURI KIPINDI CHOTE WALIKUWA WAPI KUKAMILISHA ILO SWALA?
 
Diamond platnumz kaonesha wazi msimamomo wake katika mhonbea anayemtaka yeye. Sipingani na maamuzi yake, ila naona kama alikurupuka kufanya maamuzi hayo.
diamond angetambua kuwa washabiki wake wengi wanaompa sapport hawapo katika mrengo anaoushabikia yeye.
Nimepitia baadhi ya comments za followers wake nakugundua kuwa 90% wamekuwa disappointed sana na alichokionesha.

Halafu ukiangalia ni kama wametumwa hivi baada ya ile hafla yao na mheshimiwa. Maana baada ya pale wasanii kibao wamekurupuka kuonesha support kwa Magufuli.

Kinachoendelea saiv ni kwamba washabiki wameanzisha kampeni ya kutomsapport tena diamond kwa kuacha kumpigia kura katika tunzo anazoshindania.
namuonea huruma sana

Unaposema Diamond kwamba kakosea kumshabikia Magufuli basi unakuwa hujui vinzuri historia ya Diamond. Hao watu watakaomchukia sasa eti kisa anamshabikia Magufuli basi walipaswa waanze kumchukia tangu alipokuwa akisaidiwa na serikali ya CCM.

Diamond ndiye msanii aliyefaidika kwa kiasi kikubwa na uongozi wa Rais Kikwete katika maisha yake ya kimuziki. Mheshimiwa Rais na serikali yake wamekuwa msaada mkubwa sana kwa Diamond. Katika mahojiano na baadhi ya vipindi vya media mfano XXL - Clouds, EFM, Sporah show, na magazeti Diamond amekuwa akieleza wazi kuwa rais JMK amekuwa akimpigia simu mara kwa mara ili kumtia moyo katika kazi zake. Hata JK kwenye hotuba ya kuvunja Bunge hakusita kumtaja Diamond.

Sasa tunapomuona Diamond anakosea, tunapaswa kwanza tujiulize, je huyo mnayemuona anafaa aliwahi kumsaidia kitu gani Diamond katika safari yake ya muziki? Diamond amepata tuzo nyingi tu, je alishawahi hata kumpa hongera kwa tuzo? Au mahaba yenu kwa Lowassa ndiyo mnataka yamuendeshe Diamond katika maisha yake?

Tuache kuingilia uhuru wa watu. Diamond ana kila sababu ya kumshabikia Magufuli na chama chake. Hawa watu wamekuwa msaada mkubwa sana kwa Diamond. Binafsi sijawahi kuona chama chochote cha upinzani kikitoa hata pongezi za kinafiki kwa Diamond. Leo mnataka Diamond aushabikie upinzani, kwa lipi hasa walilomsaidia?

Kama kura za tunzo zinatolewa kwa ushabiki wa vyama basi waache na wasimpigie kabisa. Hii nchi ina watu wa kinafiki sana, eti mnaacha kumpigia kura kisa anamshabikia Magufuli, so what? Ndio maana watu wengi tunaogopa kuchagua upinzani kwa sababu ya visasi vya kijinga kama hivi kwa watu wasiokuwa wafuasi wao. Siasa za chuki namna hii hazitatufikisha popote. Diamond hawezi kushuka kisanii eti kisa watu wa upinzani hawatampigia kura kwenye tunzo. Haitatokea, na kamwe haitaweza kutokea kila mtu ashabikie upinzani, never.

b.jpg

diamond%2Bakiwa%2Bna%2Braisi%2Bkikwete%2Bikulu.jpg

Siku mbili zilizopita ndio picha ya kwanza ya Diamond alipokutana na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ilitoka, walikutana New York na haikujulikana kama kuna kolabo inanukia.

Ilipoanza kolabo ya kimataifa ya wimbo aliofanya na Davido headlines za Diamond zilizidi uzito Afrika lakini kama hii inayoshughulikiwa itafanikiwa basi headlines zake ndio zitakua nzito kuliko.
Sasa kolabo inayonukia sasa hivi ni ya staa wa muziki kutoka Marekani ambae ni Trey Songz ambae taarifa za ndani millardayo.com ilizopata ni kwamba kama kolabo hii ikifanikiwa basi Rais Kikwete atakua ameshiriki kuiunganisha kwa asilimia zaidi ya 90.

Kwenye hii picha President ameonekana akiwa karibu sana na meneja wa Trey Songz na waliongea kwa kirefu, kwa sababu President siku zote anasupport sana Wasanii wake wa Tanzania.
Baada ya Diamond kukutana na Rais kwenye hicho kikao na meneja wa Trey Songz, Diamond alitumia time yake kuandika ya moyoni >>> wapi Utapata Rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa thamani ambao unatafutwa karibu na kila mtu Duniani.. akautumia kukusaidia kukukutanisha na kukuconnect na mdau mkubwa duniani katika tasnia uliyopo ili kuhakikisha tu unafikia malengo na ndoto ya kazi zako…. Dah! Asante sana Mh Rais, Mwenyez Mungu akuzidishie na kukusimamia katika uongozi wako na siku zote za Maisha yako‘

SOURCE: Rais Kikwete na Diamond Platnumz Marekani

Nmrmuona na wema nae kawehuka kbisa.cjui anautaka ukuu wa kitongoji.!!!yaan page ya ya ig adi inaboa.
 
DIAMOND wewe ni mtu mkubwa sana ktk TZ, hakuna dakika inayoenda bila jina lako kuwepo kwenye mitandao au magazeti,radio na tv na kila jambo lako ni mjadala wa kitaifa je alishatokea msanii kama yeye ???? mimi nasema hajawahi kutokea.Back 2 the mada ni hivi DIAMOND ATAKUWEPO SIKU YA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM MWENZENU KESHAVUTA MKWANJA TENA MREFU MNO KULIKO MUNAVYOFIKIRI NYINYI HELA AMBAYO AJAWAHI KUIPATA KTK SHOO ZA TZ. JAPO MIMI NI UKAWA ILA NAMUELEWA YEYE ANAFANYA KWA AJILI YA KAZI SI VINGINEVYO.

Mkuu sawa unachosema na inawezekana ni kweli jamaa kavuta mkwanja lakini tambua mkwanja huo ni kama rushwa flani hivi maana anapiga kampeni tena kabla ata ya muda wake na ungekuwa mkwanja kwa ajili ya KUTUMBUIZA JUKWAANI KWA KAZI YAKE YA MUZIKI ILIBIDI ATANGAZE TAREHE ZA SHOW ZAKE KATIKA KAMPENI ZA CCM NA SIO KUSHAWISHI WATU JUU YA MAGUFULI.
 
Sio laki Tatu tu na matisho juu lisemwalo lipo kama halipo laja wasanii wakiendelea kutumika bila hati miliki lazima ile kwao. Na msanii huwezi Ku shine siku zote sasa wao kuhadaika na ubwabwa wa Mlimani city i feel sorry for them.

Diamond hawezi kutishwa kwa laki tatu, mleta propaganda angefanya kwanza reserch ya kipato cha Diamond na malipo anayolipwa kwenye shoo na matangazo ndipo alete huo uzushi wake.
 
Mkuu sawa unachosema na inawezekana ni kweli jamaa kavuta mkwanja lakini tambua mkwanja huo ni kama rushwa flani hivi maana anapiga kampeni tena kabla ata ya muda wake na ungekuwa mkwanja kwa ajili ya KUTUMBUIZA JUKWAANI KWA KAZI YAKE YA MUZIKI ILIBIDI ATANGAZE TAREHE ZA SHOW ZAKE KATIKA KAMPENI ZA CCM NA SIO KUSHAWISHI WATU JUU YA MAGUFULI.

Wolper mbona hamjamsema? Au anachofanya siyo kampeni kwa Lowassa?
 
Lakini tukumbuke Diamond 2010 Alipigia CCM kampeni sasa mwaka huu tumwache tu.Naona kaamua kuwa timu moja na kipozeo chake WEMA maana huenda tofauti zao wamezivunja
 
Rose Muhando, Prof:- Jay sijaona wakisemwa vibaya na wako Chadema wazi tunawajua mpaka ubunge tunaona wanagombea lakini sijawahi sikia mashabiki wanapiga domo kulikoni kwa Platnumz…!!!! Mi shabiki wa muziki tena Platnumz na ndio msanii wa kwanza Bongo ambae nilishawiahika kununua albamu yake 2010 kamwambie lakin mpaka leo licha ya kufanya show kwenye majukwaa ya maCCM sijawahi kuteteleka cos ye anatafuta chakula so sioni issue ya maana apa ni utoto tu
 
[h=1]diamondplatnumzKitu cha kwanza nlichokipinga Maishani mwangu ni kuchagua kiongozi ambae kutwa kakunja nne tu kwenye AC... kuchakalika nichakalike mie kutwa nzima juani, halaf ye asubiri Pesa ale, SIWEZI KUBALI!!! Atajuaje Matatizo na shida zinazotukabili..??? atajuaje uchungu na thamani ya kazi ninayoifanya..???? Atajuaje kama bajeti ama Mshahara flani hautonitosha kukidhi haja kama mwananchi...??? Atajuaje kama alopewa tenda ya kujenga nchi yangu kweli anaitendea haki...???? Mi sinaga Shanapa za Siasa ila penye Ukweli Siwezi kukaa kimya EVER!!... eti nchi ipate Kiongozi ambae sio imara kesho na kesho kutwa yaanze majanga hata tembele tushindwe nunua... Ntaftie picha na Clip ya Mgombea wako katika Muda wa uongozi wake wote alowai pitia akiwa anawajibika Front kama Hivi.....Tuache kufata Mkumbo, Penye ukweli tuweni wawazi!!!!! Eti Mtu uonekane umepost chama flani Ukipost CCM eti Umehongwa wakati hivyo vyama mvisemavyo ndio vinavyoongoza kutaka kutu*** watu tunakataa!!!!! #HapaKazitu #CcM #TeamMagufuli[/h]
 
Diamond platnumz kaonesha wazi msimamomo wake katika mhonbea anayemtaka yeye. Sipingani na maamuzi yake, ila naona kama alikurupuka kufanya maamuzi hayo.
diamond angetambua kuwa washabiki wake wengi wanaompa sapport hawapo katika mrengo anaoushabikia yeye.
Nimepitia baadhi ya comments za followers wake nakugundua kuwa 90% wamekuwa disappointed sana na alichokionesha.

Halafu ukiangalia ni kama wametumwa hivi baada ya ile hafla yao na mheshimiwa. Maana baada ya pale wasanii kibao wamekurupuka kuonesha support kwa Magufuli.

Kinachoendelea saiv ni kwamba washabiki wameanzisha kampeni ya kutomsapport tena diamond kwa kuacha kumpigia kura katika tunzo anazoshindania.
namuonea huruma sana

Nami nimejiondoa katika upigaji kura kwake na nimejiunnfollow kwenye page zake zote,,,to be honesty sipingani anachokiamini but kweli kakurupuka,,yaan kaingia kwenye siasa kupitia mlango wa nyuma
 
Kijana anajua kutumia fursa ipasavyo,cio mpuuzi yule awe mrahisi kihivyo kujirisk ktk kazi yake kwa ajili ya wanasiasa.cku zote anasema,anafanya kazi yenye maslahi kwake.

Ni vizuri pia akaangalia na hasara!!
 
[h=1]diamondplatnumzKitu cha kwanza nlichokipinga Maishani mwangu ni kuchagua kiongozi ambae kutwa kakunja nne tu kwenye AC... kuchakalika nichakalike mie kutwa nzima juani, halaf ye asubiri Pesa ale, SIWEZI KUBALI!!! Atajuaje Matatizo na shida zinazotukabili..??? atajuaje uchungu na thamani ya kazi ninayoifanya..???? Atajuaje kama bajeti ama Mshahara flani hautonitosha kukidhi haja kama mwananchi...??? Atajuaje kama alopewa tenda ya kujenga nchi yangu kweli anaitendea haki...???? Mi sinaga Shanapa za Siasa ila penye Ukweli Siwezi kukaa kimya EVER!!... eti nchi ipate Kiongozi ambae sio imara kesho na kesho kutwa yaanze majanga hata tembele tushindwe nunua... Ntaftie picha na Clip ya Mgombea wako katika Muda wa uongozi wake wote alowai pitia akiwa anawajibika Front kama Hivi.....Tuache kufata Mkumbo, Penye ukweli tuweni wawazi!!!!! Eti Mtu uonekane umepost chama flani Ukipost CCM eti Umehongwa wakati hivyo vyama mvisemavyo ndio vinavyoongoza kutaka kutu*** watu tunakataa!!!!! #HapaKazitu #CcM #TeamMagufuli[/h]

Hamna chochote hapa #MONDI Anajistukia menyewe hajakatazwa kupost lakini kwanini iwe baada ya hafla ya M.city na sio baada tu ya magufuli kuchagulia mgombea kwa tiketi ya CCM?...mbaya zaidi ni mwendelezo uleule wa wale waliohudhuria ile kwenye hafla ya M.City...sasa kwanini iwe hivyo??...yani KIBA naye akijichanganya tu sina ubia nae!
 
Back
Top Bottom