Nitakua mnafiki nikipita kimyakimya bila kusema neno kwako
Dinazarde, kwanza naomba niweke wazi kua tamko lako hili limenifurahisha sana.
Sijafurahi sababu ya ule upinzani wetu humu uliozoeleka wa Kiba vs Mondi...lah!
Nafurahi kuona wadada wenzangu tunaamka namna hii, sasa tunaelewa matatizo yetu kama Watanzania.
Tumeamua kwa nia ya dhati kabisa kuwa sehemu ya mabadiliko yanayokwenda kuondoa serikali dhalimu ya CCM madarakani.
Nimefurahi sana, hongera zako.
Sikuwahi kufikiria hata siku moja kuwa Dina ana upeo mkubwa kiasi hiki katika masuala ya maslahi ya taifa!Ni furaha iliyoje kuona wana celebrities tumeamka kiasi hiki?
Tumewazidi hata hao wanaojiona wakongwe wa siasa humu JF!