Jumanne Mkota
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 2,987
- 1,757
Kama ni kweli yuko UKAWA basi naahidi kuwa mshabiki wake from today ....
[h=3]UKOO WA CHADEMA BUNGENI WAANIKWA: GAZETI LA UHURU[/h]
BAADHI ya wabunge wameiumbua CHADEMA, wakieleza kuwa chama hicho ndicho kinaongozwa kwa utawala wa kifalme.
"Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa Mwenyekiti wa Chama ana ndugu watatu, Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme? Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, Samahani Mh. Ndesamburo"
Akichangia juzi, muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011,
Assumpter Mshama (Nkenge CCM), alisema utawala wa kifalme upo CHADEMA.
Mfadhili wao amekuja na mtoto wake, kuna mdogo wake, ukienda kwa Lissu kaja na dada yake. Ukienda kwa mwenyekiti wa chama ana ndugu watatu, nani ameleta ufalme zaidi, alihoji.
Aliongeza: Slaa kuna mke wake, nani ana utawala wa kifalme, Ndesamburo amekuja na mtoto wake na mkwe wake, samahani mheshimiwa Ndesamburo.
CCM ilitengeneza utaratibu wa kupata viongozi wa viti maalumu, wao si kifalme tu, tuseme ni kaskazini tu, nawashangaa watu wanaojiita CHADEMA, wenzako wako bungeni huulizi wamepatikanaje.
Kwa upande wake, Livingstone Lusinde
(Mtera-CCM), akichangia jana, alisema CHADEMA ndiyo yenye tabia ya kupeana madaraka kwa kufuata unasaba.
Alisema viti maalumu vimetolewa kwa unasaba, na kama hilo lingefanywa na CCM ingekuwa wimbo kila siku.
Ndiyo maana humu ndani wamo wakwe, dada, kaka, ingekuwa ni kwa CCM ingekuwa wimbo kila siku. Nashangaa wanaposema rais anaongoza kifalme, alisema.
Lusinde alisema wanaotoa vitisho vya kuandamana na kwamba wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba waachwe wafanye hivyo kwani wa kuzuia fujo wapo.
Wanaotaka kufanya vurugu waachwe tu, wengine wanasema wapo tayari kufa kwa ajili ya katiba. Mimi sipo tayari nataka nione katiba mpya, ambayo Watanzania wamekuwa wakiitaka kwa muda mrefu, alisema.
Lusinde aliohoji busara ya wazee wa CHADEMA ambao wameshindwa kutoa kauli baada ya vijana wao kuchafua hali ya hewa.
Mbunge huyo alisema CHADEMA inafanya hivyo kutokana na ahadi ya fedha waliyopewa na Ujerumani.
CHADEMA imesusa kujadili muswada huo unaohitimishwa leo, baada ya kujadiliwa kwa siku nne, kwa kile wanachodai umekosa uhalali kwa kukiuka Kanuni za Bunge.
Hata hivyo, CHADEMA imekuwa ikijibu hoja zinazojadiliwa na wabunge bungeni, kupitia mikutano na waandishi wa habari inayofanyika kila siku mchana, ambapo katika mkutano wa jana imeliomba bunge kutopitisha muswada huo.
Mikutano hiyo imekuwa ikiitishwa na viongozi wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo) na Tundu Lissu (Singida Mashariki), ambaye Jumatatu wiki hii aliwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani Bungeni, kuhusu muswada huo.
Katika maoni hayo, alipendekeza baadhi ya mambo kwenye muswada huo na pia aliwachefua wabunge kutokana na hoja zake kuhusu Muungano na pia kutamka kuwa Tanzania ina urais wa kifalme.
John Lwanji (Manyoni Magharibi-CCM), alisema wanachofanya CHADEMA ni sawa na kiini macho katika mazingaombwe, akitumia neno abrakadebra.
Benardetha Mushashu (Viti Maalumu-CCM), alihoji CHADEMA walitoka bungeni kwa kanuni gani na mbona hawachukuliwi hatua.
Wanawalaghai wananchi, Lissu alichangia muswada. Wanaharakati wanatangaza kufanya maandamano yasiyo na kikomo kama kwamba hakuna serikali, wakijaribu wataona, alisema.
Alisema kinachoendelea Arusha ni matokeo ya maandamano ya kila siku, ambayo hivi sasa yameanza kushamiri Mwanza, ambapo watu wanapigwa mabomu ya machozi.
Libya walianza na maandamano, Gaddafi ameuawa, lakini hivi sasa wanauana, alisema.
Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, amesema hamlazimishi mbunge kuingia kwenye kamati, bali anachofanya ni kufuata Kanuni za Bunge na Katiba.
Alisema hayo bungeni jana, kutokana na malalamiko yanayotolewa na CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwamba, spika alilazimisha wabunge kuingia katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, kujadili muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011.
Spika Anne alisema CHADEMA hawakutumia busara kutoka ndani ya ukumbi wa bunge, bali wangewasilisha hoja zao, na endapo wangeshindwa, basi wangeshindwa kishujaa.
Ccm je? Mme,mke,mtoto- jk,salma,riziwani. Kaka ,mdogo mtu.: jk na membe. Nape na babake.
huyu naye amalize kwanza kesi yake ya kubambikiwa mtoto ndo aje tujadili naye mambo ya ROWASSA
Diamond platnumz kaonesha wazi msimamo wake katika mgonbea anayemtaka yeye. Sipingani na maamuzi yake, ila naona kama alikurupuka kufanya maamuzi hayo. Diamond angetambua kuwa washabiki wake wengi wanaompa support hawapo katika mrengo anaoushabikia yeye.
Nimepitia baadhi ya comments za followers wake na kugundua kuwa 90% wamekuwa disappointed sana na alichokionesha.
Halafu ukiangalia ni kama wametumwa hivi baada ya ile hafla yao na mheshimiwa. Maana baada ya pale wasanii kibao wamekurupuka kuonesha support kwa Magufuli.
Kinachoendelea saiv ni kwamba washabiki wameanzisha kampeni ya kutomsapport tena Diamond kwa kuacha kumpigia kura katika tunzo anazoshindania.
Namuonea huruma sana..
My point is, asingeonesha wazi maana itamletea effect kwenye kazi zake za kimuziki.
Just imagine saiv mashabiki washaanza kampeni ya kutompigia kura kwenye tunzo anazoshiriki. Na nimepitia comments za mashabiki, 90% hawakufurahishwa na kitendo hicho. Unategemea nn? Wakati kura za washabiki ndo zinampa ushindi katika tunzo?
Nashukuru BADILI TABIA kwa kunielewa na wengine PIA,msionielewa its ok lakin nafs zinawasuta vijana tunahitaji mabadiliko,hatutaki watawala tunataka viongozi,kipindi anaingia Kikwete mlisifia msafi ,mzuri lakin kaboronga kila kitu hata Richmond anahusika yeye ndio maana haongelei Hilo,sasa tunamtaka huyo mchafu ndio atuongoze atasafishika Tu,mmempa Richmond na escrow mnapa nani mbona mpo kimya kwa Hilo,Diamond aangalie wananchi wanataka nini aendele Tandale kule aangalie anasahau alipotoka,ye Ni mtu maarufu Ana mashabiki na ndio keshatugawa hivyo hili swala Ni la nchi ingekua mpira sawa,we unaesema nna chuki ndio nna chuki tena kubwa nikiona watu wanavyokufa kwa kukosa huduma,kwa hili Daimond angekaa kimya Tu akaenda mpa kura magufuli,sijasema waniletee pesa tunataka huduma nzuri za kijamii kama wameshindwa ccm na miaka yote wanatawala tunataka mabadiliko,watoto wapate elimu bora,tupate maji safi,yaan hapa wengine mnajifanya kuniponda wakati hata maji ya chupa mnaishiaga kuyaona dukani,mbona nchi zingine zimeweza,sie tusiweze kwa nini,madini tunayo lakin tunaachiwa mashimo Tu,Ni hivi msituibie Tu kura zetu SI mshazoea kuiba safari hii patachimbikaaa tumechoka ,ukiona umebanana kunywa maji baridi yatakupunguzia mhemko msijifanye wote matajiri hapa hamjui maisha ya watanzania wanavyoishi alaaaa
Kutokana na kushabikia ccm, upendo wangu na ushabiki wangu kwake umepoa kabisa. Nyimbo za diamond zikipigwa huwa nazima kama ni radio au tv, na kama niko na serebuka basi narudi kukaa kwenye kiti changu. ..Fafulukti!
Kwahiyo hayo mabadiliko mnayohubiri ni yapi ikiwa wote ni wale wale.Tena CHAGGADEMA ni zaidi maana wao wameanzia kwenye chama siku wakishika nchi(God forbid) watu watalia tu......................
List ya wabunge viti maalumu UVCCM mwaka 2015:
1.Halima Bulembo -Mtoto wa Mwenyekiti Jumuia ya Wazazi Abdalah Bulembo
2.Zainab Katimba -Mtoto wa Maimuna Tarishi aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali mbali
3,Juliana Masaburi-Mtoto wa Meya wa Jiji la Dar Masaburi Didas
4.Mariamu Ditopile-Mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM wilaya ya Sengerema Ditopile Mzuzuri aliyeua Dereve wa daladala
5.Maria Kangole-Mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Onesmo Kongole
6.Sophia Kizigo Mtoto wa Naibu katibu Mkuu UVCCM Taifa Bwana Mafume Kizigo
7.Jaquiline Mzindakya-Mtoto wa Chrisant Mzindakaya ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kwale.
8.Margaret Sitt-Mke wa Samwel Sitta(Mbunge viti maalum 2010-2015)
9.Kawawa,Sokoine, (Watoto wa Mfaume KAwawa na Sokoine Moringe Marehemu)-Ubunge viti maalum2010-2015
Niambie kama CCM ina moroal authority ya kuwanyooshea vidole upinzani.
Kabla hujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako toa kwanza BORITI kwenye jicho lako.
Siku njema.....
Mkuu sijui kama utaeleweka hapa...........................Uchambuzi murua kabisa huu,
Unatakiwa ujue Watanzania wamechoka na ccm kwa mambo kama haya, ndio maana wanataka kuona mbadala wa ccm ambae hatafanana na ccm kwa lolote,
Kama upinzani umeona haya kwa ccm na wao wanarudia na kupita njia ile ile ya ccm, kuna sababu ya kuwa na upinzani nchini?
Mwambieni na Mbowe aache kupiga nyimbo zake pale kwenye lile danguro lake BILICANUS,Na hilo danguro litakuwa linatoa huduma kwa CHAGGADEMA TU.....................
Hivi kwani hapa tunamzungumzia mbowe?
Nimesema sisikilizi nyimbo za diamond, sababu diamond ni mtu wa kutengeneza siyo msanii mwenye kuheshimu taaluma na kipaji yake.
kwasababu haamini chama na mtu unayemtaka wewe au??
Uchambuzi murua kabisa huu,
Unatakiwa ujue Watanzania wamechoka na ccm kwa mambo kama haya, ndio maana wanataka kuona mbadala wa ccm ambae hatafanana na ccm kwa lolote,
Kama upinzani umeona haya kwa ccm na wao wanarudia na kupita njia ile ile ya ccm, kuna sababu ya kuwa na upinzani nchini?