Uchambuzi murua kabisa huu,
Unatakiwa ujue Watanzania wamechoka na ccm kwa mambo kama haya, ndio maana wanataka kuona mbadala wa ccm ambae hatafanana na ccm kwa lolote,
Kama upinzani umeona haya kwa ccm na wao wanarudia na kupita njia ile ile ya ccm, kuna sababu ya kuwa na upinzani nchini?
Mr.Hero,inategemea na njia halisi upinzani hasa kwa Tanzania ulivyoanza.Tujiulize sote ulianza kwa kasi?Ulipokelewaje na wanachama,wananchi,viongozi wa chama Tawala,serikali,polisi,jeshi na wanachi wa kawaida?
Je hatukuaminishwa kwamba upinzani ni uadui,upinzani utaleta vita,upinzani una ukabila,udini nk nk.Tuone vyama vilivyokuwa vikuu kabisa CUF,NCCR mageuzi vilikufaje hivi?Tena vikiwa kwenye PEAK.
Ilikuwa siyo rahisi kwa watanzania wakawaida kukubaliana na vyama vya upinzani,mikoa michache ya mipakani ndiyo ilikuwa ya kwanza kupokea upinzani labda sababu ya mazingira yaliyokuwepo.Na kwa sababu hiyo waliokubali kuingia kwenye harakati za upinzani ni Ndugu wa waliokubali kwa uharaka upinzani napo ilikuwa shughuli kuwabadilisha,familia na marafiki wa karibu.Hivyo kwangu mimi sioni kama tunatakiwa kuwalaumu kwa jinsi ya mengi hawa waliyoyapitia,na ndiyo maana wengi walipewa vyeo ili hasa kuviweka vyama kushikamana.
Wengi waliona CUF na NCCR zilivyokufa hivyo kuhofia hasa haya ya kununuliwa na chama tawala ndipo vyama hivi vilipokuwa na imani kwa wale wa karibu ambao wanaweza kuwa-control.hata JKN alivyoamua kuingia kwenye siasa nina uhakika alianza na waliokaribu naye hasa na aliowaamini.
Na ninachokifikiria baada ya miaka hii ishirini vyama hivi vitajitoa katika kuwapokea ndugu wa karibu na kuwaingiza wengine na kuwaaminisha kama wanaaminika.Nina imani hiyo.Lakini leo miaka 54 CCM imekuwa na tatizo lile lile la kubeba ndugu wa viongozi,kuwarithisha uongozi na kuwaacha watoto wasiyo na careoff kugwaya mtaani,kushindwa hata kuingia kwenye siasa.
Nadhani ningeiona CCM imeamua kubadilika kama haya majina ya watoto wa fulani yangepungua zaidi mwaka huu ili kuwaonyesha watu wanabadilika.
Picha ya watoto wa watawala kuwa ndiyo wenyewe kuingia kwenye SIASA kunanipa hofu kuu kwamba sasa serikali inatengeneza TABAKA LA WATAWALA na ndiyo maana tunasikia kila aina ya sauti.Kama CDM ingekuwa chama TAWALA na kama kina nia ya kuwa CHAMA tawala sitasita kukisema waziwazi kuondoa ile dhana ya WATAWALA wawe ndiyo wale wale na familia zao.
Leo Didas Masaburi anagombea Ubunge Ubungo tuseme anapata,BUNGENI tuna BABA na MTOTO ni wabunge ile hali ya NDIYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO hata kwa sera mbovu hazitaisha.Ila kama assessment ikafanyika akapita mtu kwa quality na siyo kwa pesa yake au kuwa mtoto wa fulani nina uhakika tutajenga bunge lenye confidence kwa watawala.Lakini RUSHWA ni RUSHWA imekaa katika kutoa HONGO ya MWILI,PESA au UNDUGU wa mtu anayegombea.
Leo watoto zaidi ya kumi wanaingia kwa viti maalum au kugombea tunatengeneza UTAWALA wa kifalme taratibu huku tukijua lakini ndani ya CCM wenyewe wanachama mnashindwa kukemea sababu ya uwoga.
Watoto wa MKULIMA hawawezi kuwa watawala wala viongozi sababu ya ELIMU DUNI wanayopewa kwenye shule za kata aka St.KAYUMBA,na hili la kuua ELIMU liko very strategically ili kuendelea kuhodhi madaraka.
Watanzania tulikemee kote siyo tu CCM vyama vyote sasa tuseme basi.