Kwa hili alilolifanya Diamond, litamgharimu sana katika safari yake ya kimuziki

Myopic thinking and poor risk assessiment ..for most of tz artist maisha na maamuzi yao ni kukurupuka tu.....lyf goez on!
 
Napenda kumjulisha msanii diamond platinumz, kuwa kwa tukio lile la jana pale uwanja wa jangwani kuwabeza na kuwakashifu upinzani umejimaliza rasmi! Kumbuka sio ccm pekee ndo waliokuwa wanahudhuria katika matamasha yako, wala kukupigia kura ulipokuwa unawania tuzo mbalimbali, ni watanzania wa itikadi zote.

Sasa kwasababu umeamua kuchagua upande, basi ni upande huo ndo watakao kusupport. Sifa zimejaza kichwa chako mpaka umejisahau na kuona hakuna wa kukuporomosha wala kukufanya chochote. Ungekuwa na busara ungejifunza kwa yaliyomkuta Marlow baada ya kufanya kama ulivyofanya wewe, leo hasikiki tena.

Nimeshangaa wewe kuwepo kwenye kundi la watu wanaowaona vijana kama sisi ni wapumbavu, malofa na vibaka! Mimi Naamini pamoja na watanzania wengine tumechukua hatua ya kukuunfolow katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Pia sitokaa kukupigia kura wala kushiriki kwenye tamasha lako lolote.

Ni hayo tu na maamuzi yangu ya kipumbavu na kilofa.

Asante..
 
Diamond ni lofa kama anafikiri yeye ana ushawishi mkubwa kwenye jamii wa kuweza kumuingiza magufuli ikulu
 
Ukawa mnazo siasa za kibaguzi , na mleta mada lazima utakuwa miongoni mwawo sisi sote tunajenga nchi moja kwa siasa utaambulia kula yako mwenyewe
 
Last emperor,
Umeanza kufuatilia siasa lini? Hivi huyo Marlaw mnayempigia mfano kila siku mnaamini hafanyi muziki kwa sababu aliwafanyia kampeni CCM? Marlaw amefunga ndoa na Besta... hawa wote ni wanamuziki lakini tangu wafunge ndoa, si Marlaw wala Besta anayefanya muziki hivi sasa... sasa ni kwanini mnadhani kinachomfanya Marlaw asifanye muziki ni hatua yake ya kuipigia kampeni na si tu kwamba wamekubaliana mtu na mke wake waachane na muziki ili kuepusha majaribu ya ndoa? Do I need to remind you kwamba kuna wasanii kibao ambao hatimae uamua kuachana na sanaa baada ya kuingia kwenye ndoa?

Tuchukue assumption yenu kwamba kilichomlostisha Marlaw ni kampeni za CCM! Why only Marlaw na si wasanii wengine ambao walimpigia JK kampeni na bado hadi leo hii wapo kwenye game? Hata huyo Diamond unayesema ndo keshajimaliza ina maana umesahau kwamba alikuwepo kwenye kampeni 2010? Mbona Chege na wenzake wote wapo wakati wote walikuwapo 2010 lakini kupotea kwa Marlaw tu uwe ndo mfano?

Acheni watu wapige pesa... hata hao wanasiasa mnaowaunga mkono wenyewe nao wapo kimaslahi!
 
Last edited by a moderator:
Tusipojiangalia siasa zitatufanya tuwe wenda wazimu....kila mtu anauhuru na haki ya kuchagua upande autakao jamani,mwisho na kelele za haya yote ni 26 oct!duh na ifike haraka maana inachosha masikioni
 
Mimi sina shida na yeye kuchagua chama cha kushabikia, lakini ukishaamua kuchagua upande aelewe upande wa pili ameisha ukataa, na sisi tuna mkataa. Ninawakilisha sauti ya mtaa.. In every action there is reaction
 
Diamond umaarufu wenyewe aliupatia kwenye kampeni za ccm kwa maneno yake mwenyewe, kwa hiyo huo ni wivu tu, uguza kidonda
 
Diamond alishiriki kampeni za ccm za 2010 na baada ya kampeni zile diamond nyota yake imeng'aa zaidi acha wivu wa kike we mpumbavu..!!
We lofa kuna tofauti kati ya 2010 na 2015!Hapa nazungumzia katunga kabisa nyimbo kutukana wapinzani. 2010 alikuwa mburudishaji wa kawaida, na ilitakiwa aendelee katika mfumo huo. Unapiga hela unaenda zako. Yoyote anaekuja na hela unachukua hela unafanya kazi unapita hivi, sasaiv yeye ameamua kuwa kada.. Tutaona, nitakuja kuwakumbusha haya hapa..
 
Ikumbukwe kuwa diamond is a businessman and biashara yake kubwa kabisa inayomuingizia pesa ni muziki sasa kama alipewa kazi na CCM unataka asiifanye kisa nini kumbuka biashara yake haichagui nani wa kumuhudumia he is like the whole seller na sio Niche businessman
 
Domo ana dharau kisa yy katoka kimaishaa ila nini ikulu hataenda tena ngoja tubebe nchiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…