Napenda kumjulisha msanii diamond platinumz, kuwa kwa tukio lile la jana pale uwanja wa jangwani kuwabeza na kuwakashifu upinzani umejimaliza rasmi! Kumbuka sio ccm pekee ndo waliokuwa wanahudhuria katika matamasha yako, wala kukupigia kura ulipokuwa unawania tuzo mbalimbali, ni watanzania wa itikadi zote. Sasa kwasababu umeamua kuchagua upande, basi ni upande huo ndo watakao kusupport. Sifa zimejaza kichwa chako mpaka umejisahau na kuona hakuna wa kukuporomosha wala kukufanya chochote. Ungekuwa na busara ungejifunza kwa yaliyomkuta Marlow baada ya kufanya kama ulivyofanya wewe, leo hasikiki tena. Nimeshangaa wewe kuwepo kwenye kundi la watu wanaowaona vijana kama sisi ni wapumbavu, malofa na vibaka! Mimi Naamini pamoja na watanzania wengine tumechukua hatua ya kukuunfolow katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Pia sitokaa kukupigia kura wala kushiriki kwenye tamasha lako lolote. Ni hayo tu na maamuzi yangu ya kipumbavu na kilofa. Asante