Simiyu Yetu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 18,949
- 4,639
Mpuuzi sana huyu mkuu badala ya kwenda kwenye hoja na akamkosoa anakwenda kwenye matusi,wacha sasa aone kama ni vizuri.
nkoyi kazi kweli bayanda balele matusi ni asili yao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpuuzi sana huyu mkuu badala ya kwenda kwenye hoja na akamkosoa anakwenda kwenye matusi,wacha sasa aone kama ni vizuri.
Mkuu wanapeleka kule kwa sababu ndipo wanapopata ufadhili wa fedha wanazochezea.
Sasa unategemea watu wachangie nini kwenye hizi cheap propaganda zako. kwani wakienda kwa Lori, baskeli, mkokoteni au kwa miguu kuna tofauti gani??
halafu simiyu kwetu ni kondoo ambaye ni masenge.ndiyo akili yenu ilivyo hapa umejibu au umeanzisha kitu kipya upeo wako ndiyo umeishia hapo?,unawaza kinyesi kama ndiyo chakula chako.
Lusewa, hii thread yako ingeuliza zaidi ili ueleweshwe kuliko kuilaumu chadema huku ukionekana huna data.
Mosi, Chadema watafanya uchambuzi na kuyawasilisha kwa tume. Hata hivyo, lazima wapeleke ushahidi wa watanzania waliotoa maoni yao. Fomu za kubeba kwa Lorry ni attachement mkuu ya ushahidi, siyo uchambuzi wa chadema. Tuna wanasheria mahiri sana akina Tundu, mabere, kibatala, prof Abdallah safari,Msanda kwa kuwataja waachache.
Pili, unasema viongozi wa chadema wamefanya hivyo ili waongeze Per Diem. Hapo ama hujui, ama unajidanganya au unapiga propaganda. Chadema wabunge wake wote hawapewi chochote, tena wanatoa magari yao bure na wakati mwingine wao ndo wanachangia. Kale karuzuku kanakotoka serikalini ni asilimia ndogo sana ya matumizi ya chadema. Ndo maana Mbowe aliwaambia ccm kama wanaweza wafute, sisi chadema tuko tayari kuishi bila ruzuku. Hakuna kiongozi wa ccm aliyemjibu Mbowe mpaka leo.
Tatu, Suala la Zitto lililetwa humu kipropaganda siku chache zilizopita. Mwana habari wa chadema akaleta majibu sahihi. Ukweli ni kwamba zitto amebanwa na kazi nyingi kwenye kamati yake ya Bunge. Kumbuka ni kamati ya PAC na POAC zilizounganishwa. Kama mimi nadanganya tuma PM kwa zitto atakupa ukweli. Said Arfi wengine ktk maeneo yao walishiriki vizuri sawia. Unless unataka awepo kwenye Chopa ambayo uwezo wake ni watu 5 pamoja na Pilot. Mbona hulalamikii Lema, wenje, msigwa au Hamad kutokuwepo? Kwanini unawataja hao tu?
Nne, unasema chadema wamechelewa kukusanya maoni na hadi 27 august wako wanakusanya na kwamba kwa kufanya hivi, hawana muda wa kuchambua maoni. Naomba nikuambie hivi, Chadema ina organization nzuri. Siyo lazima kwamba uchambuzi wa maoni uanze baada ya ziara ya chopa kuisha. Uchambuzi unaendelea huku Chopa iko mitaani. kazi zinafanyika usiku na mchana. Wewe unadhani wakati mbowe na slaa wako chopa akina Prof Adallah safari wamelala?
Kwa kuhitimisha,
Chadema itapeleka uchambuzi mzuri wa maoni yaliyokusanywa tena uchambuzi ulioandikwa na wanasheria mahiri wanaoheshimika hadi makamu zote hapa nchini. Pili, uchambuzi huo utaambatana na lori lenye fomu husika (kama utaratibu utabakia hivyo) ili ccm wasije wakapiga propaganda kwamba tumejifungia vyumbani tukaandika maoni ya Mbowe na Slaa.
NB; Kumbuka kila fomu ina namba ya simu na mahali anapoishi ya mtoa maoni, ni ushahidi wa uhakika. Kumbuka chadema ni chama cha siasa cha kitaifa inayofanya vitu kisomi. ASANTE.
halafu simiyu kwetu ni kondoo ambaye ni masenge.
Mods, tafadhali msiunganishe uzi huu na nyingine.
Wana JF,
Wakati akifunga Mikutano ya kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Rasimu ya Katiba kwenye viwanja vya Mwembeyanga, wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Agosti 2013, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr WILBROAD SLAA alisema kuwa, watapeleka maoni hayo kwenye ofisi za Tume kwa LORI kwa kuwa ni mengi. kwamba, CHADEMA kimefanya mikutano 49 katika mikoa tisa ambapo jumla ya wananchi milioni tano walitoa maoni.
Ikumbukwe kuwa CHADEMA kama taasisi ni baraza la katiba na kwa hali hiyo ilikuwa na uhalali wa kukaa kama taasisi kukusanya na hatimaye kuchambua maoni ya wanachama wake juu ya Rasimu ya Katiba. Hata hivyo, mbinu walizotumia hazikufanikisha lengo. Baada ya ya kutafakari kauli hiyo ya Dr SLAA, mapungufu yafuatayo yamebainika katika mchakato wa kukusanya maoni ya Rasimu ya Katiba ndani ya CHADEMA.
- Imedhihirika kupitia kauli hiyo ya Dr Slaa kuwa CHADEMA hawakuelewa nini cha kufanya katika kuchambua Rasimu ya Katiba na kutoa maoni ya Taasisi. kutokana na hali hiyo, CHADEMA wamejikuta wakifanya mikutano ya hadhara ikiwahusisha wananchi ambao ni wafuasi wa CHADEMA na vyama vingine vya siasa pamoja na wale wasio wafuasi wa vyama vyovyote vya siasa. Kwa hali hiyo, maoni waliyokusanya CHADEMA si maoni ya taasisi na kwa kiasi kukubwa yameshabihiana na yale yaliyokusanywa na tume. Lawama kubwa naielekeza kwa Tume ya Katiba chini ya Jaji WARIOBA kwa kutotoa semina ya kutosha kwa viongozi wa CHADEMA juu ya mchakato huo.
- CHADEMA walihangaika na kupata idadi kubwa ya watoa maoni badala ya kuchambua Rasimu ya Katiba. Kauli kuwa Chama hicho kimekusanya maoni milioni tano katika mikoa tisa inadhihirisha kuwa lengo lao kubwa ni kutaka kushindana na CCM baada ya kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, ABDULRAHMAN KINANA aliposema kuwa CCM wamekusanya maoni ya wanachama milioni mbili
- CHADEMA kimekosa watu makini ambao wanaweza kuchambua maoni waliyokusanya na kuwasilisha kwa Tume yakiwa yamechambuliwa. kutokana na umbumbumbu wa viongozi wa CHADEMA, Dr Slaa amejikuta akitoa kauli ambayo imekiaibisha chama chake. hii ni tofauti na CCM ambao wamekusanya maoni hayo na kuchambua kuanzia ngazi ya matawi hadi Taifa na hivyo kupeleka kwenye tume kwa njia ya soft copy. Bado najiuliza, ikiwa Tume wangeamua kutumia utaratibu wa CHADEMA wa kukusanya tu maoni pasipo kuchambua, je leo hii tungejadili Rasimu ya KATIBA?
- Ubabe wa viongozi wa CHADEMA umevuruga mchakato wa kujadili Rasimu ya Katiba ndani ya chama hicho. viongozi wa ngazi za juu wa CHADEMA hasa Mwenyekiti na Katibu Mkuu hawashauriki. Ingawa baadhi ya viongozi waandamizi walitoa ushauri mahsusi kwa viongozi hao juu ya namna nzuri ya kukusanya na kuchambua maoni ya Rasimu ya Katiba kutoka kwa wanachama wao, imebainika kuwa viongozi wakuu hawakuwa tayari kupokea ushauri huo.
- CHADEMA walikuwa nyuma ya muda katika mchakato wa kukusanya na kuchambua Rasimu hiyo. Ikumbukwe kuwa mwisho wa kuwasilisha maoni ya mabaraza ya katiba kwenye tume ni Tarehe 31 Agosti 2013. Hadi tarehe 27 Agosti 2013, CHADEMA walikuwa wanaendelea kukusanya maoni kutoka kwa wananchi. kutokana na hali hiyo, ni wazi kuwa CHADEMA wasingeweza kukaa kama taasisi na kuchambua maoni hayo kwa vile viongozi wa juu wa chama hicho walikuwa wanahangaika kutafuta idadi kubwa ya watoa maoni. Aidha, kuna taarifa kuwa Katibu Mkuu, Dr SLAA ameanza ziara visiwani Zanzibar tarehe 29 Agosti 2013 hali ambayo inadhihirisha kuwa viongozi wa chama hiki hawajui watendalo.
- Tamaa ya fedha ya viongozi wa juu wa CHADEMA ndiyo imechangia kuvuruga mchakato ndani ya chama hicho. viongozi wakuu walitawaliwa na tamaa ya fedha hali iliyolazimu viongozi hao kutembea maeneo mengi tena mengine ambayo yana wabunge wao ili tu perdiem iongezeke. aidha, tamaa hiyo ya fedha imefanya baadhi ya viongozi wengine wasishirikishwe kwenye mchakato huo. Mathalan, katika mchakato huo, sijaona ZITTO KABWE, SAID ARFI, SHIBUDA na wengineo wakishiriki ipasavyo
My TAKE: Ninachokiona ni kuwa CHADEMA wamegomea mchakato wa katiba BILA YA KUJIONESHA (PASSIVE RESISTANCE). Kwani kitendo cha CHADEMA kutokuwa makini katika kukusanya na kuchambua maoni ya wananchi ikichagizwa na uamuzi wa chama hicho kupeleka maoni hayo kwa njia ya LORI ni wazi kuwa yakiwasilishwa kwenye tume yatapigwa kiberiti na mchango wa CHADEMA hautakuwepo. Ikumbukwe kuwa Jaji WARIOBA alisema kuwa hawatapokea maoni ya CHOPA, je kitendo cha kupeleka kwa njia ya LORI si kitaongeza hasira zaidi kwa WARIOBA? Tusubiri hiyo tarehe 31 AGOSTI 2013 mbivu na mbichi zitajulikana
Kinachokusumbua hapo ni lugha ya picha.