Kwa Hili la CHADEMA kupeleka Mapendekezo ya Rasimu ya Katiba kwa Lori, ni Umbumbumbu wa hali ya juu

Kwa Hili la CHADEMA kupeleka Mapendekezo ya Rasimu ya Katiba kwa Lori, ni Umbumbumbu wa hali ya juu

Ni wale tu walioweka akili zao rehani wanaweza kusema namna hii na kwa wepesi wa hoja km huu unaonesha si uhalisia ila chuki za mtu kwa CHADEMA. Heri anayepeleka maoni ya wananchi wake kwa lory aliyokusanya hadharani kuliko wale waliowarubuni watu kwa kwenda na maoni yao kufungia watu kwenye vyumba na kuwambia cha kusema kisha kusuka takwimu za uwongo.
Time is over. If you don't accept changes, changes will change you. Let's wait.
KIGUMU Chama cha Mapinduzi
 
  1. Tamaa hiyo ya fedha imefanya baadhi ya viongozi wengine wasishirikishwe kwenye mchakato huo. Mathalan, katika mchakato huo, sijaona ZITTO KABWE, SAID ARFI, SHIBUDA na wengineo wakishiriki ipasavyo

My TAKE: Ninachokiona ni kuwa CHADEMA wamegomea mchakato wa katiba BILA YA KUJIONESHA (PASSIVE RESISTANCE). Kwani kitendo cha CHADEMA kutokuwa makini katika kukusanya na kuchambua maoni ya wananchi ikichagizwa na uamuzi wa chama hicho kupeleka maoni hayo kwa njia ya LORI ni wazi kuwa yakiwasilishwa kwenye tume yatapigwa kiberiti na mchango wa CHADEMA hautakuwepo. Ikumbukwe kuwa Jaji WARIOBA alisema kuwa hawatapokea maoni ya CHOPA, je kitendo cha kupeleka kwa njia ya LORI si kitaongeza hasira zaidi kwa WARIOBA? Tusubiri hiyo tarehe 31 AGOSTI 2013 mbivu na mbichi zitajulikana

RED: Yupo kwenye majukumu ambayo mafisadi walipenda asiyefanye ili waendelee kuchakachua-CDM walishtuka
BLUE: Yuko India kwa upasuaji wa Nyonga
GREEN: Maoni yake yapo kwenye mawasilisho ya CCM
BOLD: Watashirikishwa kwa hatua za mwisho..

Mleta mada, unaweza ukawa umesoma ila si TAALUMA zote....!
Unaposema TAASISI unaelekea kutoelewa maana ya Taasisi hata kidogo!
Mie sijawahi kuona mahali popote hata wakati wa Wagiriki ambako kila mtu anashiriki kwenye suala lilelile kwa asilimia mia!
CHADEMA wanaweza kukusanya maoni kwa watu mbalimbali LAKINI hayo maoni ya watu wakayaunganisha katika maoni ya chama kama TAASISI!
Kitakachopelekwa TUME si maoni ya mtu mmojammoja bali maoni yaCHADEMA mbayo yamegusa mawazo ya watu mbali mbali!
Utaasisi wa taasisi hauji kwa kila mtu kushiriki asilimia mia.
Nenda tena shule
 
Mmmh, bora nipite tu kwani uzi wenyewe umeletwa na mtu mmoja na mtu huyo huyo ndiye ameuendeleza peke yake.@LOKISA achana na kilza huyu. mtajitaja kwa avatar nyingi ila mawazo na uelewa wenu utabaki uleule.

Mhhhh, kwani kinachojadiliwa ni uzi au watu?
 
RED: Yupo kwenye majukumu ambayo mafisadi walipenda asiyefanye ili waendelee kuchakachua-CDM walishtuka
BLUE: Yuko India kwa upasuaji wa Nyonga
GREEN: Maoni yake yapo kwenye mawasilisho ya CCM
BOLD: Watashirikishwa kwa hatua za mwisho..

Mleta mada, unaweza ukawa umesoma ila si TAALUMA zote....!
Unaposema TAASISI unaelekea kutoelewa maana ya Taasisi hata kidogo!
Mie sijawahi kuona mahali popote hata wakati wa Wagiriki ambako kila mtu anashiriki kwenye suala lilelile kwa asilimia mia!
CHADEMA wanaweza kukusanya maoni kwa watu mbalimbali LAKINI hayo maoni ya watu wakayaunganisha katika maoni ya chama kama TAASISI!
Kitakachopelekwa TUME si maoni ya mtu mmojammoja bali maoni yaCHADEMA mbayo yamegusa mawazo ya watu mbali mbali!
Utaasisi wa taasisi hauji kwa kila mtu kushiriki asilimia mia.
Nenda tena shule

Mkuu, kuhusu kukusanya maoni, Tume ilishafanya hivyo. baada ya mchakato huo kukamilika, Rasimu ya Katiba iliandaliwa. kinachoendelea ni mabaraza ya katiba kujadili rasimu hiyo na kutoa mapendekezo yao. CHADEMA hawakuweka baraza la katiba badala yale likaendesha mikutano ya hadhara kurudia kile kile kilichofanywa na tume. hapo ndipo walipojidhihirisha kuwa hawakujua wafanyacho
 
Hivi huko CCM hata lugha ya picha mliosoma Form III iliishia wapi! Mtu kusema lori basi imekuwa taabu!!
 
Dr slaa kwa kamba hajambo,watu million tano wametoa maoni katika mikutano 49,mbona hesabu inakataa wajameni,ukichukulia kwamba hiyo mikutano wao ndo walikua wakiongea na kutoa mda mfupi tu kwa watu kutoa maoni,hao milioni tano walitoa maoni wapi na saa ngapi?
 
mtoa mada alishatoa hukumu kabla ya kuwasiliana na Chadema ili ajue kwanini wanatumia lori.Its amazing mtu anapost one sided story bila kuhusisha mhusika au msemwa.
Mimi sio mwanaChadema na sina Chama ili ni muumini wa magaeuzi
Chadema wataeleza kwanini wametumia Lori, na hiyo sio hoja ya kujadili.
tunatakiwa kujadili kilichomo katika hilo lori wakishakabidhi na sio kujadili lori

Mkuu, tupe basi tafsiri ya LORI kwa mujibu wa Kamusi ya CHADEMA
 
CHADEMA hawakuweka baraza la katiba badala yale likaendesha mikutano ya hadhara kurudia kile kile kilichofanywa na tume. hapo ndipo walipojidhihirisha kuwa hawakujua wafanyacho

Tehe!
CHADEMA wana akili kama utakavyoona huko mbeleni!
Na niwajuavyo CHADEMA waliona mbali hadi kufanya walivyofanya...
Ni bahati mbaya nyie hamjajua kati ya mawazo ya wananchi yaliyochukuliwa na TUME na maoni ya wana-CHADEMA yatakayowasilishwa TUME kwa mkono wa CHADEMA!
Ni halali yako kusema hawakujua wafanyalo kwa sababu hii ni pilipili usiyokula....
Huwezi kujua mantiki ya CHADEMA kwa kutumia akili ya CCM.
 
Back
Top Bottom