Kwa hili la homa ya Ini, Serikali haiko makini na afya za raia wake. Raia wote wangepatiwa chanjo bure

Kwa hili la homa ya Ini, Serikali haiko makini na afya za raia wake. Raia wote wangepatiwa chanjo bure

Parabora

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2019
Posts
1,504
Reaction score
2,221
Kuna muda unashindwa kuelewa kama viongozi waliopo madarakani wapo kwa maslahi ya wananchi na Taifa hili kwa moyo wa dhati, leo asubuhi vyombo vingi vya habari ikiwemo magazeti wameandika na kuzungumzia usambaaji wa kasi wa hii homa ya Ini. Homa ambayo watawala hawajaichukulia kwa uzito wake kuwakinga Raia na watanzania masikini wa nchi hii.

Hii chanjo ni gharama sana na sidhani raia wengi walio maskini wataweza kupata chanjo ya kujikinga na ugonjwa huu., na kibaya Zaidi matibabu yake yameondolewa kwenye bima ni unalipa Cash (Hii ina maana kwamba serikali inajali kodi kuliko afya za raia wake). Watanzania ni mungu tu huwa anaetuepusha na majanga na hili tuombe tu atuepushe la sivyo tutapukutika kama kuku wa mdondo.

Hii nchi ina rasimali za kutosha lakini ukweli ni kwamba hazitunufaishi kwa chochote kila kitu serikali inataka tulipie hata chanjo hii ambayo inasemekana ni ya ugonjwa hatari zaidi hata ya HIV si mgefanya bure kama mnawapenda wananchi wenu wanaowaweka madarakani, Ina maana serikali haitaki watu waishi wakifurahia maisha pia waepukane na magonjwa.

Inatia uchungu sana ingekuwa ni nchi zinazojali utu mpaka sasa asilimia kubwa ya wananchi wake wangekuwa washapewa chanjo tena bure na hapa ndipo ninapowaona Mabeberu ni watu kuliko sisi, angalia wanavyowakinga raia wao kwenye majanga na magonjwa ya mlipuko.

Lakini hapa kwetu tunajali kodi kuliko afya za raia tena wengi walio masikini, mfano angalia statement ya juzi ya raisi kuhusu waliokufa kwa kupata majanga ya mafuriko huko mkoani Lindi, Ni kweli hawa watu yawezekana wanaishi mabondeni lakini serikali inapokea pesa ya kodi ya ardhi na majengo yao yaliyo hukohuko mabondeni na kuna watu wana biashara huko na serikali inapokea kodi yao kuendeshea miradi mbalimbali ila wakipata majanga serikali haiwajali...Wao wanachojali ni kodi tu.. Mnaudhi sana.

Ifike sehemu serikali iwe na huruma kwa raia wake tena hii ni serikali ya wanyonge maana Kwa tafiti chache zilizofanyika mpaka mwaka 2018 iligundulika kuwa kati ya watu 117 ni mtu 1 tu anakuwa ameathirika na virusi vya UKIMWI/VVU lakini ni watu 22 wanakuwa wameathirika na HOMA YA INI sawa na asilimia 18.8% lakini pia vifo vilivyosababishwa na homa ya ini kwa report ya dunia mwaka 2018.

ilikuwa ni mil 1.35 kwa mwaka na idadi kubwa ilikuwa ni raia kutoka Africa. na kwa hapa nchini kwa takwimu za wizara ya afya mwaka huohuo 2018 WACHANGIAJI damu 13,613 kati ya 307,835 waliojitolea damu walibainika kuwa na maambukizi ya virusi vya homa ya ini.Bado naishauri serikali hii ya wanyonge,Hili gonjwa liangaliwe kwa jicho pana na zile nguvu zinazotumika kupambana na ukimwi zihamishiwe na huku pia

Wakuu HOMA YA INNI ni moja kati ya mangonjwa hatari sana kama una uwezo nenda kapime na upate Kinga

Nawaonea huruma sana wananchi maskini wa nchi hii.
 
Hii homa ni janga japo serikali haijaweka mkazo, naunga mkono andiko chanjo itolewe bure na wahudumu wa afya wapelekwe karibu na jamii, kwa mfano wawe na siku maalum za kuwa wanatoa hii chanjo kwenye serikali za mitaa
 
Pamoja na kwamba serikali haijali raia wake, raia wenyewe ni tatizo zaidi maana hawajui wala hawadai haki zao wapo tu kuomba huruma/kusaidiwa wakati wao ndio wanaolipa kodi. Wenzetu mkate tu ukipanda bei hapakaliki sisi tumekalia ndio mzee. Hacha tusio na uwezo wa kulipia chanjo tufe maana tumeyataka.

Leo utasikia wananchi wakishabikia miradi mikubwa ikipewa kipaumbele kuliko ustawi wao lakini janga kama hili tunaomba huruma ya serikali. Ni ujinga uliopitiliza.
Mfanyakazi anakatwa pesa za bima lakini anaambiwa hawezi kutibiwa kwa bima anakenua tu. Nasema acha tufe ili kije kizazi kinachojitambua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wee jamaa umetumwa na mabeberu, unataka serikali ikose fedha za kujenga Stiegler's gorge na SGR kisa ugonjwa wa ini!
 
Unategemea serikali ikupe chanjo? Tena bure? Embu acheni utani. Mjue hata hizo campaign za kuhamasisha na kuelemisha kuhusu ukimwi. Dawa za ARV, vipimo vya Viral load etc vyote ni kwa msaada wa watu marekani na mashirika mengine. Ukikaa kutegemea serikali hata malaria itatuua na kutumaliza wote.

Wao wanajua kujilipa mishahara na posho etc wananchi haiwajali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afya kwanza kaka, maana hata hiyo miundombinu bila watu sio chochote
Nani kakudanganya kuwa serikali hii inajali afya za wananchi wake?

Shukuru sana hisani ya watu wa Marekani kwa kugharimia baadhi ya chanjo.
 
Unategemea serikali ikupe chanjo? Tena bure? Embu acheni utani. Mjue hata hizo campaign za kuhamasisha na kuelemisha kuhusu ukimwi. Dawa za ARV, vipimo vya Viral load etc vyote ni kwa msaada wa watu marekani na mashirika mengine. Ukikaa kutegemea serikali hata malaria itatuua na kutumaliza wote.

Wao wanajua kujilipa mishahara na posho etc wananchi haiwajali.

Sent using Jamii Forums mobile app
unajua ulichoandika ndugu yangu…, au umeamua tu kuchangia..
 
Nani kakudanganya kuwa serikali hii inajali afya za wananchi wake?

Shukuru sana hisani ya watu wa Marekani kwa kugharimia baadhi ya chanjo.
sasa hao wanyonge watajaliwa na nani, au kuna wanyonge wengine Zaidi ya hao
 
sasa hao wanyonge watajaliwa na nani, au kuna wanyonge wengine Zaidi ya hao
Wanyonge watahamasishwa kuunga juhudi za JPM na kumpigia kura. Afya zao Mungu anajua.
 
Serikali yako ya wanyonge imeweka mambo waazi kabisa.
Kanunue kifurushi cha bima ya afya. Kwa mwaka haizidi milioni moja pungufu unaongea.
 
Serikali yako ya wanyonge imeweka mambo waazi kabisa.
Kanunue kifurushi cha bima ya afya. Kwa mwaka haizidi milioni moja pungufu unaongea.
mimi ninayo mkuu but hainisaidii kunitibu homa ya Ini,
 
Back
Top Bottom