Kwa hili la Inyala, Mbeya ninampinga Makamu wa Rais Dr. Mpango kwa agizo lake "quick fix" na kumsihi awe serious na maisha ya Watanzania

Kwa hili la Inyala, Mbeya ninampinga Makamu wa Rais Dr. Mpango kwa agizo lake "quick fix" na kumsihi awe serious na maisha ya Watanzania

Unalionaje agizo la Dr. Mpango?

  • Zuri linafaa sana

    Votes: 4 21.1%
  • Halifai kabisa

    Votes: 15 78.9%

  • Total voters
    19

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Katika taarifa yake kuhusu ajali ya pale Inyala Mkoani Mbeya iliyoua watu kadhaa pamoja na DED wa Igunga, Gazeti la Mwananchi limetoa taarifa kwamba ajali hiyo imetokea ikiwa ni siku tatu zimepita baada ya Makamu wa Rais Dkt. Mpango kutoa maagizo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kuanza ukaguzi wa magari ya mizigo katika eneo hili.

Sasa nashindwa kuelewa busara ya Makamu wetu wa Rais kwamba suluhisho la kuzuia ajali pale Inyala ni kuyakagua magari ya mizigo kabla hayajapita kile kipande cha barabara. Hili nalipinga kwa dhati. Nimeshindwa na hata kuchukizwa na jinsi watu walio na madaraka nchini kama Dkt. Mpango wanavyoyachukulia mambo mazito kirahisi namna hivi.

Hili ni eneo ambalo karibu kila wiki panatokea ajali mbaya sana, na Dkt. Mpango anasema kagueni magari kabla hayajapita hapa. Hii ni busara kweli?

Kwanza Dr Mpango amejiuliza inachukua muda gani kukagua lori moja? Ukiweka utaratibu wa kukagua malori pale atapata wapi wakaguzi wa kutosha ili kutosababisha msongamano wa malori pale? Hajafikiria kwamba tunaweza kukuta lori linakaa pale siku mbili likisubiri kukaguliwa ili lishuke au kupanda mlima? Hebu atembelee mizani kwanza aone ikiwa mizani hali ndio hiyo, kukagua breki za magari itakuwaje. Yaani viongozi wanaongea tu, wanatoa tu maagizo "impractical" kirahisi!

Anapaswa kuelewa nini kinasababisha ajali pale kabla ya kutoa kile tunaita utatuzi wa kisiasa kwa tatizo la kisayansi.

Kwa kumsaidia tu na kumpa ushauri wa bure usio wa kisiasa, ni kwamba kuna sababu kubwa tatu zinazosababisha ajali pale;
  1. Barabara imeharibika sana na kuweka matuta ya lami kudidimia ambayo mara nyingi yanakulazimu kupita upande usio wako wa barabara au kupoteza control ya gari unapopanda tuta kwa sababu gari zinayumba sana kwenye haya matuta
  2. Hiyo sehemu ina mlima/mteremko wa umbali mrefu
  3. Hiyo sehemu ni ya solid line ambayo huwezi ku-overtake gari nyingine (japo madereva wa mabasi hawajali hili)
Sasa Dkt. Mpango anapaswa kutoa wazo la kuzuia ajali pale kwa kuangalia hizo sababu tatu. Na kwa mawazo tu, haya yanapaswa kufikiriwa na Serikali ili kuzuia vifo na ajali za kila wakati eneo hili;
  1. TANROAD waamrishwe kutengeneza hili eneo haraka sana. Matengenezo yanayotakiwa hapa ni kama yale yaliyofanyika mteremko wa Kitonga katika kuzuia barabara kuweka matuta kutokana na uzito wa malori.
  2. Kwa kuwa hili ni eneo la mlima/mteremko wa umbali mrefu, pawekwe climbing lane ili kuwepo na njia tatu na ambayo moja itatumiwa zaidi na malori yanayopanda taratibu sana eneo hili
  3. Zaidi ya kuweka climbing lanes, eneo hili liwekwe "lay-by" kadhaa (yaani michepuko katika barabara iliyo kama sehemu ya kituo cha basi) ili madereva wanaopanda au kuteremka wawe na eneo la kuingia pale wanapoona gari lao linaanza kuleta matatizo na kulifanyia marekebisho, badala ya kusimamisha lori barabarani eneo la hatari.
Mwisho, ninawaomba sana viongozi wetu jaribuni kuwa serious na matatizo yanayowakabili Wananchi, hasa yale yanayosababisha vifo. Msitangulize kukimbia gharama za kutatua matatizo kama haya na kupendekeza majibu ya kisiasa ambayo hayatatusaidia. Kama tatizo ni fedha, tunakatwa sana tozo, tumieni hizo pale Inyala kama suala la emergency.
 
Wapigwe kisiasa
Bila hivyo tunayo safari ndefu bado. Zingatia mkurugenzi alipaswa kusubiri malori kupita. Asubiri vipi mlamba asali? Wasikie vipi walamba asali kina Mpango? Tangu lini mwenye shibe akakusikia wewe kapuku?

Kufikiria kuwafurusha kama hawatusikilizi si wazo baya. Kwani wanajinasibu kumwakilisha nani?
 
Nimeona taarifa ya Mkuu wa Mkoa Mbeya, Homera, akisema DED na dereva wake waliambiwa na polisi wa usalama barabarani wasubiri kwanza, wao wakalazimisha kwenda wakisema walikuwa na haraka.

Naona hiyo haraka yao ndio iliyosababisha mwendo kasi ulioleta ile ajali, ndio maana ile gari ya DED imechakaa vibaya sana. Hawa viongozi wa serikali waache kutumia vyeo vyao kulazimisha mambo hadi kwenda kinyume na taratibu, wataisha.
 
Katika taarifa yake kuhusu ajali ya pale Inyala Mkoani Mbeya iliyoua watu kadhaa pamoja na DED wa Igunga, Gazeti la Mwananchi limetoa...
Ila kweli kile kipande anzia ile barabara ya MPYA kutoka makambako inapoishia ni kibaya Sana na mbaya barabara ni ndogo Sana.

Labda KWa mda kuanzishwe utaratibu Kama ule wa pale kwenye mlima wa kushuka Mbalizi, magari yasubiliane KWa nusu saa Kama wafanyavyo pale
 
wapumbavu tupo wengi sana aisee.

Yaani miaka yoooote tunapambana na vitu vidogo vidogo saaana, WaAfrica tuna matatizo lakini watanzania tuna matatizo zaidi.

Viongozi wanamatatizo, wananchi wanamatatizo, CHANZO KIKUU NI POOR BASIC EDUCATION KWA WATU WOOOOTE.
 
wapumbavu tupo wengi sana aisee.

Yaani miaka yoooote tunapambana na vitu vidogo vidogo saaana, WaAfrica tuna matatizo lakini watanzania tuna matatizo zaidi.

Viongozi wanamatatizo, wananchi wanamatatizo, CHANZO KIKUU NI POOR BASIC EDUCATION KWA WATU WOOOOTE.

IMG_20220914_180443_804.jpg
 
Katika taarifa yake kuhusu ajali ya pale Inyala Mkoani Mbeya iliyoua watu kadhaa pamoja na DED wa Igunga, Gazeti la Mwananchi limetoa taarifa kwamba ajali....
Uko sahihi ila hilo la sijui TanRoads waamuliwe Kutengeneza Kwa haraka haiwezekani kwa sababu sio dharula kwamba pamezuia traffic flow ya kawaida..

Kwa nini VP ameagiza njia ya mchepuko wa dharura na kukagua Usalama wa magari sababu ni kwamba matengenezo uliyoyasemea yanahitaji gharama kubwa tena Billions of money na sio millions..

Pia hiyo barabara yote inaenda kujengwa upya kwa kufanyiwa rehabilitation na pia kujengwa njia nyingine kuwa njia 4.
 
mtaendelea kufa mpaka mtakapopeleka madereva shule.
Kuna madereva kenge,nyoka na kinyonga.
Barabarani kuna madereva 99 ni wendawazimu wewe peke yako ndo mzima.
UDEREVA WA KUJIHAMI.
jinsi ya kuovertake n.k.

Miundombinu Inaruhusu kujihami? Unajihami vp kwenye single carriage road kwenye mteremko? Gari nyingine ikifeli break na kuja kwako unaenda wapi? Unapajua Inyala au?

Common sense isn't common hakika
 
Marlezo yote haya ni hofu ya ukaguzi kwani mnabeba vitu gani?
 
Back
Top Bottom