Fast Forward
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 551
- 709
Mku wala wasikuumize sana kuwaelewesha hawa ndio sehemu ya tatizo lililopo na hawataki kusikia ushauri unaotolewa humu na wanajiamini wao ndio wenye akili na ujuzi pekee.Hebu tumia akili kidogo wewe. Yaani wewe umefikiria ukaguzi wa kuzuia ajali Inyala ni kukagua lori limebeba nini? I say kuna watu mnajifinya na kulalamika. Halafu unakuta mtu kama wewe eti unaruhusiwa kupiga kura kutuchagulia viongozi!
Mie bado nakupa mifano ya maeneo mengine ambayo ni hatari zaidi ya hapo inyala na angalia viwango vya ajali vikoje, mfano kitonga,lukumburu, K9, nk. Halafu njoo hapo kilomita chache tuu iweje ajali ziwe nyingi sana?
Ni kweli ishu ni brake tuu huko kote gari ilikuwa na brake ila ikafika inyala tuu brake zikapotea?
Ukweli ni kwamba vinavyochangia ni miundo mbinu na utumaji mbaya wa hizo brake mpaka inafikia kufeli na hasa ushukaji wa speed zaid ya 30 kwa gia za high range inasababisha brake kupata moto na ndio hilo linakuja kusikika brake zilifeli, sasa tujiulize iweje uendeshaji huu tutokomeze ili hizi ajali tuzipunguze ndio kwenye ufumbuzi na wala si kama kinacho zungumzia na viongozi wetu mbali mbali.
Napenda sana hizi ajali wahusika wa usalama barabarani wangekuwa na utaratibu mzuri wa rekodi za mahojiano na madereva husika hasa kwa wale watakaokuwa wameepuka na vifo wakieleza ukweli wa jambo husika na njia ya kuupata ukweli huo uwe kwa njia ya investigation kama zile habari za ugaidi na uhalifu wa kipekee.
Madereva wana namna yao wakikaa utawasikia wakihadisiana namna ya uteremkaji kwenye milima hiyo, haoo sasa ndio inatakiwa mchunguzaji au wachunguzaji wavae uhusika wa hao madereva wakiwa barabarani ndio watu watajua ukweli wa mambo ukoje.
Shida viongozi wetu huwa wanakurupuka sana chanzo cha tatizo huwa hakifatiliwi kwa undani, vyuo vyeti vya udereva vina msaada kwa hawa wahitimu wanaopatikana ? Au ndio tunajali tupate ada na tuoneshe tumesomesha madereva wengi lakini wametoka hawana basic knowledge ya maana?.
Je mara baada ya dereva huyo kutoka chuo kwenye hatua za majaribio ya kupata leseni watahini wanasimamia sawa sawa vigezo vya waombaji wanazo sifa na kuwa competence?
Miaka ya nyuma wako jitahidi sana kulisimamia hili na hata ilikuwa kawaida kusikia watu wanafeli kwenye kupata leseni je miaka hii haya mambo yapo?.
Kuna mahali tumeyumba sana kama taifa na sababu ni kupuuzia vitu vya msingi na haya yaliyopo ni madhara ya upuuzi huo.
Tujirekebishe tuanze upya na msasa kwa madereva wetu hauepukiki ili kuweka sawa hali ya usalama barabarani.