Kwa hili la Inyala, Mbeya ninampinga Makamu wa Rais Dr. Mpango kwa agizo lake "quick fix" na kumsihi awe serious na maisha ya Watanzania

Unalionaje agizo la Dr. Mpango?

  • Zuri linafaa sana

    Votes: 4 21.1%
  • Halifai kabisa

    Votes: 15 78.9%

  • Total voters
    19
Kwa intervention ya mda ndicho wanafanya kwamba magari yanasubiriana hata sasa lakini pia wameambiwa wafanye ukaguzi wa brake za malori kabla ya kushuka ila haieleweki kama Polisi walikagua brake au laa maana tatizo la kufeli brake lilijirudia..

VP alichosema na ambacho ni plan ya mda ya TanRoads ni ku divert malori kwenye njia nyingine Wakati wanajiandaa na kujenga hiyo barabara yote ikiwemo bypass..
 
Miundombinu Inaruhusu kujihami? Unajihami vp kwenye single carriage road kwenye mteremko? Gari nyingine ikifeli break na kuja kwako unaenda wapi? Unapajua Inyala au?

Common sense isn't common hakika
Asante Mkuu, tumeliongelea sana humu swala la kuwa na 'Runaway trucks Ramp.
Malori Duniani kote huwa yanafeli breki kwenye miteremko mikali au mirefu.
 
Inasikitisha sana jinsi tusivyoweza kuwa na majawabu sahihi huku kuna lundo la Wataalamu
Chadomo mna matatizo Sana aisee,yaani zaidi ya kuropoka sidhani kama hata mnafuatiliaga hata mipango ya Serikali zaidi kukurupuka..

Hiyo barabara inaanza kujengwa yote kutoka Igawa hadi Tunduma kuwa njia 4 na inaanza mwaka huu sio hadithi ila wanaanza kwa vipande kama Uyole hadi Airport na Mlowo hadi Tunduma..

Interventions aliyoagiza VP ni ya mda na nzuri tuu,wakishachepusha malori njia yake hakuna ajali utasikia hapo..
 

Safi kabisa, umenena vyema , hizo ndo solution zinatakiwa kuletwa na viongozi wetu!! Siyo solution rahisi rahisi tu, inasikitisha sana,,
 
Pole ndugu afadhali umesema sasa haya matatu uliyoweka hapo yanafanya sasa gari kubwa kutumia brake nyingi ambazo zinamaliza reserve ya upepo katika mitungi matokeo yake ni kufail brake. Hawa wanasiasa na polisi likitokea janga wao cha kwanza kutengeneza mazingira ya wao sio chanzo cha ajari na hawahusiki.

Kuna mjinga mmoja anaweka foleni ya malory yafatane matokeo yake kwakuwa hayana mwendo na distance kati ya lorry na lorry ni ndogo yana mwaga upepo tu ngoma likifika down halina brake. Sie wananzengo tulifikiri wangeshauri trucks ziongeze ukubwa wa mitungi ya upepo, b. yake malorry yasiwekwe katika foleni na mwisho barabara iwe na parking anayemaliza upepo aingie kushoto kujaza upepo.

Yaani polisi wanasingizia marehemu wa watu bure wakati bado ajari zinazuilika, wenye mamlaka waache politike watimize wajibu wao sio majibu mepesi kila kukicha.
 
Si wangeanzia hapo kwenye shida na mauaji ya kila siku
 

Barabara ya kudumu iliyo katika matumizi, tangu lini kuwa operated kama single lane?

Single lane isiyokuwa katika matengenezo inaingia je akilini?

Barabara yenye mteremko mrefu, kulikoni kukosekana parking in between? Kulikoni kukosekana climbing lane?
 
Iko hivi hilo eneo ajali asilimia zaidi ya 90% husababishwa na ma lories ambayo huwa Yana fail brake! Moja ya kudhibiti ajali ni kuangalia brakes kama ziko sawa! Pia njia ziwe angalau tatu au nne ! Lkn bado swala la brake ni muhimu mno! Yaani unapopita hapo lazima uwe makini na rear view na mbele na uwe unatoa maamuzi ya haraka mno!
 
Si wangeanzia hapo kwenye shida na mauaji ya kila siku
Kwa hapo sijajua ila wamekuja na hiyo intervention ya ku divert malori..

Shida ziko Hapo mteremko wa Inyala na Mlima Mbalizi,hii njia ya kusubiria imefanya Kazi kule Mbalizi huku Inyala inaonekana mlima ni mrefu zaidi ndio maana wameamua kufanya diversion ya trucks..
 
Mkuu toka miaka ya Magufuli akiwa Wazirii wa Ujenzi na Rais, serikali imenyanyapaa barabara za mkoa wa Mbeya kwa kiwango kikubwa.
Matokeo ya dhambi hii sasa imeanza kuwala hata viongozi.
 
Utaratibu kama wa Mbalizi upo pale Inyala.
Hawa wakubwa waliooata ajali walisimamishwa wakakaidi.
Wameyapata ya kuwapata.
Lakini kimsingi barabara ni mbaya mbaya mbaya mno kipande chote toka Igawa hadi Tunduma.
Serikali iko kimya kama haioni.
Wananchi wamekufa wengi hadi tumechoka kulia.
Sasa tusubiri viongozi waendelee kufa kwa wingi ili suala lieleweke.
 
Na wataisha kwelikweli haya mambo hayahitaji ujuaji...
Lakini apumzike kwa Amani.
 
Unakwepa ukweli wa mambo.
Magufuli PhD, alijenga flyover hata ziwani L. Victoria , mbadala wa kivuko cha Busisi.
Hapo ni upendeleo kwa sehemu fulani na chuki kwa sehemu nyingine.
 
Ai
Aisee kumbe, tatizo nao wakisha KUWA kwenye v8 Basi mazalau Kama yote wanaboaga sana
 
Sawa ila Kuna member hapo juu anasema walisimamishwa wakakaidi ,so ni vyema pia watu kutii SHERIA , unasimamishwa hutaki kisa ni mtu flani,sio sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…