Kwa hili la kuwasafirisha Yanga, natofautiana na Serikali

Kwa hili la kuwasafirisha Yanga, natofautiana na Serikali

Siku ya jana Jumatatu April01, 2024, baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanzania vimeripoti vikiwakariri baadhi ya viongozi wa serikali wakitoa taarifa ya kugharamia safari ya mashabiki wa club ya Yanga kwenda na kurudi nchini Afrika kusini ili kwenda kuishangilia timu hiyo itakapoumana na timu ya Mamelody Sundowns ya huko Afika ya kusini katika mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya ligi ya mabinwa Afrika unaotarajiwa kupigwa siku ya tarehe 5, April , mwaka huu.

Hapana shaka kitendo hiki cha serikali ni cha kupongeza, kwani kinaunga mkono maendeleo ya michezo na vilabu nchini.

Hata hivyo serikali ilipaswa kutafakari kwa kina kama kweli Yanga walistahili kupewa huo msaada!....Unatoaje msaada kwa mtu ambaye anaweza kufanya kazi na kutengeneza fedha kwa jasho lake lakini kaamua kutoa huduma bure alafu gharama zinapomfika anakuwa ombaomba?

Kwa ukubwa, msisimko na mvuto wa ile mechi kati ya Yanga na Mamelody ni Dhahiri hapakuwa na sababu ya kuweka kiingilio bure na Yanga ingeweza kutengeneza pesa ndefu ambayo leo hii ndio wangeitumia kugharamia hizo gharama badala ya kwenda kuomba msaada wa serikali.

Ni ajabu Serikali kila siku inazihamasisha taasisi zake kuweka mkazo kwenye kukusanya mapato na kuna viongozi wengi tu wametumbuliwa ama kwa kuzembea kukusanya mapato au kutumia vibaya fedha za makusanyo ya mapato, alafua leo hii serikali hiyohiyo inakuja kumgharamia mtu ambaye anaachia mapato yanapotea kizembe wakati angeweza kuyakusanya kirahisi kabisa kuna miradi kibao ya wananchi imekwama kwa kukosa fedha za kuiendesha.

Sikatai serikali kusaidia kugharamia michezo , hapana lakini kwa hili la Yanga kuna kitu hakipo sawa, sababu mechi hiyo ya mkondo wa pili sio ya kushtukiza, bali tangu mwanzo Yanga walifahamu fika kuwa baada ya mechi ya mkondo wa kwanza watakuwa na mechi nyingine ya mkondo wa pili hivyo walipaswa kuweka mkakati wa kukusanya fedha ili kuwezesha hilo.

Tena walikuwa na nafasi kubwa kabisa ya kulifanikisha hilo sababu kampeni yao ya uhamasishaji wa mashabiki kuja uwanjani ilifanikiwa vya kutosha, ajabu kumbe walikuwa wakitangaza kutoa huduma bure huku upande mwingine wanawaza kwenda kuikamua serikali!

Nihitimishe kwa kusema serikali ifanye tafakari upya, hapa itajibebesha mzigo wa gharama usiokuwa na sababu kwa uzembe wa watu wachache. Fedha hizo kama kweli serikali itazitoa basi tukubali tuna tatizo katika menejiment ya fedha za umma tunazozipata na hii ni mojawapo ya sababu zitakazotufanya tuendelee kukopa huko mataifa ya Magharibi mpaka mwisho wa dunia hii.
NATAKA NIWAAMBIE ALIESIMAMA HAPA N RAISI.

NENO LAKE N LA MWISHO
 
Kwa mentality za kupikia mashabiki supu na kuruhusu mashabiki kuingia bure, sahau maendeleo. Siyo yanga tu hata hao wengine nao wana uswahili.
Umefikiria hayo tu?
Vipi kwasasa ujenzi wa uwanja upo kwenye mchakato wa kuanza kujengwa.
Vipi kwasasa Yanga wana point 31 vs 39 za Simba wakati awali walikuwa na 0.5?
Vipi kuhusu Yanga kwasasa ipo katika mchakato wa kuwa ni kampuni?
Vipi kuhusu ubingwa wa NBC?

Tukiweka graph ya maendeleo basi yanga inapanda juu huku simba ikiporomoka chini na ndio maana sio ajabu kuona Whatsapp channel, na kibegi mkijisia tena kwenye mkutano mkuu kuwa ndio mafanikio yenu
 
Nyie hamkuonyesha uzalendo kama wa Yanga kuruhusu mashabiki waingie bure kutazama mechi
'Visit Tanzania' imetangazwa bure na simba karibu misimu miwili kwenye mashindano makubwa ya CAF. Je 'Visit Tanzania' haikuwa uzalendo?. Ila ni dhahiri tu serikali wanaiona uto ni timu yao wakati timu yao ni Tanzania Prison , Polisi Tanzania na JKT
 
Mnaolalamika hapa kumbukeni hapa mnazungumzia timu yenye medali za CAF kumbukeni hii ni timu iliyocheza fainali mashindano makubwa Afrika na ndiye timu yenye makombe mengi ya Ligi kuliko timu yoyote na bado inaongoza ligi kwa sasa, Msisahau hilo! Mimi ni Simba ila Serikali ipo sahihi
 
Mafanikio ya yanga yanakuwepo Mara nyingi serikali unapokuwa ya kifusadi, timu zinaporuhusu mashabiki bure huwa zinajiweza kifedha. Kama yanga waliruhusu mashabiki bure inakuwdje inakosa pesa za kumsafirisha mashabiki wake.
Ni siasa imetumika.
 
Back
Top Bottom