Kwa hili la Mbowe Marekani na Umoja wa Ulaya wamejitia aibu, ni rasmi sasa kuna kitu wanakitafuta Tanzania

polisi wamepata wapi ushahidi wa taarifa waliyoitoa?

machoni mwa Watanzania tulio wengi pamoja na wadau wa maendeleo kama USA, EU, nk ile taarifa ya polisi ni sawa na karatasi ya kuchambia tu.
 
wanasema uongo? wamesema tangu 29 haijatolewa taarifa ya mwenendo wa corovid-19, ni uongo? Kumbe nawewe ni wale wale!
Wale wale wakina nani?
Ndio Mimi nasema ni waongo tu kwasababu huu ni mwezi wa sita ndio kipindi ambacho wao walisema tutaokota maiti mabarabarani haya niambia huo ndio ukweli unao utaka??
 
Ili wajiridhishe kuwa wamepata aibu hebu waruhusuni waje wachunguze tukio hili na yaliyopita.
Kwani unafikiri wakija wao ndiyo wanajua sanaaa au? Mbona huko kwao mambo mengi tu yamewashinda? Mashahidi ni walewale waliohojiwa na Polisi wameshasema hawakusikia kelele zotezote kwa akili yako wakija hao mabeberu watakuja na mashahidi wao au? Punguza u slavery mentality.
 
Makamanda wamepigwa bumbuwazi!
Nakumbuka hadithi ya kijana aliyekuwa hapendi kuchunga mifugo, ilikuwa kila akienda machungani anapiga yowe la kuomba msaada "chui ananiua jamani! chui huyoo!" watu wanakusanyika kutoa msaada ila wanakuta hakuna chui! Mchezo ukaendelea hadi siku alipotokea chui wa "ukweli" Pamoja na kijana kupiga yowe kuomba msaada wanakijiji walidhani ni yale yale ya siku zote, kumbe chuo anamtafuna kijana!

Mkuu mleta mada acha Marekani na Ulaya waendelee kuitikia "fake alarm" hadi wachoke na siku hawa jamaa watakapotandikwa kweli. Ndio maana wengine tunajiuliza Mbowe ashambuliwe kwa lipi hasa!
Naomba TAKUKURU wamfuate hapo alipo wamuhoji maana janja ya kuwakwepa imebuma!
 
Aibu gani wakati wso walitaka uchunguzi ufanyike haraka
 
Nachelea kuamini kama polisi waliopata mafunzo vizuri wanaweza wakaandika barua ya kisiasa, ya aibu na kujidhalilisha kwa kiwango hiki.

Hii barua ni kama imeandikwa na spika halafu ikawekewa address ya/na polisi.
 
Maswali ya kujiuliuza hv mbowe hana mlinzi nyumbani kwake pili kwenye gari huwa n yeye na dereva tuu tatu mbona achukuliwi picha usoni zote anakwepesha uso tuu mwisho kwanini mnyika alisema kuwa mbowe kaumizwa vibaya na kavunjwa mguu lakini picha tunaona n POP tuu japo hata mm nlivunjika nikawekewa POP japo mie sababu n umaskini na nlikuwa sina haraka ya kupona ila kwa mbowe mambo ya chaguzi kuu yashaanza hvyo anatakiwa awe fit mapema sasa POP huchukua miezi mitatu na zaidi ili mguu kuunga vp hatoenda kujenga chama?
 
wanasema uongo? wamesema tangu 29 haijatolewa taarifa ya mwenendo wa corovid-19, ni uongo? Kumbe nawewe ni wale wale!
Taarifa ya Covid -19 itolewe ili iwe Nini?
 
polisi wamepata wapi ushahidi wa taarifa waliyoitoa?

machoni mwa Watanzania tulio wengi pamoja na wadau wa maendeleo kama USA, EU, nk ile taarifa ya polisi ni sawa na karatasi ya kuchambia tu.
Kwa suala hili ushahidi wote ukitolewa Kuna watu wataingia uvunguni kuficha sura zao kwa aibu na fedheha...mark my words..the police force has an ace in its sleeve..
 
Taarifa ya Covid -19 itolewe ili iwe Nini?
Kweli akili imehama! CCM ina dawa kali ya kuua akili za welevu! A UDSM graduate of early 80's unaongea hivyo. Waachie wa vyuo vya kata! Yale yale ya nimetoka jalalani! Nilitegemea ujibu hoja na siyo kejeli! But you aare a gentleman, huna matusi kama wenzako!

Kweli hawa wote kwenye hii link ni wapumbavu/wajinga welevu ni Jiwe and team?

Coronavirus Update (Live): 7,671,787 Cases and 426,030 Deaths from COVID-19 Virus Pandemic - Worldometer

Kwaheri ndugu yangu!
 
Unadhani hilo jipya tungelitarajia kutoka wapi mkuu, nadhani shida ni kwamba polisi wametoa majibu ambayo ni kinyume na Imani na matarajio yako mkuu.
 
Mbona wewe hujajibu hoja kwa swali langu?! Eleza tufahamu ...halafu Mimi siyo graduate...level yangu ni ya chini kabisa..
 
Dam55,

Umesahau bunge pia liliacha kazi zake na kuhamia kumjadiri Mbowe? Je, bunge letu siku hizi linajadiri tabia za watu binafsi zilizofanywa nje ya bunge?
Bunge litaacha vipi kuongea sasa wakati tukio hilo linahusishwa na serikali kwa uzushi uzushi sasa kwanini bunge lisijadili wakati watu wanavumisha uzushi wa makusudi kuchafua nchi, tena mzushi mwenyewe ni mmoja kati ya wabunge wa bunge hilo hilo.
 
wanasema uongo? wamesema tangu 29 haijatolewa taarifa ya mwenendo wa corovid-19, ni uongo? Kumbe nawewe ni wale wale!
Mkusanye wana habari, ilivyo kawaida yenu, mtembelee hospitali zilizofurika wagonjwa wa COVID-19 na/au makaburi walikozikwa, kuuthibitishia umma wa dunia kuwa Serikali inaficha ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…