Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Shida ni kwamba bado Kuna watu wenye mawazo ya kikoloni ya kuamini wazungu ndio wajuzi zaidi kuliko waafrica hapa ndio kosa lilipo nadhani na wewe pia ni mmoja wa wahanga wa hilo tatizo mkuu.
Huko kwao polisi aliye ua mtu live tena kwa makusudi kabisa ameachiwa kwa dhamana.
Ila huo uchafu wewe hajauona hata kidogo.
Picha ya alichofanya huyo polisi kila mtu kakiona, CCTV footage za hilo tukio la Mbowe umeliona? Huyo polisi huko US kaachiwa kwa dhamana maana sheria zao zinaruhusu, sio hizi sheria za hapa za kukomoana. Suala la kuwa wazungu kuwa juu kuliko sisi, na wamestaarabika kuliko sisi wala halina mjadala. Na hili sio suala la kuwasifia bali ndio ukweli. Narudia tena hakuna mzungu wa kuamini huo uchafu wa polisi, walishaamka zamani sana kwenye huo utoto.
Umejaribu kuandika mambo mengi kwenye uzi wako namba moja, ukidhani utaweza kutuchota mawazo, lakini kwa bahati mbaya tumeshaamka. Kwa huku mitandaoni ile propaganda mfu iliyoandikwa ni kama unapaka rangi upepo. Labda mkawahubirie watu huko mtaani , ambako wanawasikiliza bila ruhusa yoyote ya kuhoji.