Kwa hili la Mbunge kwenda Dubai bila kujua dhumuni la safari, Spika anatakiwa kujiuzulu!

Hii hatari
 
We mwongo, amesema wakienda Dubai kujifunza uendeshaji wa kisasa wa bandari, ila la kuuza bandari hawakulijua.
 
KUUZA nchi yetu hatutaki kabisa..Kwanza Mmetukosea sana hivi hata hawa watu mnawatoa wapi??? Yaani mtu mnatoa sijui wapi hana ushawishi wowote hajafanya la maana kwenye jamii tukaona anakuja kuwa Kiongozi ndio hayo sasa mnapelekwa huko hamjui..
 
sifi leo weka hii content hapo juu inaelezea vizuri habari yako kuliko ulivyoielezea wewe
 
Mbona sio mara ya kwanza..tushazoea.
Kama ni kweli TPA ndio umelipia safari hiyo basi ni kweli RUSHWA imetupofusha.

Na kama ni kweli Mteja wetu Mtarajiwa DPW naye aliwalipa posho watunga sheria wetu, basi kwa mara ya kwanza tumetumbukizwa shimoni
 
Sawa kabisa ni danganya toto hiyo na kweli kuna watu wamelipwa fedha nyingi kupitisha mkataba laghai kuwahi kutokea.
 
Alipewa ngapi??
 
Bado kustaafu kutokana na umri sio kipaumbele cha CCM!
Mkuu sasa mbona anawahimiza wenzake wastaafu kwa sababu umri umeenda wa zaidi ya miaka 60 maana wanapoteza kumbukumbu; maana hata yeye sasa anapoteza kumbukumbu, hakumbuki KATIBA inasemaje juu ya Wizara za MUNGANO; hakumbuki kwamba wafanyakazi wa Serikali hapaswi kuwa wanachama wa Vyama vya Siasa n.k
 
Kwa hiyo huyo mbunge yeye akiambiwa kuna safari basi anakimbilia posho tu. Anakwenda safari km mzigo hajui ht afanyalo masikini!
Sasa huyo ana uchungu na pesa zetu kweli!
Wabongo wengi wako hivyo. Haswa Watumishi wa umma
 
Hahahaha
 
Jamani mi naomba tu kujua hivi hawa waarabu watakua wanalipa sh. Ngapi kwa mwezi na sisi tulikua tunaingiza sh. Ngapi ili tujue tu kama inalipa kama mm nipo nipo tu shule sina hata sielewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…