Kwa hili la Mbunge kwenda Dubai bila kujua dhumuni la safari, Spika anatakiwa kujiuzulu!

Kuna Vituko Sana Tanzania, Mbunge Akamatwe Haraka Na Spika Wake
 
Ujumbe wako umebeba mambo mawili makuu (nadhani ndio kiini au lengo la kuleta ujumbe); katiba, na wabunge wasomi. Je, unataka kutuambia kuwa, katiba ianishe moja ya sifa ya wabunge ni kuwa wasomi? Na usomi huo uwe wa kiwango gani?
Yes katiba itamke sifa za mbunge huku kiwango cha elimu kianzie degree kwenda juu. Hii itaondoa wabunge wapumbavu bungeni ambao wanajigamba na darasa la nne na la saba lao wakati huo huo wakiugua wanaenda kutafuta madaktari bingwa wasomi hata nje ya nchi.
Pia viti maalum kwa wanawake viondolewe kwa sababu kwa sasa kila mifumo unawasapoti. Lakini pia majimbo yapunguzwe, yaani mbunge mmoja asimamie hata majimbo ma3 hii itasaidia serikali kupunguza gharama kubwa ya kuendesha hilo bunge lisiroiwajibisha serikali. Kwa namna hiyo napendekeza ndani ya bunge wabunge wasizidi 150
 
Kipindi cha jpm haya mambo ya safari aliyatupilia mbali wabunge wakaqnza kubweka ,ukisikia mama anafanya kaz nzuri I pamoja na hayo
 
Kelelee mradi wa bandari ni mzuri wacha mwalabu ajee, mutapata ajira, mbona magu alijenga Airpot chato hamukuhoji hela alitoa wapi?
 
Dada ongeza sauti tafadhali!!
 
Kwa hiyo huyo mbunge yeye akiambiwa kuna safari basi anakimbilia posho tu. Anakwenda safari km mzigo hajui ht afanyalo masikini!
Sasa huyo ana uchungu na pesa zetu kweli!
Na huyo aliyejuwa anamuhoji pia nae ni piyoyo tu. Enzi zangu mtu kama nayasindikiza maelezo yake na bonge la kibao!! Muongo zembe mkubwa!
 
Kwenda sehemu bila kujua unaenda kufanya nini tunaita ni uzururaji. Kwa hiyo, kwa maneno ya huyo mbunge walienda Dubai kuzurura huku wakitumia Kodi za wananchi wanaouziwa bandle la internet la 1000 unapata mb 300 kwa 24hrs, wananchi wanaonunua sukari 3400 kwa kilo nk. Hii ni hatari.
 
Hili bunge ni sehemu ya hasara za kitaifa. Bora DP Word wangelichukua tu
 
Ni kweli. Inasikitisha sana kuona watu wanaotuwakilisha kutamka maneno ya kutia aibu na kukatisha tamaa. Hivi kweli mbunge mzima unajisifia kuishia darasa la nne au la saba?! Hapo unawafundisha au kuwaelekeza nini wananchi wako? Mimi nadhani mbunge hata kama hukubahatika kupata elimu, huna haja ya kujisifia kukosa elimu hiyo, bali uwe mstari wa mbele kuhimiza watu waitafute elimu kwa juhudi zao zote. Elimu ni ufunguo wa maisha, hivyo kila mtu yampasa kuipata. Kama hukuipata, hiyo ni bahati mbaya sana kwako, lakini isiwe sababu ya kujisifia kuikosa. Kwa habari ya kuongeza eneo la uwakilishi, hilo ni jambo jema ikiwa mhusika (mbunge) ataweza kuhudumia eneo husika, kwani hii itaipunguzia serikali mzigo mkubwa wa kuwahudumia hawa wawakilishi wetu.
 
Pale hamna spika, Anna Makinda alishiriki kuuza gesi ya Mtwara, huyu kashiriki kupiga mnada nchi
🤣🤣🤣Tulieni vijana maana ukiona panapofuka moshi ujue Pana jambo linatendeka kwani Aya yote kama mliyaona mliwezaje kushindwa kuzuia mpk tunaingia kwenye shida kiasi hiki🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…