Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Pia hata Mimi nilishangaa kanisa katoliki kutaka kumpa utakatifu Mwalimu. Wakati alitumia uchawi wa dagoo.
Dagoo ni aina ya uchawi wa kimamlaka wa kutumia fimbo, mkia wa mnyama, ngozi za wanyama, kofia za wanyama.Lengo kuu Ili kuwa nguvu ya kutawala bila kupingwa au kusikilizwa KILA atendalo,hizi nguvu upewa na shetani.
Mfano mobutu,bokasa,nguvu yake ilikuwa kwenye mnyama chui.
Moi,iddi Amin walikuwa na fimbo za kichawi.
Zile fimbo walipoinua juu au kuweka juu ya meza mikutanoni watu wote kimya.
Odinga, kenyatta uchawi wao ulikuwa kwenye mkia wa mnyama so akipunga juu na kusema harambee! mapepo yanatoka utoka kuzimu na kuuvaa mkutano wote kuwafanya watu wamsikilize wamtii yeye tu Hakuna kupinga. Watawala wengi wa kiafrica walitumia uchawi kwa kubeba fimbo ndimo zilikuwepo nguvu zao. Na waliua watu Ili kumpa shetani damu. Shetani afanyi Kazi ya hasara anakupa pesa, madaraka lakini lazima umtolee damu.
Hittler uchawi wake ulikuwa kwenye mkono wake akiinua juu alikuwa akibadilika sura mapepo utoka kuzimu na uvamia mkutano wote na kumuona Hakuna kama yeye.
So mchakato wa kanisa kumuita mtakatifu unatia shaka ya kiimani, pili alibariki ibada za mwenge,ambao ni pure satanism, mwenge ni moto wa kuzimu kwa nia ya kuwaloga watu waweze kutawaliwa, kufungua miradi ni geresha tu.
 
Sitaki kuzungumzia maovu ya kisiasa aliyoyafanya kwa Taifa huyu mtu, maana hata ukurasa huu hautatosha, nataka nizungumzie tu maovu aliyowafanyia kanisa Katoliki na Makanisa Mengine, halafu leo hii wanaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake

Kwanza kabisa kulikuwa na mauaji na watu kupotea kulivyoshamiri mwaka 2017 Kanisa Katoliki lilitoa waraka wa kulaani mambo hayo na kuliombea Taifa lirudi kwenye mstari, alichojibu bwana huyu ni kulikejeli Kanisa katoliki na kusema kuwa halikukemea mauaji ya Kibiti (Kitu ambacho ni uongo, Kanisa lilikemea) na hata kama halikukemea kweli ndio itafanya mauaji ya watu wale kuwa sahihi? Ni mtu muovu namna gani anayeweza kuwaza hivi? Kanisa halioni aibu kumuadhimisha mtu kama huyu?

Pili, Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Kiprotestanti nao wakatoa waraka wa kukemea mauaji yaliyokuwa yameshamiri nchini kipindi kile, lakini mtu huyu alivyokuwa wa ajabu alitoa wa notisi kwa makanisa hayo kufuta waraka huo ama yatafutiwa usajili, hii ilileta sekeseke hadi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kipindi kile Mwigulu Nchemba kuondolewa

Tatu, Askofu Kakobe, aliposema kuwa Tanzania ni nchi ya vyama vingi na vyama vyote vinapaswa kupewa nafasi, askofu huyu alitukanwa na kudhihakiwa sana na vijana wa kazi wa huyu mzee, na kunyang’anywa paspoti yake na kuambiwa sio raia wa Tanzania, haikuishia hapo askofu Kakobe alitishiwa kufilisiwa mali zake na za kanisa endapo ‘asingeunga juhudi’ . Huytu ndiye mtu Kanisa Katoliki linamuadhimisha?

Nne, Askofu Niwemugizi aliposema kudai katiba mpya sio uchochezi, mtu huyu bila chembe ya aibu alimuundia zengwe kuwa sio raia wa Tanzania na akapokjonywa paspoti, japo Askofu huyu ndio alikuwa Askofu wake tangu kabla hajawa Rais..!

Tano, Kulipokuwa na Wimbi la ugonjwa Corona, mtu huyu kwa siasa zake za kilaghai akasema Corona imeondolewa kwa maombi ya siku 3, Kanisa Katoliki ambalo linajua kuwa Mungu katupa Sayansi ya kukabiliana na majanga, likasisitiza watu kuchukua tahadhari za kisayansi na kushauri Serikali ifuate njia zilizothibitishwa Kisayansi kukabiliana na hili Janga.

Kanisa lilienda mbali na kutoa takwimu za watumishi wake kama maaskofu, mapadri, masista n.k waliokufa wengi kwa kipindi kifupi kwa dalili za ugonjwa wa Covid. Mtu huyu mnakumbuka alifanyaje?

Alikejeli vibaya viongozi wa Dini na kusema wanapotosha watu kiimani, kuna kipindi aliingia kanisani na kumkejeli padre mmoja aliyekuwa anazingatia kanuni za kujikinga na Corona. Mtu huyu leo ndio Kanisa..Au linataka kumtangaza Mtakatifuu?

Nimechagua baadhi tu ambayo yalifanyika hadharani na mtu fmfuatiliji wa siasa atayajua, ila yapo mengi sana mtu huyu aliwafanyia viongozi wa Dini kama yale ya akina Mwingira, na kukamata mapadri huko Moshi, ila niishie hapa

Najua baadhi wanaweza kuteta na kusema alikuwa kiongozi mkubwa wa nchi aliyefanya mambo makubwa hivyo lazima wamuadhimishe.

Lakini Mkapa, ambaye ni kiongozi aliyekuwa na mapungufu yake pia japo hayakufikia kiwaongo hiki, alifanya mambo makubwa sana na alipofikisha mwaka mmoja tangu kifo chake, Kanisa Katoliki halikufanya chochote
Magunia alikuwa kichaa
 
Back
Top Bottom