Kwa hili la TANAPA ni lazima Waziri wa Maliasili ajiuzulu

Kwa hili la TANAPA ni lazima Waziri wa Maliasili ajiuzulu

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Poleni sana wana Mbarali,

Jana nimemfuatilia Mbunge wa Mbarali Mtega akielezea kwa huzuni kubwa jinsi Watumishi wa TANAPA walivyowatesa wananchi wa vijiji vinanvyopakana na hifadhi kwa kuwachapa na kuwavua wanawake nguo zao na kubaki uchi, kuwapiga mbuzi na mbwa kwa risasi za moto na kuwauwa.

Hii ni aibu kubwa kwa nchi na kutokana na aibu hii;

(1) Kwanza lazima Waziri wa Maliasili awajibike kwa kujiuzulu.
(2) Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA awajibike kwa kujiuzulu.
(3) Mhifadhi Mkuu wa eneo husika awajibike na ajiuzulu.

Maaskari wa TANAPA nchi nzima wanawatesa sana wananchi wanaoishi jirani na hifadhi za wanyamapori. Hii ni aibu kubwa kwa nchi na lazima hatua kali ichukuliwe na iwe fundisho kwa wengine.
 
Poleni sana Wana Mbarali. Jana nimemfuatilia Mhe. Mbunge wa Mbarali Mhe. Mtega akielezea kwa huzuni kubwa jinsi Watumishi wa TANAPA walivyowatesa...
Hivi kujiuzulu unahisi ni nyepesi sana hapo hamna hoja wananchi wanapewa pole mtu anaitwa polisi kesi kwisha
 
Poleni sana Wana Mbarali. Jana nimemfuatilia Mhe. Mbunge wa Mbarali Mhe. Mtega akielezea kwa huzuni kubwa jinsi Watumishi wa TANAPA walivyowatesa wananchi wa Vijiji vinanvyopakana na Hifadhi kwa kuwachapa na kuwavua wanawake nguo zao na kubaki uchi...
Tanapa siku hizi ni Jeshi Usu.

Maana yake ni mtarahame kaeni nao mbali
 
Hili neno labda uwe umeliandika kwa hisia na hasira tu.

Lakini wote tunajua hata dereva hawezi kujiuzuru sembuse waziri
 
Wale jamaa wanajali uhai wa tembo na swala kuliko wa binadamu
 
Madai ya Mbarali yanatia shaka, askari wameshuka na chopa wamefanya mashambulizi ya aibu kisha wakaondoka na ng'ombe zaidi ya 200 kwenye chopa!
 
Kujiuzulu nchi hii ni msamiati mgumu sana,wamezoea kufukuzwa,kuachishwa
 
Hao mbarali. Huko kila mwaka wanaambiwa watoke kwenye Hilo bonde na hawataki...shida nini?
 
Kwanza unajua Wazir wa maliasili ni nani au unajiandikia tu?
 
Back
Top Bottom