Kwa hili LATRA mmechemka

Kwa hili LATRA mmechemka

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri hapa nchini LATRA jana ilitoa waraka wa kuyafungia mabasi ya Kampuni ya Ally's Star na Katarama kwa Sababu walizozitaja kuwa Eti wanashindana kufika kwenye vituo vya Mabasi na mabasi yao kumwagiwa Maji.

Kama LATRA wangekuja na Hoja ya mabasi haya kufika kwenye vituo kabla ya wakati ningewaelewa ila kinachofanyika kwa sasa ni Ubabaishaji wa kiwango cha hali ya juu na ni nia Ovu ya kudhoofisha biashara za wenye mabasi na Biashara z wasafiri wenyewe ambao huo muda wa safafi wa saa tisa ulikua unasaidia sana. Nafikiri LATRA wanaomuda wa kujitafakari na kuwarudishia Allys na Katarama Muda wao wa saa sita wa safari.

Mabasi haya yamekuja kuleta ushindani wa mabasi ya Madaraja ya Raha (Luxury) ambapo tumeona Mikoa yote kwa sasa kuna mabasi ya madaraja ya Biashara ambapo wasafiri tumekua tukisafiri kwa Raha zaidi, na kufurahia safari zetu, hivyo Latra wamekosea, kwakua madereva wa magari haya wanatembea Mwendo ambao ni wa kawaida, wanapita kwenye vituo vya mabasi kwa muda uliopangwa hivyo Sababu zao ni za Hovyo na Kwa haraka wanapaswa kurudisha mabadi haya kuanza kufanya kazi kwa muda waliotoa kibali.
Screenshot_20230620_172748_Instagram.jpg
 
Nadhani calculation ya muda ingetumika na sio kuyazuia. Kama gari inayotoka Dar saa Tisa alfajiri na inatakiwa kupitia Morogoro saa Moja wangezingatia Hilo na kutoza faini kama watafika kabla ya muda huo. Vivyo hivyo Kwa vituo vingine kama Dodoma, Manyoni, Singida, Nzega na Shinyanga.

Walichokifanya ni kukurupuka sana
 
Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri hapa nchini LATRA jana ilitoa waraka wa kuyafungia mabasi ya Kampuni ya Ally's Star na Katarama kwa Sababu walizozitaja kuwa Eti wanashindana kufika kwenye vituo vya Mabasi na mabasi yao kumwagiwa Maji.

Kama LATRA wangekuja na Hoja ya mabasi haya kufika kwenye vituo kabla ya wakati ningewaelewa ila kinachofanyika kwa sasa ni Ubabaishaji wa kiwango cha hali ya juu na ni nia Ovu ya kudhoofisha biashara za wenye mabasi na Biashara z wasafiri wenyewe ambao huo muda wa safafi wa saa tisa ulikua unasaidia sana. Nafikiri LATRA wanaomuda wa kujitafakari na kuwarudishia Allys na Katarama Muda wao wa saa sita wa safari.

Mabasi haya yamekuja kuleta ushindani wa mabasi ya Madaraja ya Raha (Luxury) ambapo tumeona Mikoa yote kwa sasa kuna mabasi ya madaraja ya Biashara ambapo wasafiri tumekua tukisafiri kwa Raha zaidi, na kufurahia safari zetu, hivyo Latra wamekosea, kwakua madereva wa magari haya wanatembea Mwendo ambao ni wa kawaida, wanapita kwenye vituo vya mabasi kwa muda uliopangwa hivyo Sababu zao ni za Hovyo na Kwa haraka wanapaswa kurudisha mabadi haya kuanza kufanya kazi kwa muda waliotoa kibali.View attachment 2663382
Wacha Mamlaka ifanye kazi nunda wewe!! Ushindani wa spidi ilii kufika mapema ndiyo chanzo cha ajali za HOVYO za mabasi.

LATRA endeleeni na kuyafungia magari yote yanayokiuka taratibu zenu, achana na hawa wanaoshindana kuwahi kufika.
 
Nitajie Basi ambalo limepata ajali kati ya hayo ya Allys Star na Katarama! kwahivyo Kama we unapanda Ndege Panda kimpango wako, sisi tunaotumia Allys Star na Katarama tunayo haki ya kwenda na wakati. kama Kesi ingekua Spidi Vingamuzi vipo, mbona hatujaskia aliyefungiwa kwa kujaribu kukiharibu.
 
Kwahiyo ww unashauri LATRA wasubiri ikitokea ajali ndio wafungie? Watu wengine bana! Halafu hawajafungiwa Bali wamerudishiwa kwenye ratiba ya zamani ya kuanza safari saa 12 asubuhi.
Halafu LATRA ni Taasisi kubwa hivyo maamuzi yao lazima yafuate taratibu zote za haki na usawa. Ukiona wamefanya hivyo ujue hizo kampuni zimepewa maonyo mengi bila kujirekebisha! Hiv unafikiri mtu anaweza kutoka kitandani tu na matongotongo akafungie kampuni bila sababu? Think twice [emoji34]
 
Unataka kunambia HAPPY Nation wao ndio wanaendesha kwa kujichelewesha? usikute Latra wamehongwa na Happy Nation wapige ban hizo ili wao wakusanye pesa kidogo
 
Tz management tunaish kwakukomoa au kuonyesha umwamba sio kusimamia kwa Tija sehemu unayosimamia

[emoji91][emoji125]
 
Hadi sasa nashindwa kuelewa ni kwa nini wahusika wanavutiwa utaratibu wa mabasi kuanza safari kwa wakati mmoja?

Hayo yaliyofungiwa yalipangiwa kuondoka wakati mmoja. Saa tisa.
Kuondoka pamoja umeyaweka kwenye mashindano ya Marathon?

Ruhusuni mabasi yaondoke wakati wowote katika saa 24 za siku.
Mfano Katayama aanze safari saa 8 usiku.
Allys saa 9 usiku.
Kampuni nyingine zipo tayari kuanza safari mchana, adhuhuri, alasiri, jioni nk.
 
Asante sana kuniunga mkonp.

Tunawaomba wasomi wetu waonyeshe elimu zao kwa vitendo.

Dar ina wakazi zaidi ya moja ya.kumi ya watanzania wote.

Hii ina.maana kuwa, maadam jiji lina wakazi wengi, watu wanaingia na kutoka.kwa wingi.
Wanaingia wakati wote kwa njia.mbalimbali.

Badala ya kuweka mazingira ya uhuru wa kuingia na kutoka jijini wakati wowote wao wanang'ang'ania kuweka mabasi kwenye 'marathon'.
Unakuta hoteli mpja.yamesimama mabasi matano na.hata kumi.
Abiria mnalazimishwa kula kwa namna fulani ili wawahi kufukuzana.

Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar, Bw.Chalamila anawaza soko la Kariakoo na mabasi ya mwendokasi kutoa huduma kwa saa 24, kuna ambao wanataka mamia ya mabasi yaondoke kwa wakati mmoja kuelekea sehemu mbalimbali za nchi.

Hata huku vijijini, wilayani na mikoani mabasi yanayokwenda njia moja hayaanzi safari wakati mmoja.

Tafadhali, LATRA ruhusuni mabasi yafanye safari saa 24.
 
Exactly, na Kigezo cha Ulinzi Nowdays Ujambazi umekoma kwa kias kikubwa hivyo Magari yanapaswa kusafiri kwa muda wote, isipokua Waajiri wa Madereva wawe na utaratibu ambao utawezesha Safafi kuwa salama, na hatujutii kusafifi masaa 24.
 
Pia kwa Agizo la Mwigulu la June, 2023 (Budget), LATRA haina mamlaka ya kufuta leseni. Sijui hawa LATRA huwa hawaskilizi BUNGE?
 
kwani Taasisi ni Nani si watu? Taarifa yao si umeona eti wameona kwenye mitandao ya kijamii , LATRA ni watu wanaotenda, mfano Mwanza kila siku kuanzia saa tatu na nusu mabasi yote Katarama, Happy Nation, Allys isamilo yanakua yamefika, si wangefungia yote? Kwahivyo Usiwe Mbishi wanaweza kuhongeka.
 
Nadhani calculation ya muda ingetumika na sio kuyazuia. Kama gari inayotoka Dar saa Tisa alfajiri na inatakiwa kupitia Morogoro saa Moja wangezingatia Hilo na kutoza faini kama watafika kabla ya muda huo. Vivyo hivyo Kwa vituo vingine kama Dodoma, Manyoni, Singida, Nzega na Shinyanga.

Walichokifanya ni kukurupuka sana
Ila huu ni ubabaifu WA latra Kwa nini Dar na Moro iwe masaa manne!? Kweli Kuna speed limits za 50 ila usiku Sio lazima kupunguza!! Tungechukulia speed constant ya 80 kph, muda WA safari ungekuwa masaa 2 na nusu, pamoja na usalama ni Muhimu kuwe na vigezo vya mwendo wenye tija Kwa abiria, Latra wanajiona kama wakisumbua wenye mabasi ndio wataonekana wanafanya kazi, hii Sio sawa!! Wajitafakari na mawazo mgando
 
Back
Top Bottom