Kwa hili nawapongeza sana viongozi wa CHADEMA

Mawazo machafu unayojaribu kuwalazimisha wanachadema yaingie masikioni mwao,jua TU kuwa wanachama wao SII mbulila kama wale wakwenu hapo Chama chukua chako mapema 😜
Sawa swaiba, ila muwe makini huko, msijikute mnatumia nguvu nyingi kwa faida ya mwenyekiti wa chama na genge lake
 
Shida mnahangaika na chadema ambayo haipo madarakani Wala kwenye vyombo vya maamuzi halafu mnaiacha CCM yenye uwezo wa kupambana na mfumuko wa Bei ikiendelea kuboronga.
Amna mkuu, hata wao (ccm) wakibolonga huwa nawachana chana mchana kweupee.
 

Kwa hiyo Lowassa sasa hivi yuko TLP?
 
Kwa hiyo Lowassa sasa hivi yuko TLP?
Lowasa alitumwa na baada ya kumaliza kazi karudi kwa waliomtuma. CCM wajanja, waligundua kuwa mwaka 2015 wangemsimamisha Lowasa kugombea uraisi dhidi ya Ukawa ambayo ilikuwa imesham target kwa tuhuma za ufisadi, wapinzani wangeshinda uchaguzi mapema sana. Kwahiyo mwenyekiti wa wakati huo akaamua kuendesha chama ki revasi ili kukinusuru chama chao.
 

Alitumwa na jiwe? Lini Lowassa aliaacha kuutaka urais? Nyie si ndiyo mnaodai pia kuwa Mbowe na hata Lissu ni makada wenu?

Mengine haya danganyaneni Lumumba huko!
 
Alitumwa na jiwe? Lini Lowassa aliaacha kuutaka urais? Nyie si ndiyo mnaodai pia kuwa Mbowe na hata Lissu ni makada wenu?

Mengine haya danganyaneni Lumumba huko!
Jiwe hakuwa mwenyekiti wa chama na wala hakuwa na nguvu yoyote ndani ya chama wakati huo. Aliekuwa mwenyekiti wa chama, na magwiji wenzake wa kisiasa wa chama hicho ndio waliamua kumchomoa Lowasa baada ya kuona kashfa zake zingeweza kumkwamisha kushinda uraisi. Kwa vile jiwe na yeye hakuwa mwanasiasa wa kuweza kusimama ulingoni na Dr Slaa ambae alikuwa na uzoefu wa mambo ya siasa, ndo ukasukwa mpango wa kwenda kuivuruga Ukawa ili CCM ipite na baada ya kupita Lowasa arudi akaendelee na maisha yake kama alivyofanya. Hili swala kama unatumia akili yako vizur kutafakari niliyoandika na yaliotokea utauona ukweli, ila kama utasubiri kile atachoongea mwenyekiti wako ndo ukisikilize basi usitarajie kuujua ukweli wowote ule kutoka ndan ya kinywa chake.
 

Umemkosa aliyemtuma Lowassa ukawa. Umeshindwa kuonyesha kuridhia kwa Lowassa kwenye agenda hiyo.

Umeshindwa kuonyesha Slaa alikuwa vipi kwenye mpango huo wala vipi au lini Slaa naye alitumwa ukawa.

Umeshindwa hata kukumbuka kuwa Slaa aliondoka ukawa kwa kususa au hata kwa nini alisusa.

Usisahau mtanzania wa leo siyo wa enzi zile.

Ninakazia Lumumba danganyaneni wenyewe huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…