Kwa hili nimemuelewa na naungana na Waziri Mwigulu Nchemba

Umemwelewa nini ? Mwigulu ametumia mifano ambayo inatoa huruma kwa serikali huku akijua alichokisema Mpina ndicho kinaleta mfumuko wa bei. Nilitegemea aeleze ni namna gani atapunguza mgumuko wa bei.
Mwigulu kataja masuala mawili.
1. Matumizi nje ya bajeti ambalo ndilo kuu
2. Mfumuko wa bei nchini.

Mpina amedai matumizi ya pesa nje ya bajeti yamesababisha mfumuko wa bei nchini.
Sasa bunge na sisi makabwela tumeulizwa je, ujenzi wa madarasa 8000 umesababisha mfumuko wa bei?
Pili kuwalipia ada vijana wetu chuo kikuu(mkopo) kunaweza kusababisha mfumuko wa bei nchini?
Hayo mawili ndiyo aliyokiri kuwa serikali ilifanya matumizi nje ya bajeti lakini Kwa agizo la Bunge.

Mjadala uko wazi tuendelee kujadili.
 
Madarasa 8000 ni Bei gani?
 
Sasa bunge na sisi makabwela tumeulizwa je, ujenzi wa madarasa 8000 umesababisha mfumuko wa bei?
Mabati, saruji, nondo, tiles, madirisha ya vioo yanahitaji kwa pamoja kila kijiji kina madarasa sio chini ya 4 yanayojengwa na viwanda ni vile vile na uzalishaji ni ule ule oda zinakuwa nyingi uzalishaji uko chini nini kitafuata ndio saruji kuuzwa 22,000 huko mikoani hapo mfumko wa bei haujaongezeka? msikilize kwa makini mpina usimchukie kwa sura yake angalia hoja yake
 
Mwigulu kataja masuala mawili.
1. Matumizi nje ya bajeti ambalo ndilo kuu
2. Mfumuko wa bei nchini.

Mpina amedai matumizi ya pesa nje ya bajeti yamesababisha mfumuko wa bei nchini.
Sasa bunge na sisi makabwela tumeulizwa je, ujenzi wa madarasa 8000 umesababisha mfumuko wa bei?
Pili kuwalipia ada vijana wetu chuo kikuu(mkopo) kunaweza kusababisha mfumuko wa bei nchini?
Hayo mawili ndiyo aliyokiri kuwa serikali ilifanya matumizi nje ya bajeti lakini Kwa agizo la Bunge.

Mjadala uko wazi tuendelee kujadili.
Amekwepa hoja. Alichokisema Mpina hajakikanusha wala kukijibu.

Ametafuta huruma kwa wananchi tu.
 
Hoja za Mpina kwenye hiyo issue anayojibu Mwigulu zilikuwa nzito sana, Mwigulu ameishia kutoa majibu ya kutafuta huruma kwa kuwatumia "watoto wa masikini" bila kukumbuka nae anawaumiza hao masikini na tozo zake za ajabu.

Mpina alisema; " huwezi uka control mfumuko wa bei kama usimamizi wako wa bajeti hauko sawa.Bilion 350 tumemlipa Symbion fedha ambazo haziko kwenye bajeti, lakini pia, kama huwezi kupeleka fedha zilizopangwa kwenye maeneo husika hasa kwenye sekta muhimu kama kilimo, ambapo jana tumeambiwa mpaka kufikia February, ni 17% ya fedha ndizo zilizopelekwa, uta control vipi mfumuko wa bei?

Mwigulu ndio alitakiwa kujibu hilo swali bila kuwaingiza "watoto wa masikini" kwa sababu umaskini sio sifa, lakini pia nae hawahurumii kwa tozo zake.
 
Mwigulu kataja masuala mawili.
1. Matumizi nje ya bajeti ambalo ndilo kuu
2. Mfumuko wa bei nchini.

Mpina amedai matumizi ya pesa nje ya bajeti yamesababisha mfumuko wa bei nchini.
Sasa bunge na sisi makabwela tumeulizwa je, ujenzi wa madarasa 8000 umesababisha mfumuko wa bei?
Pili kuwalipia ada vijana wetu chuo kikuu(mkopo) kunaweza kusababisha mfumuko wa bei nchini?
Hayo mawili ndiyo aliyokiri kuwa serikali ilifanya matumizi nje ya bajeti lakini Kwa agizo la Bunge.

Mjadala uko wazi tuendelee kujadili.
Mkuu asante kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom