MoureenAbel
Member
- Sep 24, 2021
- 29
- 43
Jana Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/22, serikali imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 5.151, ikiwa ni asilimia 94 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 5.462.
Kiwango hicho cha makusanyo ni ukuaji wa asilimia 17.4 ikilinganishwa kwa kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita.
Rais Samia mara tu baada ya kuingia madarakani alinukuliwa akisema kuwa hata ukusanyaji wa kodi kwa mabavuu, na kwa mantiki hiyo serikali imefanikiwa kukusanya kiasi hiki ambacho hakijawahi kufikiwa kwa miaka mitano iliyopita kwenye kipindi hicho pasi na kutumia mabavu. Kwa hili Rais anastahili pongezi kwani huu ni mwanzo mzuri ambao utachochea watui wengi zaidi kulipa kodi kwa hiari.
Jambo kubwa ambalo sasa linabaki ni kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya kiasi hicho kilichokusanywa. Wananchi wakiona kuna value for money, hawatosita kulipa kodi zaidi. Value For Money ndio hufanya nchi za magharibi wananchi wake wanakuwa na mwamko wa kulipa kodi, ambazo ndio tunakopeshwa au kupewa kama misaada.