Kwa hili, Rais Samia apongezwe

MoureenAbel

Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
29
Reaction score
43
Jana Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitangaza kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/22, serikali imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 5.151, ikiwa ni asilimia 94 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 5.462.

Kiwango hicho cha makusanyo ni ukuaji wa asilimia 17.4 ikilinganishwa kwa kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita.

Rais Samia mara tu baada ya kuingia madarakani alinukuliwa akisema kuwa hata ukusanyaji wa kodi kwa mabavuu, na kwa mantiki hiyo serikali imefanikiwa kukusanya kiasi hiki ambacho hakijawahi kufikiwa kwa miaka mitano iliyopita kwenye kipindi hicho pasi na kutumia mabavu. Kwa hili Rais anastahili pongezi kwani huu ni mwanzo mzuri ambao utachochea watui wengi zaidi kulipa kodi kwa hiari.

Jambo kubwa ambalo sasa linabaki ni kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya kiasi hicho kilichokusanywa. Wananchi wakiona kuna value for money, hawatosita kulipa kodi zaidi. Value For Money ndio hufanya nchi za magharibi wananchi wake wanakuwa na mwamko wa kulipa kodi, ambazo ndio tunakopeshwa au kupewa kama misaada.
 
πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ

Takwimu za kupikwa
 
Hakuna kodi isiyokusanywa kwa mabavu. Hata Yesu mwenyewe alipodaiwa kodi alilalamika, lakini alilipa kwa vile alitaka wasimsumbue, sembuse mfanyanyabiashara au mwananchi anayekatwa tozo za miamala.
 
Tumpongeze Pia Commissioner Kidata..Jamaa Ni mtu mzuri anajua sana Kazi..Ila ndio hivyo nchi hii watu wazuri hupigwa vita sana.

Brain kama ya Kidatta majungu yangemmaliza.
 
Hakuna kodi isiyokusanywa kwa mabavu. Hata Yesu mwenyewe alipodaiwa kodi alilalamika, lakini alilipa kwa vile alitaka wasimsumbue, sembuse mfanyanyabiashara au mwananchi anayekatwa tozo za miamala.
Kodi iliyokwepwa ndiyo hukusanywa kwa mabavu. Kulalamika kuwa umelipa kodi kwa hiyari yako ili usikutane na mkono wa sheria au usisumbuliwe hiyo siyo mabavu. Kama wewe ni nfanyabiashara utakuwa unajua tofauti ya hizi awamu mbili.
 
Tanzania my beautiful katriiiiii
 
Kila siku nawaambia humu kwamba kama ni ishu za Chuki binafsi kwa Samia ni sawa ila kwa rekodi za Uchumi kwa mda aliokaa hakuna wa kumlinganisha.























 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…