McDonaldJr anapotajwa DIAMOND acha kumtolea mfano na vitu vya ajabu.Angalia hii tofauti ;-
-Familia nzima ni brand (bongo hakuna mwingine)
----Mtoto wake alipata ufadhili mkubwa.(haijawahi kutokea)
----Nyimbo zake ni za taifa,itajadiliwa mno na kuvunja rekodi zake mwenyewe (mfano hii)
-----Ni msanii aliyepata TUZO nyingi mno kwa Afrika mashariki kama si Afrika nzima.
-----Ni msanii aliyefanya Shoo nyingi mno E.A.
------Ni msanii anayependwa zaidi E.A.
------Ni msanii ambaye nyimbo zake zinachezwa zaidi E.A.
------Ni msanii ambaye LEBO yake ipo juu zaidi kuliko wote E.A.
------Ni msanii ambaye kaingia kwenye orodha kama mmoja wa Icon ya taifa.
------Watu wake wa karibu ni maarufu kuliko watu wa msanii yeyote E.A. kuanzia mameneja wake,Dancers wake, wapiga picha wake,Designer wake, Bodyguard wake,Mama yake, Dada zake, Baba yake, Mtoto wake na zaidi wapenzi wake.
-------Ukimtaka DIAMOND kibiashara utamkuta kwenye Boooonge la ofisi yake si Bar wala barabarani (hakuna kwa E.A)
--------Kaajiri vijana wengi sana zaidi ya 40+ (hakuna msanii mwingine E.A.)
--------Keshatoa michango/misaada mingi sana kwa mtu mmoja mmoja hadi vikundi (hakuna kwa bongo)
----------Ni msanii anayelipwa pesa ndefu E.A.(hakuna mwingine)
-----------Ni msanii mwenye ubalozi wa makampuni mengi na yenye pesa ndefu kuliko na haijawahi kwa msanii yeyote kwa E.A.
--------Ni msanii mwenye muonekano wa ki super star haswa sio kama muuza njugu wa Buguruni.
--------Atakapo tokea yeye ni lazima asababishe foleni na shuguli kusimama kwa muda kokote E.A.