Kwa hili Yusuph Manji atatisha

Tresor Mandala

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Posts
40,905
Reaction score
86,203
...Katika pita pita zangu mitandaoni nimeona hii Habari inayomuhusu mwenyekiti wa Yanga .Yusuph Manji...kutaka kuanzisha mashindano maalumu ya Kupambana na EBOLA...na yeye manji atatoa kiasi cha dola 500,000/=

..Kilichonifanya mpk kuleta hii mada hapa nikuwa wazo hilo limepelekwa moja kwa moja ..katika UMOJA WA AFRIKA AU...

...SOURCE..:
....SONDACOM

[h=2] YUSUF MANJI AONYESHA JEURI YA FEDHA, AMWAGA MILION 900 MBELE YA MARAIS WA AFRIKA [/h] Posted by edward michael On 10:46 PM | No comments
mfanyabiashara Yussuf Manji wiki iliyopita alikuwa sehemu ya msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete uliokwenda Addis Ababa, Ethiopia kwenye Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU).Na akiwa huko, milionea huyo mwenye asili ya Kiasia, ambaye bila ya yeye kwa sasa ‘Yanga haipumui‘ ametoa msaada wa dola za Kimarekani 500,000 kiasi cha Sh. Milioni...
 
Si bora angelitoa msaada pale Muhimbili kununulia dawa na vifaa tiba! Ama angeweza kulipia bima ya afya kwa familia masikini, ama angelinunua madawati kwa shule za Dar ambazo watoto wanakaa chini.

Kweli vipaumbele vinatofautiana!
 
Tatizo si kuwa na MALI, tatizo ni UNATUMIAJE MALI ZAKO.
 
Hapa Tanzania wamama hawana vifaa vya kujifungulia yeye anapeleka pesa nje ya nchi, bure kabisa huyo anatafuta sifa nje ya nchi!
 
Hapa Tanzania wamama hawana vifaa vya kujifungulia yeye anapeleka pesa nje ya nchi, bure kabisa huyo anatafuta sifa nje ya nchi!

Peleka za kwako kwa hao akina mama. Kama huna uwezo wapo watoto wanasoma primary bila ya kuwa na viatu, unaweza kuanza na hao. Viatu kwa mmoja haizidi Tsh. 20,000/= tu ambayo naamini unayo. Ukifanya hivyo, sasa unaweza kumnyooshea Manji kidole. Anza na boliti katika mboni yako kisha utatoa kibanzi katika jicho la Manji.
 
Msimhukum Manji kwa anavyotaka kufanya huo ni uamzi wake na ni hela zake.serikal yetu inatapanya mamilioni ya shilingi wameshindwa kuyaona hayo matatizo?
 
Pesa Za Wale Wachezaji Wa Kenya Ameshamaliza Kuwalipa? Uwanja Wa Yanga Aliowaahidi Upo Wapi? Mrisho Ngassa Sasa Analia Njaa Je Ameshamlipa? Kocha Wa Makipa Pondamali Hajalipwa Mshahara Kwa Miezi 3 Sasa Je Manji Atamlipa Lini? Wachezaji Wa Yanga Wanalala Ghettoni 4 wa 4 Kwa Kukosa Pesa Ya Kodi Je Manji Atawasaidia Lini? Manjia Anawazuga Tu Bali Anawatumieni Ili Ajijenge Zaidi Kisiasa Kwani Mwaka Huu Amejipanga Anataka Kugombea Ubunge Jimbo La Kigamboni Na Yanga Kwake Ndiyo " Stepping Stone ".
 
Ngasa analia njaa kwa ujinga wake mwenyewe, na hilo litakuwa fundisho kwa wajinga wengine,umesahau kuwa viongozi wenu walikula rambirambi ya Mafisango(R.I.P)
 
Mkuu inaonekana leo hujasuguliwa sawsawa, pole.
 
Ngasa analia njaa kwa ujinga wake mwenyewe, na hilo litakuwa fundisho kwa wajinga wengine,umesahau kuwa viongozi wenu walikula rambirambi ya Mafisango(R.I.P)

Mkuu Umenikumbusha Mbali Na Natokwa Na Machozi Sasa Kwani Huyo Marehemu Alikuwa Ni Kipenzi Changu Na Alikuwa Ni Mtu Wa Watu. Ila Je Na Wewe Umesahau Yanga Walivyomchimbia Mtu Nusu Mchangani Baharini Bagamoyo Wakati Wa Mechi Ya Simba Na Yanga Ile Mliyopigwa 5 - 0 na Tulipowafunga Mkamsahau Baharini Na Maji Yalipojaa Yakamfunika Na Akafariki Na Mkaahidi Kuilinda Familia Yake Lakini Kilichotokea Mpaka Leo Mmeitelekeza Hiyo Familia. Najua Wewe Hujui Jambo Hili Ila Mtafute Mwenyekiti Wako Wa Mashindano Na Maandalizi Wa Yanga Mdau Wangu Mohamed Binda Atakuelezea Vizuri Kwani Masuala Yote Ya Uganga Kwa Timu Ya Yanga Anayaratibu Binda Na Yule Mtunza na Mbeba Jezi Wenu Jamaa Mmoja Hivi Ana Kibyongo.
 
Si bora angelitoa msaada pale Muhimbili kununulia dawa na vifaa tiba! Ama angeweza kulipia bima ya afya kwa familia masikini, ama angelinunua madawati kwa shule za Dar ambazo watoto wanakaa chini.

Kweli vipaumbele vinatofautiana!

Kweli watz tuna akili finyu sana!!!!
 
.....aseee pamoja na mambo yote hayo watu wa kala 5-0
 
Ni sawa na Asilimia 0.1 ya PESA aliyoKWIBA EPA. What makes a diffence to him ?
 
Si bora angelitoa msaada pale Muhimbili kununulia dawa na vifaa tiba! Ama angeweza kulipia bima ya afya kwa familia masikini, ama angelinunua madawati kwa shule za Dar ambazo watoto wanakaa chini.

Kweli vipaumbele vinatofautiana!

usimpangie mtu msaada au matumizi ya pesa zako we kwa huruma yako ulishawapelekea hata catton moja ya sabuni na juice,kwani umeambiwa huko ilikopelekwa hkuna wahitaji??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…