Kwa hoja ya Rais Mama Samia, ninadhani hoja ya Dkt. Kigwangalla tulitumia rungu kumdhibiti

Kwa hoja ya Rais Mama Samia, ninadhani hoja ya Dkt. Kigwangalla tulitumia rungu kumdhibiti

Kuhusu Kigwangala na hoja zake Mimi nilieleza hivi.

KAMA KIGWANGALA NI MNAFIKI BASI WATANZANIA WOTE NI WANAFIKI.

Inashangaza kuona watu wengi wakimsakama mh. Kigwangala Kwa kutoa maoni yake kuhusu chanjo ya COVID 19 . Maoni ambayo ni tofauti na yale aliyoyatoa enzi za Magufuli (Mwenyez Mungu ampunguzie adhabu za kaburi)

Katika akaunt yake ya Twitter mh. Kigwangala amechapisha maoni kuhusu mtazamo wake juu ya chanjo ya ugonjwa huo akisema " Ni lazima Tanzania ijitazame sasa na iingie kwenye orodha ya nchi zinazotakiwa kupata chanjo ya COVID".

Watu wengi wamemshukia Kigwangala Kama mwewe wakihoji juzi tu wakati wa JPM alisisitiza matumizi ya nyungu katika kukabiliana na CORONA, iweje Leo ghafla abadili na kutoa maoni tofauti?

Wapo ambao wamekwenda mbali zaidi na kumtusi mh. Kigwangala Kwa kumuita mnafiki Kwa kitendo chake cha kuigeuka nyungu na kuipigia chapuo Chanjo dhidi ya CORONA.

Pengine wapo wengine wanajiuliza je Kigwangala angeweza kutamka maneno haya Kama JPM angekuwepo? Jibu ni rahis tu kwamba asingeweza.

Kimsingi sitaki kubisha au kukubali endapo mh. Kigwangala ni mnafiki au la lakin napinga vikali kutimia mitazamo yake hii miwili tofaut kuhusu CORONA kumuhukum kuwa ni mnafiki.

Sababu za kukataa kuhusisha maoni haya tofauti ya kigwangala na unafiki ni Kama ninavyozijadili hapa chini.

Mosi ni hadhi na mamlaka ya rais. Wakati Kigwangala anashaur na kusisitiza kuhusu "Nyungu" tayar mh. Rais alikwishatoa toa au kuonyesha msimamo wa kuamini zaid nyungu kuliko chanjo. Hivyo Kigwangala alikuwa anasisitiza msimamo wa rais na Kwa vile kauli ya rais ni Sheria na mtazamo wa rais ndio mtazamo wa taifa Kigwangala alikuwa sahihi kabisa. Lakin pia Rai's ana vyanzo vingi vya utafit hivyo haikuwa lazima Kigwa atafit naye ili kupata uhalali wa mtazamo wa rais.

Kwa sasa tuna Rais mwingine hiyo inafanya mitazamo na kauli za rais aliyepita kukosa nguvu na Kwa kuwa rais aliopo madarakani bado hajatoa kauli rasmi kuhusu mtazamo wake juu ya chanjo au nyungu basi kila mtu anawajibu wa kutoa maoni yake kuhusu chanjo lakin rais Samia akishatoa kauli kuhusu chanjo au nyungu basi anakuwa amefunga mjadala.

Pili ni aina ya rais tuliyekuwa naye wakati Kigwangala anasisitiza nyungu. Hapa sitaweza kujadili sana lakin ipo mifano ya watu wachache waliotaka kwenda kinyume na kauli ya rais Kwa nia njema au mbaya lakin wote ni mashahidi nini kiliwapata. Rejea tukio la uvamizi wa clouds na harakat za mh. Waziri husika wa wakat huo.

Tatu ni akili ya mwanadam. Mwanadam hajaumbwa Kama jiwe bali ameumbwa Kwa namna ambayo mitazamo yake hubadilika kulingana na sababu kadha wa kadha. Na ndio maana wakati fulani unaweza kusema Una Imani na Lowassa na wakat fulani ukasema ikulu sio wodi wagonjwa Kwa kumlenga Lowassa huyo huyo ambaye ulisema juz tu kwamba Una Imani naye. Au kesho unaweza kumuunga mkono mtu ambaye Jana ulimlaani.

Lakin pia katika hoja namba tatu hii hii ,, hivi karibuni tumeshuhudia watu wengi wakipoteza maisha Kwa kile kilichoitwa kwamba " changamoto ya upumuaji" japo wapo wengi pia waliohusisha vifo hivyo na madhila ya CORONA. Hapa inaleta ishara kwamba upigaji nyungu haujaleta mafanikio Kama tulivyotarajia hivyo watu wenye akili timamu Kama Kigwangala wameona ni vema kuwaza tofauti.

Nihitimishe Kwa kusema Kigwangala yupo sahihi sana na Kama ni unafiki basi sisi wote ni WANAFIKI.
 
Back
Top Bottom