Nsanzagee
JF-Expert Member
- Jun 28, 2023
- 2,209
- 4,769
Kitendo cha Sekeretaliet ya bunge kukubali kuwa mkataba unamapungufu, hii imewaongezea credit kubwa wote waliokuwa wakipinga mkataba huu na kuwapunguzia heshima wote waliokuwa wakishabikia mkataba!
Ieleweke hivi! Watu wanapinga mkataba na siyo wawekezaji! Wawekezaji waje na mikataba rafiki, na watia saini watumie vema akili zao kwa manufaa ya watanzania wote, huko nyuma, tumewahi kuingia mikataba mingi ya kijinga na imeendelea kutugharimu kama watanzania!
Viongozi wetu popote pale walipo, sasa wajue, Tanzania italindwa na watanzania na leo siyo jana tena! Tumelizwa vya kutosha!
Watu wameitwa kila aina ya majina! Suala la udini nalo halikuachwa nyuma utadhani udini ni chakula!
Ni vyema sasa mtu ukitaka kuongea jambo, ujiridhishe kwanza kama unachotaka kusema, kina ukweli, kitakuletea heshima iwapo hakitakuwa kama ulivyotarajia ama kitakuvunjia heshima na kudharaulika
Kwa hoja ya shekhe mwaipopo! Awaombe msamaha hao viongozi wa dini na awaite ni watanzania wapigania nchi na maliasili zake
Lakini kwa hoja za wananchi, basi Tanzania imeshinda, kinyume kabisa na ambavyo baadhi ya viongozi wa dini fulani wao walilinasibisha jambo hili la DPword na mkataba wenye utata kuwa ni la watu wa dini fulani wanampinga Mh Rais kwa kuwa siyo Mkirsto
Kwa mara nyingine tena, imedhihirika kuwa, Watu waliosoma, wamesoma tu, watu werevu wataendelea kuwa werevu tu,
Tuwaombe sana wasomi wa nchi hii kutoka kada mbalimbali, wasichoke kuwabeba wajinga na wasiogope kuandamwa na hoja dhaifu za kidini pindi yanapotokea mambo yenye utata kama hili la mkataba wa DPWORD
Mwisho wa siku hata hao wajinga waseme asante kwa msaada wenu
Na hili liwe funzo kwa wote wasiotaka hoja ishindanishwe na hoja na badala yake, kwa akili zao ndogo hukimbilia udini!