Kwa hospitali za hapa Tanzania mtu aliyevunjika mguu njia nzuri ni kuwekewa chuma au muogo ili apone haraka?

Kwa hospitali za hapa Tanzania mtu aliyevunjika mguu njia nzuri ni kuwekewa chuma au muogo ili apone haraka?

BUSHMEN 88

Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
25
Reaction score
31
Habarin wanajukwaa

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada yapata mwezi mmoja na nusu uliopita nilipata ajali ya bodaboda na kuvunjika mguu wa kushoto mara mbili yani mfupa wa nyuma na mbele na daktari niliyeonana baada ya kumuonyesha picha ya mionzi akanishauri ili mguu uweze kukaa sawa ni lazima niwekewe chuma ingawa mimi nilimuomba niweke muogo ukizingatia kipato nilichonacho ni kidogo kulinganisha na bei yakuwekewa chuma.

Basi kulingana na ushauri wa kitabibu ikabidi nikubaliane nae kwamba nitaweka chuma ngoja nikajichange upya baada ya siku mbili kupita nikawa nimepata hiyo pesa na kufanyiwa operesheni.

Cha ajabu baada wiki tatu kufanyiwa operesheni nikawa nakanyagia mguu na wiki ya nne niliweza kutembea vizuri tu nakuweza kuvaa kiatu sasa swali langu linakuja je kuwekewa chuma ni njia salama zaid au ni mwili wa mtu na kinga alizonazo au vyakula ukizingatia wenzangu wengine tuliokuwa nao pamoja bado wapo kitandani na wengine bado awajaanza kukanyagia mguu.
 
Habari!

Kuna mambo mengi ya kuzingatia kwenye nini kifanyike baada ya mtu kupata mvunjiko wa mfupa:

1: Aina ya mfupa husika
2: Aina ya mvunjiko
3: Kiasi cha mvunjiko
4: Upatikanaji wa teknolojia
5: Upatikanaji wa vitendea kazi
6: Gharama na uwezo wa mhusika.
7: .........nk.

Kwenye suala la kupona pia kuna mambo mengi ya kuzingatia:

1: Aina ya mvunjiko
2: Kiasi cha mvunjiko
3: Njia ya urekebishaji
4: Umri wa mhusika
5: Afya ya mhusika kabla na baada ya ajali
6: Lishe baada ya mvunjiko
7: Uanzaji wa kujongea/mazoezi baada ya mvunjiko
8: Aina ya mfupa
9:........nk.
 
Back
Top Bottom