Kwa huu utitiri wa ajali Hayati Magufuli aliwahi kumtumbua Waziri

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nakumbuka Magufuli aliwahi kupewa maneno magumu sana baada ya ajali kuongozana kwa wingi. Unaweza usione mantiki ya uamuzi ule lakini ukweli ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uongozi unaolegalega na ajali ambazo zinaondoa maisha ya watu kila siku.

Inaniuma sana kusikia karibia kila siku iendayo kwa Mungu Watanzania wenzetu wanakufa kwa ajali na wengine kupata ulemavu wa kudumu uharibifu mkubwa wa muda na mali huku mamlaka husika zikisalia mabubu.
 
Waziri ndiyo ameendesha hayo magari? Ajali zipo kila mahala hp duniani madereva wafuate taratibu za uendeshaji magari. Yale mabasi yanajulikana kwa speed hasa Asante Rabi, cha ajabu abiria ndiyo wanafurahia.
Kwa hiyo waziri pale anafanya kazi gani
 
Yaani madereva wanaedesha magari wakiwa wamelewa na hawafuati sheria za barabaran halafu mnataka waziri ndo awajibike! ?
 
Ajari zimekuwa nyingi, inawezeka askari wa barabarani hawafanyi kazi kwa weledi maana ajari nyingi sababu ni mwendo kasi

ushauri kwa madereva wazngatie sheria na wasitumie vilevi
 
Mm nikiwa rais, Kila ajari inaondoka na RPC, rto, ocd, dto na asikari wote iliyowaoita ikiwa na makosa.

Nikiwa rais, ujambazi WA kutumia siraha yakiwemo mapanga nafukuka kazi RC, RPC, RSO, RCO, DC, OCD, DSO.

Sheria kali zikiwabana wakubwa wadogo watazifuata tu.
 
Yaani madereva wanaedesha magari wakiwa wamelewa na hawafuati sheria za barabaran halafu mnataka waziri ndo awajibike! ?
Waziri haponi kwenye hayo mambo sababu yeye ni msimamizi wa utekelezaji wa sera na Sheria kwa maslahi ya umma analipwa kwa kazi hiyo!! Kwa nini wasimamizi wa Sheria wapo!?
 
Kwa Sasa tuna rais mbovu sana haijawahi kutokea.ajali zimekithili sana lakini yeye hajali chochote.Anachojua yeye ni kurembua macho tu lakini kuwawajibisha wateule wake hakuna.Uuaji umetokea mchana kweupe wa mzee kibao hakuna hatua amechukia zaidi anachekacheka na kukejeli kwa mumwita kibao ni sisimizi.
 
Waziri haponi kwenye hayo mambo sababu yeye ni msimamizi wa utekelezaji wa sera na Sheria kwa maslahi ya umma analipwa kwa kazi hiyo!! Kwa nini wasimamizi wa Sheria wapo!?
Tatizo waafrica hujazoea kujusimamia wenyewe mpk tusimamiwe ndio maana unaona ni sawa t kumuajibisha waziri apo
 
Hakuna nchi duniani watu wanajisimamia wenyewe nenda china ukavunje Sheria kama huta liwa kichwa!!
 
Sw hamna ila ukienda china hukuti utitizi wa ajali zinazosababishwa na ulevi na uzembe wa madereva tena usafiri wa umma!!
 
Nakumbuka Magufuli aliwahi kupewa maneno magumu sana baada ya ajali kuongozana kwa wingi. Unaweza usione mantiki ya uamuzi ule lakini ukweli ni kwamba kuna uhusiano mkubwa sana kati ya uongozi unaolegalega na ajali ambazo zinaondoa maisha ya watu kila siku.

Inaniuma sana kusikia karibia kila siku iendayo kwa Mungu Watanzania wenzetu wanakufa kwa ajali na wengine kupata ulemavu wa kudumu uharibifu mkubwa wa muda na mali huku mamlaka husika zikisalia mabubu.

Sheria inabidi zifuatwe ,madereva inatakiwa wawe wawili ,elimu itolewe kwa madereva.

1.Same - Dereva alikuwa amesinzia ,sheria inataka kwenye long route dereva wawe wawili ,akichoka mmoja anampa mwingine.

2.Ajali ya Mwanza - Dereva aliovertake bila kuchukua tahadhari - reckeless driving.
 
Ajari zimekuwa nyingi, inawezeka askari wa barabarani hawafanyi kazi kwa weledi maana ajari nyingi sababu ni mwendo kasi

ushauri kwa madereva wazngatie sheria na wasitumie vilevi
Tusikwepeshe maneno ni kwamba mamlaka zilizowekwa kusimamia mambo ya usalama barabarani hazitimizi wajibu wake hivyo mambo yanaenda kiholela tu lazima waziri awajibike
 
Back
Top Bottom