Pre GE2025 Kwa huu utitiri wa miradi aliyomwaga Rais Samia mkoa wa Mwanza, angekuwa anatokea kanda ya Ziwa wapinzani wangesema anapendelea kwao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kumbe ndio sababu Wanasiasa hawakatiki huko 😂😂

Kwa hiyo sisi wa Njombe
Mwanza ni kitovu na tegemeo kwa mikoa ya kanda ya ziwa magharibi , siasa ya mwanza ukiacha wao kua wengi zaidi ya milioni kama 20 , lakini Kura ya mwanza hupigwa pia Kagera, kigoma, mara, tabora, simiyu, shinyanga, geita, hao wote hutegemea mwanza na kidogo katavi
 
Na ili kuwatuliza kanda ya ziwa unatakiwa uwatulize hivo na ndio maana uliona makonda wakati anafanya ziara mwanza , alisema wazi mara, shinyanga, Kagera, geita, simiyu, na kigoma Tabora ni kwao kwa maana ni mikoa ya kimkakati kwa kanda ya ziwa yote, na Kura za hiyo mikoa huamua lolote , tazama wanavoifungua kigoma , geita, utaelewa jambo
 
Mbeya ilibeba hatma ya nyanda za juu kusini lakini ubishi umewatoa mchezoni serikali imebaki inaangalia kwenye maslahi kama Njombe , Ruvuma , Iringa , na mbeya kuendekeza siasa ndio imewafikisha hapo imebaki kidogo akina tulia wanapambana kivyao japo watu wa mbeya wabishi na hawana shukrani
 
Kanda ya kati dodoma na singida wao hawana maneno wametulia na uvivu wao kila mwaka labda waanze kuwasapoti viongozi wao kwa nguvu kubwa maana wanabahati ya kupata mawaziri karibu kila awamu lakini deliverance ndio zero
 
Kanda ya kati dodoma na singida wao hawana maneno wametulia na uvivu wao kila mwaka labda waanze kuwasapoti viongozi wao kwa nguvu kubwa maana wanabahati ya kupata mawaziri karibu kila awamu lakini deliverance ndio
 
Kanda ya mashariki Dar tegemezi, kinachotokea Dar basi Moro kitafika , pwani kitafika , hao hawana shida wanafanyiwa mengi japo kwa Dar mambo ya siasa wananchi hawataki kabisa maana wanakimbizana na maisha kila kukicha
 
Wapiga kura karibu 20% wanatoka MWANZA haijalishi uko wapi wasukuma ni WENGI sana nchi hii hata kama wapo dar ila nyumbani ni nyumbani na wanaangalia maendeleo ya mkoa wao. Sasa ukijichanganya kwenye uchaguzi kazi unayo
 
Lengo ni kuinasa ngome ya Kanda ya ziwa, ni kama ilikuwa CCM wameanza kupoteza ushawishi.

Na ndio sababu ya Dotto Biteko kutokea kanda ya ziwa kuwekwa makamu wa Waziri Mkuu
 
Kanda ya kaskazini Arusha , Tanga , Manyara, Kilimanjaro huko kitambo wanafaidi mema ya nchi toka enzi ya mwalimu Arusha akiwa kinara na kumpeleka makonda pale ni makusudi Mazima japo ukiacha tanga ambayo CUF ilikua imetakeover lakini Arusha na Kilimanjaro ni wapinzani wa asili pamoja na hayo wako eneo lenye faida kwa nchi , mererani, Kilimanjaro na mbuga za wanyama bado zinawabeba serikali kuona aibu , idadi ya wageni wanaoingia pale na kuacha dolari nyingi ndio unakua mwendo wa serikali kuharakisha maendeleo huko
 
Kwa muda mrefu maendeleo mwanza iliachwa nyuma. 2005 Mwanza lilikua Jiji la pili Kwa ukubwa TANZANIA ikiacha nyuma Arusha na Dodoma lakini hivi sasa Arusha na Dodoma wako mbele ya Mwanza Kwa ukubwa na maendeleo. Airport ya Mwanza ilikua kituko, Barabara ni vituko.

Kuona uthubutu aliofanya mama, kwangu Mimi nimefajirika na licha ya Kwa muda mrefu kutomkubali, Kwa maendeleo haya Mimi nafikiria kumpa kura yangu ya NDIO
 
Orodha ya miradi kibao, utekelezaji wake ni siasa tupu. Ni bora mngeweka mnayoiweza, sio list lirefu huku utekelezaji ni chini 50%.
 
Wapiga kura karibu 20% wanatoka MWANZA haijalishi uko wapi wasukuma ni WENGI sana nchi hii hata kama wapo dar ila nyumbani ni nyumbani na wanaangalia maendeleo ya mkoa wao. Sasa ukijichanganya kwenye uchaguzi kazi unayo
Wasukuma pekee yao Wana mikoa ya Mwanza, Geita , Simiyu, Shinyanga, Tabora, Acha wale ambao wako lindi , mtwara, chunya, ifakara, sumbawanga, mpanda, uvinza, kibondo, bahi, handeni, ubaruku, madibila , kwa idadi ya watu wako wengi wanaa athari Sana , chadema alilegea ngome imeshachukuliwa jumla na CCM walivo wajanja hawataki utani na Kura za kanda ya ziwa na ziwa magharibi na ndio sababu hua tunasema Tanzania upinzani hakuna
 
Inaonesha wazi upo kitengo cha propaganda, huwezi kumhadaa anayejielewa kwa data za uongo

Kawadanganye wengine wasio ijua mwanza!.
 
Kanda ya ziwa ndiyo inawatu wengi and so is the number of votes. Ukitaka kushinda u-Rais Tanzania bila kutumia nguvu nyingi basi kaa vizuri na wasukuma
 
Yes alafu huwaga wanaga mambo mingi wao kwenye uchaguzi lazima wavote hata bibi kizee anatumia fimbo lazima a vote sasa kwa uchunguzi wangu niangalia karibu 95% ya wapiga kura kanda ya ziwa ni wanaccm na karibu majimbo yote Ccm inashinda Kwa 97.9% ispokuwa nyamagana tu ndio kunaonekana Kuna upinzani walikuwa wanaondoka na 75% baada ya mabula kuingia nyamagana now kufanya makubwa Ccm wamejua 99% kanda ya ziwa mtu atakae win Kanda ya ziwa huyo ndio anaetoa president hiyo haipingiki 100% chadema wamezubaa sana.. ndio maana kuna wale walikuwa wanajiita sukuma gang walikuwa wanajiamini mno sababu kubwa ni nguvu ya wasukuma kama chadema wanataka kuwin Ccm Hawa budi kuiteka Kanda ya ziwa miji vijiji na vitongoji vyake japo 60%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…