Uchaguzi 2020 Kwa janja hii ya CCM kutumia ugeni wa kitaifa kuomba kura NEC semeni jambo

Uchaguzi 2020 Kwa janja hii ya CCM kutumia ugeni wa kitaifa kuomba kura NEC semeni jambo

onjwayo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2020
Posts
1,356
Reaction score
1,309
CCM kupitia mgombea wake wa urais Sasa wanatumia janja janja ziara na ugeni wa kitaifa kufungua miradi na kuomba kura. Ratiba ya Magufuli inasema ana pumziko kwa muda wa siku 10 na kuendelea baadaye. Lakini leo hii na muda huu anatumia nafasi yake Kama rais kufungua miradi na hapo hapo kuomba kura.

Balance ya fairness iko wapi, hawa wenzake kina Lissu wanawekewa barrier kila Kona. Hawatakiwi hata kutembelea mashina yao na kudhibitiwa kila wakionekana kujumuika katika shughuli either kiuchumi au kijamii. Ni Lini katika kipindi chote viongozi wa nje ndio wawe wanatuwekea jiwe la msingi kwenye miradi yetu? Na kwa Nini atumie nafasi hiyo kuwaombea kura wagombea wake na yeye kujiombea kura.

Wito kwa NEC, kwa kuwa huyu anayo advantage hiyo Basi wengine nao mazingira yawaruhusu kutumia fursa itakayojitokeza.
 
Tume ya Uchaguzi NEC, Tume ya Maadili Uchaguzi na Msajili wa Vyama tunauliza kama ni halali kwa Rais Magufuli kutumia ziara ya ujio wa Rais Dr. Lazarus Chekwera wa Malawi kupiga Kampeni?

Kwenye Uwekaji wa Jiwe la msingi Ujenzi wa Mbezi Mwisho Bus Terminal Rais Magufuli ameomba Kura kwa Kuwatambulisha Wagombea wa Ubunge na Udiwani kwa majimbo ya Dar!

Lakini pia Rais Magufuli ametamka wazi kuwa yeye ati ndiye mshindi wa Ugombea Urais Tanzania!! Sijui ametumia kigezo gani ilhali Uchaguzi bado na kura hazijapigwa!!!

Kama NEC muko makini na muko Huru kama mnavodai tunaomba Mgombea w Urais CCM awajibishwe kwa kukiuka Maadili ya KAMPENI.
 
Labda stendi hiyo inajengwa kwa fedha toka Malawi ndugu...

Inawezekana ukitazama pembeni kidogo mwa stendi hiyo labda utaweza kuona bango kubwa lenye maandishi;

"....MRADI HUU WA STENDI HII UNAJENGWA KWA MSAADA WA FEDHA ZA WATU WA MALAWI - MABEBERU...."

Kama ndivyo, ni haki ashiriki kuweka jiwe ka msingi kwa sababu fedha za wananchi wake ndizo zinajenga stendi yetu...!!!
 
Mgombea mwenyewe ana asili ya nchi jirani so no wonder
 
Very Interesting.., ChiChiem Wameshikwa Makalioni so they have to use all Mbinu na Janja Janja otherwise Maandiko yako Ukutani kila mtu anaweza yasoma ChiChiem Bye..Bye.. Bye..Bye.. mmoja Kapigwa Ban na Tume HURU YA UCHAGUZI, mwingine Kapewa nafasi ya Kupumzika na Kuamua afanye nini kwa muda Mhafaka.....Daaa!! only in Bongo .But all in all CCM must go....
 
Eti Lissu anaenda Kariakoo kutafuta mahitaji kwa kupanda mwendokasi. Wanatuona wote wajinga kweli
 
Unatambua kuwa Magufuli bado ni Rais wa Tanzania.

So, Unataka hii Miradi izunduliwe baada ya kampeni/uchaguzi..Huku ni Kupoteza muda.

Acha Magufuli aendelèe kutimiza Majukumu yake kama Rais.

CHADEMA mbona mnaonesha Weakness mapema.
T. Lissu

Leo anakuja kukata ticket hapa Terminal Ubungo.

then anaenda kununua Ndizi Mabibo.LoL[emoji23][emoji23]
 
Pamoja na yote hayo, wamechelewa sana. Hawawezi kuathiri uamuzi wa wapiga kura kwa sasa. Hadi sasa zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura wamesha kuamua nani watampa kura.
 
Upuuzi mtupu kudhani shughuli za kiserikali zina ukomo kipindi cha kampeni.
Mkuu ukiweka ushabiki wa kivyama pembeni kisha ukafikiri kwa makini basi utagundua kuwa tunae Kiongozi aliyepungukiwa Hekima na Busara.

Haya yote ni kuwadhalilisha wale aliowateua hasa Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kwakuwa tu ni yeye aliyewateua.

Haya anayoyafanya hivi sasa yangeweza kufanyika kabla au baada ya Uchaguzi.
 
Hiki nini tena?! Yaani Rais wa nchi aache kufanya na kutimiza majukumu na kazi zake za Kitaifa kwa sababu ya kampeni za uchaguzi!? Kweli, are you guys serious!?

Juzi kaja Rais wa Uganda mbona hamkusema hili, au kwa vile hili linafanyikia hapa Dar-es-Salaam? Sielewi unataka NEC waseme nini, kwani sheria, kanuni na taratibu zinazuia hili!? Jibu ni HAPANA. Huyu ni Rais wa JMT hadi hapo atakapoapishwa Rais mwingine.
 
Upuuzi mtupu kudhani shughuli za kiserikali zina ukomo kipindi cha kampeni.

Swali ni Je, leo JPM alikuwa na ratiba ya kampeni Kibamba?

Kama hakuwa na ratiba hiyo then why ameomba kura akiwa kwenye eneo ambalo kiratiba za NEC hakupaswa kuwa hapo?
 
Hiki nini tena?! Yaani Rais wa nchi aache kufanya na kutimiza majukumu na kazi zake za Kitaifa kwa sababu ya kampeni za uchaguzi!? Kweli, are you guys serious!? Juzi kaja Rais wa Uganda mbona hamkusema hili, au kwa vile hili linafanyikia hapa Dar-es-Salaam? Sielewi unataka NEC waseme nini, kwani sheria, kanuni na taratibu zinazuia hili!? Jibu ni HAPANA. Huyu ni Rais wa JMT hadi hapo atakapoapishwa Rais mwingine.

Uwe unasoma na kuelewa hoja sio unakurupuka tu!

Ratiba ya JPM kwa maswala ya kampen ni kuanzia tarehe tisa

Na Leo kwa ratiba za nec mgombea urais wa ccm Hana ratiba Kibamba

Imekuwaje yy Leo kwenye Eneo la Kibamba anafanya kampen?

Hiyo ndio hoja
 
Back
Top Bottom