- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimeona poster mbalimbali zinazoonesha kuwa Lissu kwa jicho hilo hawezi kutoboa, je caption hiyo imeandikwa na mwananchi?
- Tunachokijua
- Makamu Mwenyekiti Taifa wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, Tundu Lissu alitangaza nia yake ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hiko tarehe 12/12/2024 kutokana na uongozi uliopo hivi sasa kuelekea kumaliza muda wake chini ya mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe.
Tarehe 17/12/2024 Lissu alichukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti katika ofisi za chama Mikocheni, Dar es salaam na baadaye tarehe 18/12/2024 alirudisha fomu hiyo katika ofisi hizo hizo.
Mara baada ya Lissu kurudisha fomu hizo kuekuwapo na grafiki zinazosambaa mitandaoni zenye nembo ya grafiki za mwananchi zikiwa na picha ya Lissu na Benson Kigaila (naibu katibu mkuu taifa, CHADEMA) huku zikiambatana na maandishi ‘Caption’ mbalimbali kama vile;
“Kwa Jicho hili Lissu kutobo labda atoboe suruali”
“Kwa jicho hili Lissu atasubiri sana”
“Kwa jicho hili Lissu ataelewa kwa nini nyimbo ya Taifa haipigwi disco”
“Kwa jicho hili Jicho la mwana ukome”
“Kwa jicho hili Lissu atajua kwa nini kisigino hakikai mbele”
“Kwa jicho hili Lissu ndiyo atajua ile kauli inasema heshima pesa shkamoo makele”
Baadhi ya taarifa hizo zimehifadhiwa hapa, hapa na hapa.
Uhalisia wa grafiki hizo upoje?
JamiiCheck imefuatilia uhalisia wa grafiki hizo na kubaini kuwa zimepotoshwa na hazikutolewa na kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za gazeti la mwananchi. Kwa kupitia ufuatiliaji wa kimtandao na google image reverse tumebaini kuwa grafiki hizo zimepotoshwa kwa kuhaririwa maneno kutoka kwenye grafiki halisi zilizotolewa na kurasa za mitandao ya kijamii ya gazeti la mwananchi.
Gazeti la mwananchi walichapisha grafiki mbili kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii ikiwemo X na instagram tarehe 18/12/2024 zenye picha ya Lissu na Kigaila zikiambata na ujumbe kwenye grafiki hiyo ukisomeka;
“Lissu arejesha fomu, Mbowe kuzungumza na makada nyumbani kwake” taarifa hiyo imehifadhiwa hapa.
Ufuatiliaji pia umebaini mapungufu katika grafiki zinazopotosha ikiwemo kutumia muandiko ‘font’ ambazo ni tofauti na zinazotumiwa na gazeti la mwananchi kwenye grafiki zake za mitandaoni.